Episode 7:
"Mimi leo sijisikii kutembea, naumwa tumbo."
"Sawa, twende zahanati kama unaumwa."
"Mmh..." nikaona nikubali tu. "Sawa, tutaenda baadae."
Mama chai ikaiva tukanywa chai tukashiba, nikawaacha na mama wanaongea mimi nikaingia chumbani kwa mama kukagua alivyotuletea. Mmh alileta mafuta, kiti cha lita tano, mafuta ya kupaka, sendo, vitenge... vitu vingi sana alileta.
"Amina! Amina!"
"Abee mama!" Nikatoka kumsikiliza mama.
"Ebu nenda na mwenzio mkanunue nyama, ila mbali sijui ataweza kutembea."
"Mama nitajitahidi nitaweza." Yaani mama kwa nini ananilazimisha kutoka mimi naogopa! 🤗🤗 Nikakubali kishingo upande, mama akanipa hela tukatoka nje.
"Baraka twende na gari, ni mbali huwezi kufika."
"Hapana, mimi nataka nikijue kijiji chenu."
Basi nikawa sina cha kufanya ila roho iliniuma sana. Tukaanza safari mdogo mdogo, tulivyofika sokoni watu waliacha mambo yao wakawa wananiangalia. Nikitaka kugusa kitu natukanwa, Baraka akawa anashangaa tu. Jamani wakatokea mashoga zangu wako watatu wakaja kwa mbele yangu.
"Tunaona umepata hawala, sasa huyo utampa sehemu gani wakati kote kumetumika? 😭😭"
"Hivi huyu bwana umemwambia kwamba umetumika kotekote?"
Jamani niliishiwa nguvu nilitaka kukaa chini, Baraka akanishika akanisogeza kifuani kwake.
"Sikilizeni ninyi mabinti, maana nahisi ni wivu tu unawatesa. Kaniambia kila kitu kinachomhusu, hata hayo mnayoyasema kaniambia. Ninachowashauri, muda unaotumia kumnyanyasa mwenzenu ni vyema mngetulia nyumbani mpate mabwana wanaojielewa. Kwa mimi, wanawake wa staili yenu siwezi owa mwanamke ambaye hampendi mwanamke mwenzake, siwezi oa. Kwa hiyo itaishia kushangaa hivyo hivyo."
Jamani ngoja kwanza, ile amani moyoni mwangu iliyopotea miaka mitatu nyuma nikajikuta imerudi. Nilimkumbatia kwa furaha nikamwambia, "Nikubalie niwe mke wako, nami nakupenda! 💋💋💋"
💋💋 Baraka hakuchelewa, akatoa pete mfukoni akapiga magoti akanivisha mbele ya mashoga zangu. Jamani walinuna! 🤣🤣 Mimi moyoni raha tu.
"Na wewe mama upo kwenye biashara halafu hutaki Amina asogee kwenye vitu vyako? Amina, wanaouza wako wengi twende kwa mtu mwingine, hela ni yetu! 🏃🏃🏃"
Matangazo
Matangazo