Episode 27:
Tulisalimiana na Juma, tukapiga stori na mama akapika tukala. Juma alikuwa anaondoka, nikamsindikiza hadi kwake. Tukakaa nje, tukapanga maisha yetu. Sikumwambia kama nimekuja na hela. Akaniambia atanioa, basi nikarudi nyumbani. Kama wiki mbili zikapita, nikaanza kumsahau Baraka.
Siku moja nilikaa na mama jikoni, nikamwambia mama, "Baraka (Juma) anataka kuja kutoa mali." Mama hakupinga maana alikuwa ampenda sana Juma, ila kwa yale yaliyotokea ndo maana akataka niolewe na Baraka awali ili nitoke kijijini pale.
Siku ya mali ikafika, akaja kutoa mali. Nikapelekwa kwake, maisha ya ndoa ya amani yakaanza. Alikuwa na mazao yake ambayo alilima wakati nipo mjini, akauza tukanunua uwanja kwa majina yetu. Nilivyomuona kaniandika na mimi kwenye uwanja, nikamuonyesha hela, nikamwambia, "Tujenge basi, zipo!"
Akanishauri tufungue ofisi, faida tutakuwa tunajengea. Kweli tulifungua ofisi ya vyakula, tukaanza biashara. Vitu tunaagiza mjini, biashara yetu iliimarika sana! Tukawa tunaongoza kijijini kwa biashara. Mama alikuwa anampenda Juma kama mwanae, na Juma naye alikuwa anamjali mama kama mama yake mzazi. Maisha yakaenda.
Siku moja nilijisikia kizungu-zungu nikaanguka. Wakatafuta gari wakanipeleka hospitali, nikapata vipimo.
"Mume wa Amina yuko wapi?"
"Mimi hapa nesi."
"Njoo ofisini." Wakaingia ofisini.
"Mkeo tumemkuta ana malaria, tutamuandikia dawa. Halafu kingine, mkeo ni mjamzito."
"π³π³ Nini?! Mke wangu mjamzito? Asante Mungu!"
"Sasa kuwa naye makini, na muanze kliniki mapema."
"Sawa nimekuelewa." Alitoka nje ana furaha.
"Nini mwanangu?" Mama akauliza.
"Mama, mke wangu mjamzito! Mwanao ana mimba, si muda unapata mjukuu!" π€Έπ€Έπ€Έπ€Έ
"Kweli!!!!? Ina maana si muda nitakuwa bibi?" ππππ
Walifurahi sana. Hata mimi nilivyopata habari nilifurahi sana, maana kwa yale matatizo nilihisi sitopata kuzaa. Basi tukarudi nyumbani.
Mume wangu alinidekeza sana, alinilea kwa madeko sana! Hii mimba, upendo uliongezeka. Miezi ikasonga ikafika miezi saba. Siku moja asubuhi nikakuta simu yangu inaita, kuangalia ni simu ya mama. Nikapokea.
"Shikamoo mama!"
"Marhaba mwanangu. Njoo nyumbani kuna matatizo, uje na hela kidogo." ππ

Matangazo
Matangazo