Episode 10:
Baada ya tukio la kile kivazi jekundu la hariri, amani ilitoweka katika nyumba ya Richard. Ingawa Richard alionekana kuwa mpole na mwenye kukubali maelezo ya kinafiki ya kaka yake, ndani ya moyo wake kulikuwa na moto unaowaka. Alianza kuunganisha doti; vicheko vya siri, miguso ya bahati mbaya, na jinsi Rahma alivyokuwa akitetemeka kila Ramadhani alipokaribia.
Richard aliamua kuwa "paka mjanja." Siku iliyofuata, alijifanya anaamka na kujiandaa kwenda shambani kama kawaida.
"Mke wangu, leo nina kazi nzito kule bondeni. Naona mvua inakaribia, hivyo nitashinda huko mpaka jioni sana. Kaka Rama, naomba uangalie nyumba, mimi nitachelewa," Richard alisema huku akivaa buti zake za shambani.
Ramadhani alitikisa kichwa kwa dharau ya chinichini. "Usijali mdogo wangu, nipo hapa. Nitalinda kila kitu, hakuna kitakachoharibika."
Richard aliondoka na jembe lake begani. Lakini alipofika umbali wa mita mia tano, aligeuka na kupita njia ya uchochoroni. Alirudi nyuma ya nyumba yake na kujificha kwenye banda la kuku lililokuwa na upenyo mdogo unaotazama dirisha la sebule na jikoni.
Ndani ya nyumba, mazingira yalibadilika mara moja. Richard alipoondoka tu, Ramadhani alitoka chumbani kwake akiwa amevalia taulo tu kiunoni. Alimkuta Rahma akiwa sebuleni akifanya usafi, lakini akiwa na hofu tele.
"Rahma, mbona unajitesa na usafi? Richard ameshaondoka, na amesema atachelewa. Njoo hapa tupumzike kidogo," Ramadhani alisema huku akimvuta Rahma mkono.
"Shemeji, hapana! Jana Richard ametutilia shaka. Ile nguo nyekundu imemchanganya. Naomba tuache haya mambo, nampenda mume wangu," Rahma alijitetea, huku akijaribu kuchomoa mkono wake.
Ramadhani alicheka kicheko cha ushindi. Alimvuta Rahma kwa nguvu na kumkumbatia. "Unampenda Richard kwa maneno, lakini mwili wako unanipenda mimi. Jana ulivyokuwa unatoa sauti kule jikoni, hukusema unampenda Richard. Usijifanye mtakatifu sasa hivi."
Ramadhani alianza kumpapasa Rahma shingoni. Rahma alihisi ule msisimko wa jana ukirudi kwa kasi. Alijaribu kusukuma kifua cha Ramadhani, lakini mikono yake ilikosa nguvu. Alijikuta akiegama kwenye kifua cha shemeji yake, akivuta harufu ya kiume iliyomfanya asahau kiapo chake cha ndoa.
Kutokea kule kwenye banda la kuku, Richard alikuwa akiona vivuli vya watu wawili wakikumbatiana sebuleni. Ingawa hakuona sura zao vizuri kutokana na pazia jepesi, alijua fika kuwa mke wake na kaka yake wamevuka mipaka. Mikono ya Richard ilianza kutetemeka kwa hasira, na machozi ya uchungu yalianza kumtoka.
"Kaka yangu wa damu... mke wangu niliyemlipia mahari kwa jasho langu..." Richard alinong'ona kwa sauti iliyojaa maumivu.
Alitaka kukurupuka na kuingia ndani na panga lake, lakini akili ya upelelezi ilimwambia asubiri. Alitaka kuwapata "laivu" ndani ya chumba chake ili wasiwe na kisingizio chochote. Aliona vivuli vile vikielekea upande wa chumba cha kulala.
Richard alishuka kwenye banda la kuku na kusogea karibu na ukuta wa nyumba. Alisikia sauti ya mlango wa chumba chake ukifungwa, kisha kukafuata kicheko cha chini cha Ramadhani na sauti ya Rahma akisema, *"Shemeji, fanya haraka kabla Richard hajarudi..."*
Moyo wa Richard ulipasuka vipande vipande. Alijua kuwa amani ya kijiji cha Mbuyuni ilikuwa inaenda kuisha usiku huo.

Matangazo
Matangazo