📖 Story Tamu

Episode 18:

"Nikaanza mipango ya kukuoa. Ila nina mke, tuna makampuni, tuna mashule. Mke wangu ndio anasimamia, hata wewe ukiwa karibu naye atakupa hata biashara moja, ni mtu mwema sana."

😳😳😳😢😢 Nilichoka sana. Inabidi nimuulize, "Kwa hiyo zamu ni siku ngapi?"

"Kwako nitakuwa nalala siku mbili, kwa mke wangu siku tano. Tulikubaliana hivyo."

"Haiwezekani! Zamu weka sawa sawa. Kama ni hivyo, nirudishe kwetu!"

"Haina shida kama unataka kurudi, ila jua nakupenda sana sana."

"Sasa kama unanipenda, kwa nini hutaki kuweka zamu sawa sawa?"

"Mimi na mke wangu tulikubaliana hivyo kabla ya mimi kuoa. Naomba nielewe."

Nikawaza, mimi ni mjinga sana. Nikisema nirudi nyumbani nitaenda kufanya nini? Bora nijipange tu huku huku. Nikakubali japo kishingo upande.

"Sawa nimekubali. Kwa hiyo leo unalala hapa hapa?"

"Hapana, mpaka siku tano ziishe maana nimekaa kwenu siku nyingi sana. Ila nataka tuinjoy leo."

Nilijikuta namchukia yule Baraka, nilikwazika sana ila nikawa sina jinsi. Basi tukaingia chumbani tukashiriki tendo, hata raha sikuona. Anaparamia tu, kweli huyu anataka mtoto tu. Alivyomaliza akaniachia kama laki mbili, "Hela za matumizi hizi."

Nilipokea, akaondoka. Niliwaza yale maisha sikuyapenda. Ndoa ina masharti; kama yupo kwa mke wake usipige simu! Mmh aya maisha gani jamani?

Mara SMS ikaingia kwenye simu yangu kutoka kwa Baraka: *(mke wangu anataka kukuona)*.

Mimi nikajibu: *Sawa, lini?*

*Leo jioni nitakuja kukuchukua.*

Sawa. Nikatulia pale, mbili haikai wala moja haikai. Nawaza nifanye nini maana hii ndoa hapana. Shemeji alikuja siku moja tu akaondoka.

Muda wa jioni ukafika, Baraka akaja na gari akanichukua tukaenda nyumba wanayokaa. 🤦🤦🤦🥰🥰 Nzuri! Bonge la mjengo. Tumepita getini tukashuka, nyumba nzuri jamani uwiiiiiiii! Tunaingia sebuleni utasema huu ukumbi umepambwa, kuna ndoa 🥰🥰 daaah maisha haya wengine tunasindikiza tu 🤣🤣.

Tukakaribishwa na wadada walikuwepo wanne, wote wafanyakazi. "Amina kaa."

Nilikaa mpaka uoga, nilitulia tuli 🥰🥰🤣. Jamani halafu harufu ikaja nzuri, nikahisi kuna majini mle ndani. Alitokea mdada, maji ya kunde, kapanda hewani, mzuri jamani uwii 🤣🤣🤣🤣.
Matangazo
Matangazo