Episode 7:
Tukiwa tumelala kwenye kile kitanda kikubwa, giza la usiku wa kijijini lilikuwa zito, likisindikizwa na sauti za wadudu wa usiku nje ya dirisha. Kelvin alikuwa amegeukia ukutani, lakini niliweza kuhisi kuwa na yeye hapakuwa amepata usingizi. Kila akigeuka kidogo, moyo wangu uliruka hatua moja.
Baada ya kama saa moja ya ukimya uliotawaliwa na mawazo, Kelvin aligeuka na kunitazama. Ile taa ndogo ya kando ya kitanda ilikuwa ikimulika nusu ya sura yake, akionekana kuwa na huzuni fulani.
"Tasha, bado hujalala?" aliniuliza kwa sauti ya kunong'ona.
"Usingizi umekataa, Kelvin. Akili yangu bado inawaza mambo mengi," nilijibu huku nikijivuta blanketi kifuani.
Kelvin alivuta pumzi ndefu. "Unawaza kuhusu milioni mbili, au unawaza jinsi utakavyotoroka hapa kesho asubuhi?"
Nilitabasamu kidogo gizani. "Nawaza kuhusu wewe, Kelvin. Una kila kituβpesa, sura, heshima, na familia nzuri. Lakini mbona unaonekana mpweke kiasi hiki? Yaani, ni kweli lile 'dude' lako limekupa upweke kiasi hicho?"
Kelvin alikaa kitandani, akasogea na kuegemea mbao za kitanda. "Tasha, tangu nikiwa mdogo, nilikuwa tofauti. Hali hii kwetu ni ya kurithi; babu yangu mzaa baba alikuwa hivi hivi. Hata baba yangu... ingawa mama hatasema, najua alipitia magumu mpaka kunizaa mimi."
"Kurithi?!" Nilishangaa. "Kumbe ni ukoo mzima?"
"Ndiyo. Lakini tatizo ni kwamba, mimi nimezidi wote. Nilipokuwa shuleni, nilikuwa naogopa hata kuoga bafu la jumuiya na wavulana wenzangu. Nilipokua na kuanza mahusiano, kila mwanamke aliyeniona uchi alikimbia. Wengine walidai nina 'majini', wengine walisema nimefanya 'ndumba' za utajiri ambazo zimeniharibu maumbile."
Nilihisi huruma ikianza kutawala moyo wangu. "Pole sana Kelvin. Sikuwahi kuwaza kuwa kuwa na 'mali nyingi' hivyo inaweza kuwa laana badala ya baraka."
"Ni laana, Tasha. Pesa ninazo, lakini siwezi kumpata mwanamke atakayenipenda kwa dhati bila kuogopa kifo kitandani. Ndiyo maana nakwenda klabu, natafuta wanawake ambao nidhani ni 'shupavu', ninalipa pesa nyingi nikitumaini mmoja atavumilia... lakini wapi. Hata wewe, pamoja na ubishoo wako wote wa klabu, ulinirudishia laki yangu na kukimbia," alisema akicheka kwa uchungu.
Niliketi na mimi, nikamsogelea kidogo. "Kelvin, siyo kwamba hatukupendi. Ni binadamu tu anaogopa kitu kinachozidi uwezo wake. Lakini hapa nyumbani, mbele ya mama yako, nimeona upande mwingine wa Kelvin. Wewe ni mwanamume mzuri sana."
Kelvin alinitazama machoni. Mkono wake ulisogea taratibu na kushika kiganja changu. Safari hii, sikustuka wala kuvuta mkono wangu. Ule ubaridi wa awali ulianza kuyeyuka.
"Tasha, unajua mama anaamini wewe ndiye utayeyusha 'barafu' ya moyo wangu? Amefurahi sana kukuona. Na mimi pia... kusema kweli, tangu nikuone klabu ukifyonza ile soda kwa mapozi, nilihisi kuna kitu tofauti kwako."
Tulikaa kimya kwa muda, tukiangaliana. Ghafla, Kelvin alinisogeza karibu naye. Nilihisi joto la kifua chake. Akili yangu ilipiga kengele: *"Tasha! Kumbuka mchi wa kutwangia karanga! Kumbuka lile dude!"* Lakini moyo wangu ukasema: *"Huyu mwanamume anahitaji faraja."*
Kelvin aliniinamia, akataka kunibusu. Nilifunga macho, nikiwa nimechanganyikiwa kati ya hamu na hofu. Lakini kabla midomo yetu haijakutana, mlango wa chumba ulipigwa hodi kwa nguvu!
"Kelvin! Kelvin mwanangu! Amkeni!" Sauti ya Mama Kelvin ilisikika kwa nje, ikiwa na wasiwasi mkubwa.

Matangazo
Matangazo