πŸ“– Story Tamu

Episode 2:

Basi Juma akaondoka tukabaki mimi na mama nikawa natwanga kisamvu mama anakoleza moto.

"Mama Amina we mama Amina!!"

"Mama unaitwa na jirani yako hausikii!!"

"Abee mama Sofia karibu ndugu yangu samahani sikukusikia."

"Nilikuwa nakupa taarifa kuna mkopo wa solar umekuja kijijini kwetu wamefikia kwa mwenyekiti twende tukaone."

"Sawa ngoja nibadilishe kitenge kimechafuka sana."

Mimi nilivyosikia nikatwanga haraka nikainjika jikoni mama alivyotoka akakuta nimeisha bandika nikamwambia mama na mimi naenda kuona twendeni wote. Mama alitaka kunikatalia ila mama Sofia alinitetea tukaenda wote.

Tulifika kwa mwenyekiti mama na mama Sofi wakaongea na mwenyekiti na wale wanaokopesha wakasaini. Basi wakasema watakuja kufunga.

Basi tukawa tunaondoka, wakati tunaondoka wale wageni mmoja wapo akaanza kumwita mama maana alisikia wakati mwenyekiti anamwita mama.

"Mama Amina samahani," akawa anakuja tulipo yule mgeni. "Samahani mama nimesikia unaitwa mama Amina, huyu ndo Amina?"

"Ndio baba huyu ndo mwanangu wa kwanza na wa mwisho anaitwa Amina."

"Mmh hongera mama mtoto kweli ulizaa. Sawa mama nimeona utachelewa kufungiwa maana foleni ni nyingi ngoja niweke jina lako mbele kesho waje kukufungia."

"Sawa mwanangu nitashukuru."

"Haina shida mama haya mimi narudi."

"Sawa mwanangu."

"Mama Amina mbona huyu kaka anamwangalia sana Amina?"

"Mimi sijui we twende nyumbani. Amina kuwa makini mwanangu."

"Eeeh mama Amina umeanza, muache mtoto kama atapendwa muache aolewe."

"Atayemwoa mwanangu nani na aibu ile? Hakuna jasiri atakayeweza kumuoa mwanangu."

"Mimi..."

Basi mimi nilikuwa kimya tu mpaka tukafika nyumbani tukapika tukala usiku ukaingia tukalala. Asubuhi nilichelewa kuamka nikaamka saa tatu nikatoka nje na kanga tu nikaenda chooni. Kabla sijatoka nikasikia sauti ya gari nikatoka ili niangalie gari kijijini kwetu linaenda wapi.

Nilikutana na watu wa solar ndo wamekuja kutengeneza wakazima gari wakanisalimia nikaitika kwa aibu nikaogopa kutembea kuingia ndani nilikuwa sijavaa kitu ndani na wao walikuwa wananikodolea macho😳😳 nilisimama tu kumbe mama...

***
Matangazo
Matangazo