📖 Story Tamu

Episode 11:

Nilihisi kama nimepigwa na radi ya mchana kweupe. Mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio, na jasho jembamba likanitoka licha ya baridi ya asubuhi ile. Nilimtazama Kelvin, ambaye uso wake ulibadilika kutoka kwenye tabasamu la mahaba na kuwa na mshangao uliochanganyika na shaka.

"Mume?!" Kelvin alitamka kwa sauti ya chini, akiniangalia kama mtu asiyeniamini tena. "Tasha, huyu mama anasema nini? Una mume mjini?"

"Hapana Kelvin! Sio kweli!" nilijitetea, lakini sauti yangu ilikuwa inatetemeka.

Tulishuka kwenye gari kwa unyonge. Pale mlangoni, kando ya Mama Kelvin, alisimama mwanamume mmoja mfupi, mweusi, aliyevaa shati la kitambaa lililochoka na suruali ya kitambaa iliyopwaya. Alikuwa amevaa miwani iliyopasuka upande mmoja. Aliponiona tu, akaanza kupiga kelele.

"Ehee! Ndiye huyu huyu! Tasha! Unafanya nini huku kwa huyu mwanamume? Yaani unatoroka na laki tano zangu za mtaji wa duka la mkaa, unakuja kujificha huku mkoani?" yule mwanamume alifoka huku akijifanya kulia.

Kaka yake Kelvin, yule mwenye dharau, akacheka kwa kejeli. "Nilijua tu! Kelvin, nilikuambia huyu ni mdau wa mjini. Ona sasa, mume wa mtu kaja mpaka huku kijijini kwetu kutafuta haki yake. Aibu gani hii jamani?"

Mama Kelvin alikuwa ameshika kichwa, akionekana kusikitika sana. "Tasha mwanangu, kumbe wewe ni mke wa mtu? Na mimi nilikupokea kama mwanangu wa damu..."

Niliwakumbuka watu hawa. Yule mwanamume aliitwa Juma 'Mkaa'. Hakuwa mume wangu, bali alikuwa ni mmoja wa "mabuzi" niliyowahi kuwachuna kule mjini miezi sita iliyopita. Tulicheza naye mchezo wa "pata potea" klabu, nikamchota laki tano nikasepa. Lakini alijuaje niko hapa? Na nani alimleta?

"Kelvin, nisikilize..." nilimshika Kelvin mkono, lakini akautolea nje kwa hasira.

"Tasha, kumbe kule klabu hukunidanganya kusema wewe ni 'muigizaji'? Kumbe maigizo yako ni ya maisha yako yote?" Kelvin alisema kwa sauti iliyojaa uchungu. "Ulinambia unanipenda, kumbe ulikuwa unatafuta pa kujificha kwa sababu ya madeni yako?"

"Hapana Kelvin! Huyu siyo mume wangu! Ni tapeli tu!" nilipiga kelele.

"Tapeli?!" Juma Mkaa aling'aka. "Hii hapa picha yetu tukiwa chumbani kwangu, na hii hapa barua ya madai niliyofungua polisi!" Alionyesha picha moja tuliyopiga klabu tukicheza, lakini katika mazingira ya giza ilionekana kama tuko chumbani.

Hali ilikuwa tete. Kijiji kishaanza kukusanyika mlangoni. Kelvin aligeuka na kuelekea ndani ya nyumba bila kuniangalia tena.

"Kelvin! Kelvin subiri!" nilijaribu kumfuata, lakini kaka yake aliniziba njia.

"Ondoka hapa wewe mwanamke tapeli! Rudi kwa mumeo kule mjini. Kelvin hataki kukuona tena, na pesa zake milioni mbili sahau! Rudi mkamalizane na mumeo wa mkaa!" kaka yake alinisukuma kwa dharau.

Nilibaki nimesimama pale uwanjani, nimechanganyikiwa. Nilimtazama Juma Mkaa, ambaye alikuwa ananikonyeza kwa mbali kama anayejua siri fulani. Hapo ndipo akili ilinikaa sawa. Juma Mkaa ni maskini, hawezi kupata nauli ya kuja huku, na hawezi kujua niko wapi. Kuna mtu alimlipa kuja hapa kuniharibia.

Niligeuka na kumtazama kaka yake Kelvin. Alikuwa anatabasamu kwa ushindi.

"Wewe ndiye uliyemleta, au siyo?" nilimnong'oneza kaka yake Kelvin kwa hasira.

"Huna ushahidi mrembo. Sasa sepa kabla sijaamuru vijana wa kijiji wakutoe kwa fimbo!" alijibu kwa dharau.

Niliamua sitaondoka hivi hivi. Kelvin ni wangu, na lile "dude" lake nimeshalizoea, siwezi kuliacha kwa sababu ya mkaa! Nilijua lazima nifanye kitu kimoja kikubwa ili kuthibitisha ukweli, hata kama nitapata aibu gani mbele ya mama yake.
Matangazo
Matangazo