📖 Story Tamu

Episode 28:

"Juma! Juma!"

"Niambie mke wangu?"

"Mama ana matatizo, kanipigia simu." Juma anavyompenda mama alikurupuka tukaenda kwa mama. Duuh! Tukamkuta Baraka jamani, wapo wanafungua sola. Nilipatwa na hasira naye. Kuniangalia, akanikuta nina mimba kubwa, alishangaa.

"Aaah Amina, una mimba?"

"Ndio, kwani uliambiwa mimi mgumba?"

"Nani kakuoa huyo?"

"Nimemuoa mimi! Kwani unamdai shilingi ngapi mama?" Juma aliuliza.

"Namdai laki mbili. Kwani mna hela za kunilipa maskini ninyi? Mnajaribu hadi kuniuliza?"

Juma hakumjibu. Aliingiza mkono mfukoni akatoa hela, akahesabu laki mbili akampa Baraka. Baraka alitoa macho! 😳

"Wewe hela hizi umepata wapi?"

"Kwani uliambiwa kiwanda cha hela unacho peke yako?"

"Juma unadharau eeeh? Sasa nitaona kama Amina atazaa!"

"Umesemaje Baraka? Uliyomfanyia mwanangu hayakukuridhisha? Toka kwangu haraka!" Mama alifoka.

"Natoka, ila mwanao hatojifungua!" Baraka akaingia kwenye gari akaondoka. Tukabaki tumesimama.

"Usijali mke wangu, maneno ya mkosaji tu." Juma alinituliza.

"Lakini Juma, Baraka ni mchawi kweli?"

"Usijari, hawezi shinda." Tukarudi nyumbani. Mimi nikabaki, Juma akaenda dukani.

Maisha yakaenda. Miezi ikapita mpaka miezi kumi na moja, sijisikii uchungu wowote! Mume wangu alihangaika sana, alikuwa anasali muda wote. Mimi tumbo zito kama nimebeba mawe.

"Mke wangu, nataka nimuombe mchungaji aje kukuombea."

"Sawa Juma, muite tu maana hata sijui kama kuna mtoto humu."

Kweli, jioni alirudi na mchungaji na waumini watano. Nikawakaribisha tukaanza nyimbo za kuabudu. Tuliomba masaa sita jamani! Hapo hapo uchungu ukapanda, mtoto alitoka mbele ya mchungaji!

Mtoto nilimzaa mnene, mchungaji alishukuru Mungu akashauri wanipeleke hospitali maana nimezalia nyumbani. Mtoto wangu wa kiume, kafanana na Juma hatari!

"Pole mke wangu, nashukuru kwa kuniletea pacha wangu." Basi nikapelekwa hospitali.

Mama asubuhi ndio alipewa taarifa ya mimi kujifungua. Daaah! Mama yangu furaha ilimzidi, alisahau hadi ndala, alikuja hospitali peku! 👣

"Amina hongera mwanangu, mtoto gani?"

"Nimeleta Juma, mama."

"Eeeh hongereni wanangu!" Basi wakamhudumia mtoto, wakaniangalia na mimi. Mchana tukarudi nyumbani. Maisha yakaendelea, biashara ikaendelea vizuri sana. 👌👌👌
Matangazo
Matangazo