Episode 12: HARUFU YA KIFO NA TOBA YA MACHOZI
Alfajiri ilipofika, mkoa Y ulikuwa umetanda ukungu mzito. Tulijikuta tukiwa kwenye kituo cha mabasi, tukiwa tumekata tiketi za kuelekea kijiji cha mbali cha *Mundindi*, mahali alipotoka Suleimanβdereva mkuu wa Juma aliyekufa kwenye ajali ya kwanza ya Fuso.
Juma alikuwa amevaa koti langu la zamani, kofia imefunika uso wake uliojaa hofu. Kila mara alikuwa akigeuka nyuma. "Mwanangu msimulizi, unahisi harufu ya dizeli? Nasikia harufu ya mafuta ya gari kila mahali!"
Mimi sikuwa nasikia harufu yoyote, lakini nilihisi baridi isiyo ya kawaida iliyokuwa inatoka kwenye koti la Juma. Tulipopanda basi, watu walioanza kukaa karibu nasi walianza kuhama mmoja baada ya mwingine. "Hapa kuna harufu kama ya hospitali au mochwari," nilimsikia mama mmoja akinong'ona akiziba pua.
Tulipofika Mundindi, hali ya hewa ilikuwa ya huzuni. Tulielekezwa nyumba ya akina Suleiman, ambayo ilikuwa ya nyasi na udongo, ikionyesha umaskini wa kutupa. Nje ya nyumba hiyo, mwanamke mmoja mzee alikuwa amekaa juu ya mkeka akichambua maharagwe.
Alipotuona, alisimama polepole. Macho yake yalikuwa na huzuni ya miaka mingi. "Karibuni wageni. Je, ninyi ndio mmekuja kuniletea habari za mwanangu? Tangu azikwe mwezi ule, sijawahi kuona hata rafiki yake mmoja aliyekuja kunifariji."
Juma alianza kutetemeka. Alipiga magoti pale pale kwenye vumbi, mbele ya yule mbibi. "Mama... mimi ndiye Juma. Mimi ndiye niliyekuwa tajiri... mimi ndiye niliyekuwa bosi wake Suleiman."
Yule bibi alimtazama Juma kwa muda mrefu. "Juma? Yule uliyemnunulia Suleiman suti ya kuzikwa lakini hukuonekana kwenye msiba? Suleiman alikupenda sana kijana wangu. Alisema wewe ni bosi mzuri, unajituma..."
"Hapana mama!" Juma alipiga yowe la uchungu, akijipiga kifua. "Suleiman hakufa kwa ajali ya kawaida! Nilimuua mimi! Nilienda kwa mganga, nikapewa masharti... mali zangu zilikuwa zikinywa damu ya watu wangu wa karibu! Suleiman alikuwa kafara yangu ya kwanza!"
Ukimya mzito ulitawala. Hata kuku waliokuwa wakizurura uwanjani walionekana kutulia. Yule mbibi aliangusha ungo wa maharagwe, akamtazama Juma kama anaona shetani.
"Ulisemaje?" Sauti ya yule bibi ilikuwa ya kutetemeka.
"Nilimuua kwa tamaa yangu ya utajiri! Magari yote yale, nyumba ile... kila kitu kilitokana na roho yake! Naomba uniue mama, nichinje hapa hapa nilipe deni la mwanao!" Juma alikuwa akigaragara vumbuni, akilia kama mtoto mdogo.
Neema alimkaribia yule bibi na kumshika mkono. "Mama, Juma amepoteza kila kitu. Hana hata senti moja. Amekuja hapa ili nafsi yake ipate amani, na ili roho ya Suleiman iache kumtesa."
Ghafla, upepo mkali ulianza kuvuma uwanjani hapo. Kile sanduku la mbao lililokuwa kwenye begi la Neema kilianza kutoa sauti ya *Taka-taka-taka!* Funguo za Fuso zilijitokeza zenyewe na kuanguka miguuni mwa yule mbibi.
Mbibi yule alitazama funguo zile, kisha akamtazama Juma. "Mwanangu Suleiman alikuwa mhimili wa nyumba hii. Tangu afe, tumekula mlo mmoja kwa siku. Hata wajukuu zake wamefukuzwa shule."
Alinyamaza kidogo, kisha akavuta pumzi ndefu. "Juma... ungekuja hapa na pesa, nisingekusamehe. Ungekuja hapa na sifa, nisingekusikiliza. Lakini umekuja hapa ukiwa huna kitu, ukiwa na vumbi na machozi... unataka nifanye nini?"
"Nisamehe mama... nisamehe!" Juma alikuwa akilia kwa kwikwi.
Yule mbibi aliinama na kumshika Juma kichwa. "Mungu akusamehe mwanangu. Mimi ni binadamu tu, sina nguvu ya kutoa roho wala kurudisha roho. Lakini kwa kuwa umekiri dhambi yako mbele yangu na mbele ya ardhi hii... nenda kwa amani. Nakuachilia."
Wakati huo huo, zile funguo za Fuso zilizokuwa miguuni mwa yule bibi zilianza kutoa moshi mweupe na kuyeyuka kabisa, zikawa majivu. Harufu ile ya dizeli na uozo iliyotoka kwa Juma ikatoweka papo hapo. Juma alihisi kama mzigo mkubwa umetoka mabegani mwake, akavuta pumzi ya kwanza ya amani baada ya muda mrefu.
Lakini walipokuwa wanageuka kuondoka, sauti ya kikatili ilisikika kutoka porini karibu na nyumba ile.
"Umesamehewa na mwanadamu, lakini mikataba yangu haivunjwi na machozi ya bibi kizee! Juma, bado unanidai!"
Ilikuwa ni sauti ya yule Mganga wa jalalani, ikirindima kupitia kivuli cha mti wa mwembe. Juma alipigwa na butwaaβMganga alikuwa amekufa kule kijijini, sasa huyu alikuwa nani?
**Je, Mzee Kalumanzila amerejea kivingine? Na deni ambalo halijalipwa ni lipi?**
**Usikose Sehemu ya 13...**

Matangazo
Matangazo