Episode 21:
"Nikanunue chupi nzuri!!! Mmmmh 😳😳 makubwa! Chupi sinunui kwanza."
Ngoja nitoke nipate hata wenyeji wawili watatu. Nikaoga nikanywa chai nikatoka nje kuangalia wa kujipendekeza naye. Nikaangalia pembeni nikamkuta jirani anafua, mdada hivi, nikaenda.
"Habari dada!"
"Salama, kwema?"
"Kwema, habari za hapa?"
"Nzuri karibu."
"Mimi nakaa nyumba ile pale, nimeona nije kuwatembelea majirani niwajue."
"Ooh karibu sana! Kwani mdada aliyekuwa anaishi humo kaishaondoka au wewe ni ndugu?"
"Mdada gani?"
"Mke wa Baraka, binti mdogo dogo tu alikuwa anaishi hapo. Kama mwezi hivi sijamuona sasa."
"Mmh 🙆🙆🙆🙆 dada mimi mwenyewe sielewi kitu. Nimeletwa hapa na mume wangu Baraka, sasa sijajua wewe unamzungumzia Baraka gani."
"Baraka mwenye nyumba hii. Yule binti alikuwa rafiki yangu ila sijamuona mwezi sasa. Ila mara ya mwisho kumuona alikuja hapa aliniambia anaweza kuondoka maana huyo Baraka alivyoona hashiki mimba akaanza kumchukia yule binti."
😳😳😳😳 Niliishiwa nguvu! Nikajikaza nikamuomba kama atakuwa na muda anipeleke mjini nikanunue vitu.
"Sawa, ngoja nimalize kufua niwaambie na wanangu, nikimaliza nitakuja kukwambia twende."
"Sawa."
Nikarudi kwangu nikapika na mimi nikala, nikaoga nikakaa naangalia TV huku nawaza yale maneno aliyoniambia yule mdada. Ina maana anakuleta, usipozaa anakufukuza? Duuh!
"Odi odi!"
"Karibu!" Yule dada akaingia ndani akakaa. "Nimemaliza kazi tunaweza kwenda."
"Ndio nimeishajiandaa." Tukaenda tukafika mjini. Nikamwambia, "Nataka kutuma bati kwa mama, stendi ya magari ya mkoani iko wapi?"
"Twende, ipo upande huu." Tukaenda nikamuelekeza mpokeaji mizigo nikamwambia mzigo unakoenda, akaniambia nikalete hizo bati.
Tukaenda na yule dada kununua bati, tukapelekewa stendi tukabuku. Nikamwambia nipeleke na sehemu ya kununua nguo, tukaenda nikanunua nguo chache za kuzugia na chupi tatu. Nikamnunulia na yule dada gauni maana katumia muda mwingi sana. Tukanza safari ya kurudi, tukaanza kuongea njiani.
"Yaani bora uwe unanunua vitu unapeleka kwenu, maana Baraka hatabiriki. Anampenda sana mke wake! 🙆🙆🤦🙆😳🙆"

Matangazo
Matangazo