📖 Story Tamu

Episode 3:

Nilisimama nikawa naogopa kuingia ndani, kumbe mama alikuwa amekwenda kuchota maji. Alivyorudi akanikuta nimeganda tu na kanga, akajua tu naona aibu. Akatua maji nje akanipa kanga aliyokuwa amezinga kichwani nikaivaa. Akawasalimia wote, hawakuitika; walikuwa bize kuniangalia. Mama akaniambia, "Ingia ndani." Mimi nikaenda ndani, akasalimia tena wakaitika kwa kushtuka.

"Pooh mama samahani, nilikuwa mbali kimawazo. Mmeamkaje?"

"Salama tu, sijui ninyi."

"Hatujambo, tumekuja kufungia solar."

"Sawa wanangu karibuni sana. Amina njoo!"

Mimi nikatoka, nilikuwa nimeishavaa gauni langu la kishamba limekomaa, ila umbo langu lilikuwa limejichora.

"Mimi naenda kubeba maji, baki na wageni."

"Sawa mama."

Nilibaki na wageni. Kuna huyo mgeni mmoja ambaye alimwambia mama atasogeza jina lake mbele ili awahi kuwekewa solar, jamani alikuwa ananiangalia hatari. Akasogea, nilikuwa jikoni nakoka moto.

"Amina umeamkaje?"

"Salama tu," nikajibu huku naona aibu.

"Una miaka mingapi?"

"20."

"Baba yuko wapi?"

"Amefariki."

"Kwa hiyo unaishi na mama peke yake?"

"Ndio."

"Sawa! Mimi ninashida ya kuongea na wewe sasa sijui wapi tutaonana?"

"Ongea na mama, akikubali sawa tutaenda kuongea."

"Sasa unadhani siwezi kumuomba mama yako? Ngoja arudi nimuombe mimi mwenyewe."

Basi mama akarudi akatua maji, wale wakaendelea na kazi ila yeye hata hafanyi lolote anaangalia tu.

"Mama Amina pole na kuchota maji."

"Asante mwanangu, yaani visima viko mbali sana yaani shida tu."

"Ngoja tukakuchotee na Amina, tupe ndoo mbili."

"😳😳 Hapana yametosha mwanangu wala usijali."

"Mama mimi naomba kuongea na Amina, nakuahidi nitamrudisha salama kabisa."

"Sawa, ila naomba muwe makini. Sijui jina unaitwa nani?"

"Ooh naitwa Baraka mama."

"Sawa, muwahi kurudi. Amina, ebu beba ndoo mbili kaka yako Baraka akupeleke kisimani."

"😳😳" Nilisita kidogo baadae nikakubali, nikabeba ndoo ndogo mbili tukaanza safari ya kisimani. Tukaenda umbali kidogo!

"Amina ebu tukae hapa kivulini nataka kuongea na wewe."

Basi tukakaa pale.

"Amina mimi nakupenda, nataka nikuoe na ndoa kabisa."

"😳 Hapana mimi nimeishaaribiwa maisha siwezi kuolewa. Historia yangu nikikusimulia huwezi hata kukaa karibu na mimi. 🙆"
Matangazo
Matangazo