📖 Story Tamu

Episode 6:

"Tunaona umetoka kwa Amina?"

"Ndio."

"Vipi umempenda?"

"Ndio nataka niwe shemeji yenu."

"Mmmh hivi unajua history yake?"

"Hapana."

"Daaaah ila poa bora umuoe utuondolee hii laana."

"Kwani anashida gani?"

"Wewe oaoa tu kopo hilo si umempenda, endelea."

Wale vijana wakaondoka wakamwacha na maswali Baraka, akawa anajiuliza, "Nina tatizo gani mpaka wanakijiji wenzangu hawataki hata kuniona?"

Maisha yakaenda, Juma ndo akawa mfariji wangu, akawa ananijali kama mdogo wake yaani. Kijiji kizima mwanaume aliyekuwa tayari kuongea na mimi ni Juma pekee yake. Rafiki zangu walikuwa wananichukia bila sababu.

Wiki ikapita, wiki ya pili ikapita, nikakata matumaini ya Baraka nikajua naye kaishaambiwa. Niliumia maana nilianza kumpenda ila Juma akaniambia niwe na subira labda kazi zimemtinga.

Siku moja asubuhi nimeamka na kanga yangu nikakojoe nirudi kulala, ile natoka tu nakuta gari nyeupe ipo mlangoni 😳😳

"Amina!"

"Abee! Aaaaah Baraka karibu!"

"Asante mamy nimeogopa kuwaamsha ndo maana nikawasubiria muamke."

Ngoja nimwamshe mama! Nikaenda mbio hadi chumbani kwa mama. "Mama amka Baraka kaja na gari! 🤣🤣" Ushamba jamani.

"Wewe mtoto unanidanganya."

"Kweli mama njoo nje!"

Mama akavaa nguo akatoka nje akamkuta Baraka anatoa vitu kwenye gari.

"Karibu mwanangu."

"Asante. Amina ebu ingiza vitu hivi ndani nimewaletea na mama."

"Asante mwanangu."

Ile kuangalia barabara, kumbe mashoga zangu wameitana wanaangalia kinachoendelea pale nyumbani. Mimi nilivyowaona nilijishaua, mume wa mjini tena! 🤣🤣

"Za safari mwanangu?"

"Nzuri tu, za hapa mama?"

"Salama mwanangu. Amina kaa na mgeni nikachume mihogo."

"Mama kuna mikate mule kwenye mfuko ya chai na sukari humo."

"Asante mwanangu, ngoja nikuandalie chai."

"Sawa mama." Basi tukabaki mimi na Baraka.

"Amina nimekununulia zawadi ipo kwenye gari nitakupa baadaye."

"Sawa asante." 🤦🤦 Aibu sasa jamani. Kaka kapanda hewani, ana kifua kizuri, ana weusi fulani hivi jamani mmmh ni mzuri!

"Leo nataka tutembee kijijini kwenu."

Nikawaza, tukitembea naye wale wanaonizomea wakinizomea mbele yake si ataniacha? Hapana ngoja nikatae tu. 🙆🙆🙆🙆

***
Matangazo
Matangazo