Episode 13:
Mwangaza wa tochi ya Richard uliendelea kumulika miili ya wasaliti hao wawili ambao walikuwa wameganda kama sanamu. Rahma alikuwa amejivuta pembeni mwa kitanda, akijifunika uso kwa mikono yake huku akilia kwa kwikwi za aibu. Ramadhani, akiwa hana pa kutokea, alijaribu kuokota shuka lakini Richard alilikanyaga kwa nguvu.
"Usijifunike, Kaka Rama! Onyesha ujasiri uliokuwa nao sekunde chache zilizopita ulipokuwa ukinitukana kwenye kitanda changu!" Richard alinguruma, sauti yake ikitetemeka kwa mchanganyiko wa hasira na maumivu makali.
Mjumbe wa kijiji, mzee mwenye heshima, alitikisa kichwa kwa masikitiko makubwa. "Ramadhani, mwanangu... hili ni laana. Kumvulia nguo mke wa mdogo wako wa damu? Tena kwenye kitanda chake? Hili halijawahi kutokea katika kijiji cha Mbuyuni tangu nimeanza uongozi."
Juma na wale vijana wawili walimvuta Ramadhani na kumpushia pembeni, wakimpa msuli wake uliokuwa umetupwa chini ya kitanda. "Vaa haraka, na usijaribu kukimbia. Leo utajibu mbele ya wazee," Juma alisema kwa ukali.
Rahma alipiga magoti kitandani, akiwa amejitanda shuka kwa fujo. "Mume wangu Richard... naomba unisamehe! Ni shemeji... shemeji ndiye aliyenishawishi! Aliniletea zawadi, akaniambia wewe hunijali... mume wangu nimepotea!"
Richard alimtazama Rahma kwa jicho la dharau ambalo lilimchoma Rahma kuliko kisu. "Zawadi? Kwa hiyo uzuri wako na uaminifu wako kwa ndoa yetu una thamani ya vazi la hariri la shilingi elfu kumi? Rahma, nilikupenda kwa dhati, nikakupa kila kitu nilichokuwa nacho. Leo umenionyesha kuwa hukustahili hata chembe ya upendo wangu."
Ramadhani, baada ya kuvaa msuli wake, alijaribu kuanza kujitetea kwa kiburi cha mjini. "Mdogo wangu, haya mambo hutokea. Mimi ni mwanaume, na huyu ni mwanamke mrembo. Imetokea tu, tuyafunike yaishe..."
*PAA!* Kofi zito kutoka kwa Richard lilimyamazisha Ramadhani. Ilikuwa ni mara ya kwanza Richard kumpiga kaka yake tangu walipokuwa watoto. "Usiniite mdogo wako! Tangu leo, huna mdogo, na mimi sina kaka. Umekiuka agano la damu."
Mjumbe aliamuru: "Vijana, wachukue hawa wawili. Wapelekeni kwenye ofisi ya kijiji. Richard, nenda kapumzike, asubuhi tutakaa kikao cha dharura chini ya Mbuyu. Hili jambo haliwezi kupita hivi hivi."
Usiku ule ulikuwa mrefu zaidi katika maisha ya Richard. Alibaki peke yake kwenye kile chumba kilichokuwa kimechafuliwa. Alichukua lile vazi jekundu la hariri, akaliwasha moto katikati ya uwanja, akitazama jinsi moto unavyoteketeza kila kumbukumbu ya usaliti ule.
Habari zilisambaa kama moto wa nyika. Kufika saa kumi na mbili asubuhi, nusu ya kijiji cha Mbuyuni ilikuwa imeshakusanyika chini ya mti wa Mbuyu kusubiri hukumu ya kihistoria.

Matangazo
Matangazo