Episode 5:
Basi tukala mihogo tukashiba, Juma akaondoka. Mafundi nao wakammaliza kazi wakaondoka, tukabaki mimi na mama.
"Amina, Baraka kisimani alikuwa anakwambia nini?"
"Aliniambia ananipenda, anataka anioe."
"Wewe ulimjibu nini?"
"Nilimwambia anipe muda nimjibu, na yeye alikubali."
"Sawa, ngoja tusubiri. Baadaye sijui anataka kuongea nini. Natamani mwanangu upate bwana utoke kijijini hapa."
"Bwana gani atanioa mimi mama? Watu watamwambia tu vitu nilivyofanyiwa."
"Tuachane na hayo mwanangu, tuandae mboga ya mchana. Hayo tumuachie Mungu."
"Sawa." Basi tukafanya maandalizi tukapika. Jioni saa kumi na mbili nipo chumbani napanga, mama alikuwa sebuleni.
"Odi odi!"
"Karibu, karibu ndani."
"Hapana mama, tukae nje. Siku nyingine nitaingia ndani mama."
"Sawa." Mama akampa kigoda. "Amina, niletee mkeka." Nikatoka nje na mkeka nikatandika tukakaa.
"Karibu mwanangu."
"Asante. Za saa hizi tena?"
"Nzuri mwanangu. Za toka muda ule?"
"Salama. Amina Kilamlya, vipi?"
"Safi."
"Mama samahani kama nitakuwa nimekukosea kwa kuongea haya. Mimi nampenda Amina, nataka nimuoe tuanzishe familia."
"Kwani Amina mwenyewe ulimwambia?"
"Ndio nilimwambia, alisema nimpe muda. Nimekubali kumpa muda, ila nahisi kuna jambo anataka kuniambia ila anasita kuniambia."
"Usijali, ikifika muda atakwambia. Labda anaogopa kwa kuwa bado hamjazoeana."
"Sawa mama. Ila mimi kesho kutwa nitaondoka nitarudi mjini, baada ya wiki nitakuja kufuata jibu."
"Sawa mwanangu, karibu."
Basi Baraka akampa mama laki moja. "Mama hii itakusaidia kipindi sipo, na hii solar nimeishailipia, hudaiwi tena."
"Asante mwanangu, Mungu akubariki sana!"
"Na wewe Amina, hamsini hii ikusaidie hizi siku mimi sipo."
Mimi nikakataa kuchukua, mama akanilazimisha kupokea. Nikapokea nikampa mama.
"Haya mimi naenda mama."
"Sawa mwanangu, jisikie uko nyumbani, njoo muda wowote." Mama alicheka kwa hela tena. 😂😂😂
Baraka akaondoka. "Mama mbona unapokea hela za watu wakati bado sijamkubalia?"
"Mwanangu huyu anakupenda kweli, we huoni? Afadhali uondoke kijijini hapa, we huchoki kuonyeshwa vidole?"
Njiani Baraka akakutana na vijana wa kijijini kwetu...

Matangazo
Matangazo