Episode 25:
"Mbegu anachukua zinaenda kwa mke wake! Nahisi wale wana mali za kishirikina."
Mmmh! Nilichoka. Nikamuaga yule jirani, nikarudi ndani. Jioni ikafika, nikapika nikala, nikawa nasubiria muda wa kulala ili kesho asubuhi nianze safari ya kurudi kwetu.
Mara nasikia, "Ngo ngo!"
"Nani wewe?"
"Fungua mlango! Unafunga mlango, nyumba ni yako?"
Nikajua ni Baraka. Nikaenda kumfungulia, kumbe kaja na binti wa miaka kama 18 hivi, yupo na begi.
"Hivi wewe huoni wageni? Huwezi kumpokea? Kwani si nilikwambia uondoke, unasubiri nini?"
"Nimekosa gari mpaka asubuhi."
"Haya! Peleka mabegi chumbani. Hii nyumba ni ya Oliva kuanzia sasa, wewe imekushinda, ondoka!"
"Sawa, nitaondoka asubuhi."
Yule binti alikuwa mstaarabu, akanisalimia vizuri. "Shikamoo dada!"
"Marhaba, karibu mdogo wangu."
"Asante." Mara SMS ikaingia kwa Baraka, alivyoisoma tu akasema, "Wewe Amina mimi naondoka, ole wako umsumbue huyu binti! Nitakutafuta popote uendako."
"Uwe na amani tu, simsumbui."
Baraka akaondoka, tukabaki na huyu binti. "Hivi unaitwa nani mdogo wangu?"
"Naitwa Oliva."
"Umekutana naye wapi Baraka?"
"Kijijini kwetu, alikuja na wale waweka sola."
"Kakwambiaje? Uko peke yako au kakwambia ana mke?"
"Kaniambia mke wake Amina ila kamuudhi, wameachana karudi kwao. Nashangaa nimekukuta! Mimi sitaki mitala, bora anirudishe kwetu."
"Pole. Mimi mwenyewe nilidanganywa kama wewe. Huyu ana mke wake, tena anamuogopa mke wake balaa! Nakuonea huruma, natamani nikwambie mengi ila siwezi. Sijui kakudanganya nini ila jua sio mwanaume, ana mambo ya ajabu sana. Mimi sijamaliza hata mwezi naondoka, kwa hiyo kama unajipenda ondoka, ila kama hujipendi baki."
"Dada Amina, mimi naondoka saa hizi hapa!"
"Hapana, subiri niondoke mimi. Ukiondoka ukiniacha mimi hapa ataniua, atajua nimekwambia mambo yake. Tukalale, asubuhi usimwambie chochote. Jioni toroka nenda kwenu, najua akija asubuhi lazima akuachie hela nzuri tu ndo uitumie usafiri."
"Sawa asante dada." Tukaenda kulala, asubuhi tukaamka.
Nikajiandaa nikawa nataka kuondoka mara akaja Baraka. "Oliva mke wangu!"
"Abee!" Akatoka Oliva, wakakumbatiana.
"Vipi Amina hajakusumbua usiku?"
"Hapana hajanisumbua, ni mtu mzuri."
"Vizuri, ngoja nimpe zawadi..." akanipa... 🙆🙆🙆🙆

Matangazo
Matangazo