Episode 17:
Mama akawaona mashoga zangu, alitafuta fimbo akaipata. Akasogea kimya kimya akawatawanya, walipoteana walitoka mbio! 💃💃💃
"Ole wenu mje tena hapa nyumbani!" Mimi na Juma tukaanza kucheka.
"Wewe Amina, mimi natoka naenda sokoni kule kuna jambo naenda kulifanya. Usitoke hapa, Juma mwambie mdogo wako asitoke."
"Sawa mama, huyu hatoki utatukuta hapa hapa."
"Sawa."
Mama akaenda, nikabaki mimi na Juma.
"Amina mdogo wangu, unaenda kuolewa usimsahau mama. Mimi kaka yako sina hela na unaniona, usijisahau ukifika mjini."
"Lakini mimi nataka kwenda na ninyi mjini."
"Hapana, nenda wewe sisi tuache. Epuka tu tamaa, usiwe msaliti kwenye ndoa."
"Sawa kaka."
Siku zikawa zinaenda, siku ya ndoa ikafika. Wakaja watu wachache tukafunga ndoa ya kijijini, akaniambia sherehe kubwa itafanyika mjini. Hapo moyo upo kwa Juma, na Juma ananichukulia kama mdogo wake. Nilimuaga mama huku nalia. Baraka alimpa mama hela za matumizi na simu ndogo. Ila Juma ndio alimpa simu kubwa, wakawa marafiki sana.
Tulidamka asubuhi safari ya mjini ikaanza, saa tisa mchana tukafika mjini. Akanipeleka mpaka kwenye hiyo nyumba tutakayoishi. Nyumba ilikuwa ya kawaida ila kubwa, nikamkuta mkaka akasema ni mdogo wake kabisa.
Nikaonyeshwa mazingira ila sikuona nguo za Baraka hata moja.
"Kwani wewe humu hujawahi kukaa?"
"Ndio, sijawahi kukaa hapa, ninakwangu. Kwa nini umeuliza?"
"Sijaona nguo zako."
"Usijali zinakuja. Mimi natoka, nitakuja kesho. Shemeji yako kakupekea, kula upumzike."
"😳😳😳 Mmh! Mbona unaniacha peke yangu?"
"Tutaongea vizuri kesho." Baraka akatoka. Shemeji akanibembeleza kula nikagoma, nikaenda chumbani.
Kesho yake akaja na nguo kidogo, ilikuwa asubuhi.
"Za asubuhi mke wangu?"
"Nzuri, za huko utokako?"
"Wazima wote."
"Umelala wapi?"
"Twende tukaongelee chumbani, sio hapa."
Tukaingia chumbani. "Haya niambie, umelala wapi mwenzangu?"
"Amina, najua nitakuumiza kwa nitakachokiongea. Mimi nina mke, wewe ni mke wa pili. Mke wangu anatatizo la kutokuzaa, akaniruhusu nioe mke wa pili. Mwanzo nilikataa kabisa ushauri wake, ila siku niliyokuona moyo wangu ulikupenda, nikamwambia mke wangu akakubali. Ndio nikaanza mipango..."
"😭😭 Yaani..."

Matangazo
Matangazo