📖 Story Tamu

Episode 16:

"Mimi nitakuvalisha siku nikikuoa."

Basi alitoka nje, mimi moyoni niliumia sana. Baraka alipoona kijijini mambo yamekaa sawa akaondoka, akaniambia, "Nakuja kukuoa kabisa."

Mama alipewa ahadi ya mimi kuolewa, na mama akafurahi sana akawa ananilinda nisiwe natoka-toka, maana mimi sasa ni mchumba wa mtu.

Sasa nashangaa, moyoni naanza kumpenda kaka Juma. Yaani nikikaa bila kumuona sisikii raha, natamani nimuone tu.

Marafiki zangu walionitenga walisikia nataka kuolewa, si wakaona waje kunizoea tena ili wajue kama nimetumia dawa au nini. Yaani wanataka kunichimba-chimba mimi.

Basi tulikaa na kaka Juma, wao wakaja. Sasa mama hawapendi kweli, na kaka Juma naye hawapendi lakini hawezi kuwafukuza.

Ila mama...
Matangazo
Matangazo