📖 Story Tamu

Episode 4:

"Kwani umepatwa na nini?"

"Hamna kitu nitakwambia, ila kwa sasa sipo tayari kukwambia kwa sasa."

"Sawa, ila jua nakupenda sana nataka nikuoe nikubalie tafadhali."

"Nitakwambia, nipe muda nitakujibu."

"Sawa, nisubirie kwa muda gani?"

"Nipe wiki moja itatosha."

"😳😳 Mbona mbali hivyo? Mimi nitakuwa nimeisharudi mjini."

"Sawa, ila nahitaji muda wa kufikiri ili..."

"Sawa basi nikienda mjini nitarudi huku kwa ajili yako."

"Sawa karibu tena, twende tukachote maji mama atakuwa na hofu."

"Sawa twende."

"Amina! Amina!"

"Abee!" Alikuwa Juma anakuja tulipo. "Vipi kaka Juma, kuna tatizo huko mbona mbio hivyo?"

"Hamna, nilimuuliza mama akasema umekuja kisimani, niliogopa nikajua uko pekee yako."

"Hamna, niko na Baraka."

"Sawa, vipi uko salama?"

"Niko poa. Huyu anaitwa Baraka, wamekuja kufunga solar. Baraka, huyu Juma ni kaka yangu wa hiyari namshukuru sana ananisaidia sana sina cha kumlipa zaidi ya Mungu mwenyewe. Nampenda kaka yangu ananichukulia kama dada yake wa tumbo moja yaani."

"Ni vizuri, nashukuru kukufahamu Juma, uendelee na moyo huo huo."

"Asante, karibu kijijini kwetu Baraka."

"Asante nimekaribia."

"Ngoja niwaache, nilijua yuko pekee yake."

"Tuongezane kwa pamoja tu haina shida Juma."

"Sawa, nikajua nitawabana bhana si unajua tena nataka shemeji mimi, dada yangu Amina amekua! 😂😂😂" Utani kidogo huku tunaenda kuchota maji. Tukarudi nyumbani mimi sikubeba ndoo, ndoo moja kabeba Juma nyingine kabeba Baraka.

"Karibuni wanangu, leo nina bahati Mungu kaniongezea watoto wa kiume." Wakatua maji, Juma akawa anaondoka mama akamzuia. "Kunja kwanza chai mwanangu."

"Mama asante nimeshiba nitakula siku nyingine."

"Haiwezekani kabisa, kaa hapo." Mama akatandika mkeka, kumbe alichimba mihogo akaweka. Akawaita mafundi wote waje kuchukua mihogo. Tulikuwa pale tukashiba, mafundi wakaendelea na kazi.

"Mama naomba kuongea na wewe baadae."

"Sawa mwanangu, ila kuna nini? Au Amina kakutukana huko kisimani?"

"Hapana mama."

"Sema Baraka, kama kakosea nimseme Amina."

"Hapana mama."

"Sawa karibu muda wowote jisikie uko nyumbani."

Baraka akanisogelea. "Umeona mama yako ananipenda? Mimi lazima nikuoe tu hata kama hutaki kuniambia mambo yako. 🙆"
Matangazo
Matangazo