Episode 26:
"Ngoja nimpe zawadi." Alinipa laki moja jamani! Nilipokea, sikuizila hata kidogo.
Niliingia chumbani nikachana kanga, nikafunga hela zangu vizuri. Kile kinguo nikajifunga kiunoni, nikajifunga vizuri kama alivyonifundisha bibi. Nikatoka, nikachukua begi langu. Nikaenda kwa jirani nikaomba ampigie bodaboda, akampigia. Bodaboda akaja akanibeba mpaka stendi.
Nikapata basi, nikakwea. Safari ya nyumbani ikaanza! Jamani sikuamini, nilifurahi sana. Nikikumbuka matatizo niliyopitia, siamini kama narudi nyumbani. Yaani daah!
Nikafika saa kumi jioni stendi ya kwetu. Sikuamini, nilishuka kwenye basi kila mtu alikuwa ananiangalia. Nilivaa gauni langu zuri, nikaifuata bodaboda nikamwambia anipeleke nyumbani. Tukakwea tukaondoka. Mama na Juma sikuwaambia kama narudi leo.
Nilifika nyumbani, nilimkuta mama anapika. Alivyoniona alinirukia! Nilivyomuona mama, nilimkumbatia nikaanza kulia. Nililia mpaka mama anashangaa tu.
"Dada naomba hela yangu niende." Bodaboda akasema.
"Shilingi ngapi mwanangu?"
"Buku tu mama."
Mama akaenda ndani kumchukulia hela, boda akaondoka. Tukabaki na mama.
"Mwanangu yamekukuta nini mbona unalia?"
"Mama, Baraka sio mtu kabisa! Sio yule uliyekuwa naye kijijini mama. Baraka kanifanyia kitu kibaya! 😭😭😭"
"Kakufanya nini?"
"Baraka ana mke mama, na Baraka alinifanya nyuma! 😭😭"
"Nini?! Baraka huyu huyu au ulikosea mwanangu wewe mkorofi?"
"Hapana mama!" Nikaanza kumsimulia mama kila kitu. Alilia jamani! Alilia mpaka alimkumbuka mume wake (baba).
"Mama nyamaza, nimerudi salama usilie sana."
Tukanyamaza pale tukaanza kusalimiana. Basi mama akaingia jikoni kuendelea kupika, mimi nikachukua simu nikaanza kumpigia Juma.
"Hallo!"
"Eeh niambie Amina, kwema?"
"Nina matatizo, naomba umpelekee simu mama sasa maana simu yake haipatikani."
Juma kwa haraka yake, bila hata kupiga simu kwa mama, akakurupuka mpaka nyumbani!
"Mama hodi!"
"Karibu mwanangu."
"Asante. Shikamoo. Amina kanipigia simu kasema ana matatizo, nikuletee simu..." Anamaliza kuongea, mimi nikatokea!
Jamani Juma alitoa macho 😳😳!
"Amina kwa nini umenifanyia hivi lakini? Hivi unajua nimekimbia kiasi gani?" Juma alikasirika, nikambembeleza akanisamehe.
***
Hapo ndipo safari ya Amina mjini inaishia, na sasa anaanza maisha mapya kijijini akiwa na siri nzito na fedha alizookoa.

Matangazo
Matangazo