📖 Story Tamu

Episode 29:

Siku moja Juma alienda mjini kujumua vitu kama kawaida yake. Katika pitapita yake, alikutana na chizi (kichaa) mmoja hivi barabarani. Alihisi kama anamjua yule mtu, akaachana naye akaenda zake kujumua vitu. Mara akamuona tena yule chizi, na safari hii akasikia vijana fulani wakimzungumzia.

"Yaani maisha haya bwana! Huyu jamaa alikuwa na hela sana, sijui kakosea masharti gani mpaka amekuwa chizi hivi."

Juma akawauliza, "Kwani unamjua huyu?"

"Ndio, si Baraka huyu! Yaani jamaa nyumba yake ilidondoka ghafla tu, akawa hivi."

Juma alivyosikia jina la Baraka, akamsogelea yule chizi kwa karibu. Akagundua ni yeye kweli, ila kachafuka sana na ana hali mbaya. Juma akanipigia simu kunisimulia, akaniambia anamchukua anakuja naye kijijini. Kweli watu walimsaidia kumkamata, wakamuweka kwenye gari. Usiku wakafika kijijini, akamleta mpaka nyumbani.

Mimi nilikuwa namchukia sana Baraka kutokana na yale aliyonifanyia, ila mume wangu Juma aliniambia, "Amina, usilipe ubaya kwa ubaya."

Juma akamfuata mchungaji, wakaja nyumbani kuanza maombi. Mchungaji aliomba hadi jasho likamtoka, masaa yakakatika tu! Mpaka saa tisa usiku tupo macho na maombi. Ghafla Baraka akaanguka chini, bado tukawa tunaomba. Mwishowe akafungua macho, akawa kama amezinduka. Juma akamwita kwa sauti.

"Baraka!"

"Naam..." akajibu kwa sauti ya unyonge.

"Mimi ni nani?"

"Wewe ni Juma."

"Na huyu je?"

"Huyu ni Amina."

"Nini kilikupata?" Juma akauliza. Hapo ndipo Baraka akaanza kusimulia stori yake ya kusikitisha.

"Naitwa Baraka. Familia yangu yote ilikufa kwa ajali, nikawa sina ndugu tena wa damu. Nikaenda mjini kuanza maisha na maisha yalikuwa magumu sana. Nilimpata mkaka mmoja hivi, nilimuomba msaada. Akaniambia hawezi kunipa msaada wa hela, ila anaweza kunionyesha sehemu ya kupata hela haraka."

"Kweli alinipeleka kwa mganga. Mganga akaniambia: *'Nakupa hiki kijiti, huyu ndiye atakuwa mkeo. Kila atakachokwambia utafanya.'* Kwa kuwa nilikuwa na shida ya hela, nikabeba kile kijiti nikarudi nacho nyumbani."

"Nilivyofika nyumbani nikajifungia geto, nikawasha udi. Nikakiambia kile kijiti nataka hela ya mtaji na ya kujengea nyumba. Nilivyofumbua macho, nilikutana na hela nyingi sana! Nilifurahi, nikaenda kumshukuru yule kaka, nikanunua nyumba na kufungua biashara kubwa."

"Nikarudi kwa mganga maana alinipa muda nikaende tena. Nikaenda, nikapewa sharti kubwa ambalo kama nikilikataa, basi nitakufa. Kile kijiti kilikuwa ni mwanamke (jini) ambaye nitakuwa nakaa naye maisha yangu yote. Sasa nikawa najiuliza, nitaishije na kijiti?" 🙆🙆
Matangazo
Matangazo