✦ Matangazo ✦

πŸ“– Story Tamu

Episode 6: Kivuli cha Robby

Maneno ya Robby yalikuwa yakichoma kama pasi ya mkaa moyoni mwangu. "Mwanamke ni gharama, Tom." Kauli hiyo ilikuwa na ukweli mchungu ambao sikutaka kuukubali. Nikiwa nimeishika ile laki nne na nusu iliyobaki ya Caroline, nilihisi kama nimeshika mkaa wa motoβ€”itakua na faida kumwokoa Lisa, lakini itaniunguza mikono yangu baadaye.

Usiku huo, nilishindwa kulala. Niliwaza: Kama Lisa amepoteza simu, amewezaje kunitumia ujumbe wa kuniomba vocha? Na kama amefukuzwa kwa Mamkubwa, kwanini hakuniambia mapema kuwa Robby alikuwa anamtafuta?

Ghafla, mlango wa chumba changu uligongwa taratibu. Nilikata pumzi. "Dora?" niliuliza kwa sauti ya chini.

"Ni mimi, fungua," sauti ya Dora ilikuwa na haraka. Nilifungua mlango, akachomoka ndani na kufunga. Safari hii hakuwa amevaa kanga, alikuwa amevaa gauni la kulalia (night dress) ambalo lilikuwa na wepesi wa ajabu.

"Tom, nimeona ujumbe kwenye simu yangu. Robby amemtumia Lisa pesa jioni hii," Dora aliniambia huku akinitolea macho ya huruma.

"Unasema nini? Lisa yuko gesti, mimi ndiye niliyemlipia!" niling'aka.

"Tom, amka! Lisa amemtumia Robby namba ya chumba na jina la gesti uliyomuweka. Robby yuko njiani kuelekea huko sasa hivi. Huyo binti anakuchezea akili, anachukua pesa kwako na anampa penzi Robby," Dora aliongeza huku akishika mkono wangu uliokuwa unatetemeka.

Sikutaka kusubiri maelezo zaidi. Nilivaa koti langu, nikachukua simu na laki nne yangu, kisha nikachomoka nje kuelekea ile gesti. Moyo ulikuwa unalipuka. Nilifika pale saa sita za usiku. Mapokezi palikuwa na kijana mmoja mvivu aliyekuwa anasinzia.

"Chumba namba 10, yule binti aliyeingia mchana yuko?" niliuliza kwa ukali.

"Yuko na mgeni wake, kaka. Walisema wasisumbuliwe," kijana yule alijibu bila hata kuninyanyulia macho.

Dunia ilizunguka. Nilipanda ngazi kwa fujo na kufika mlangoni mwa chumba namba 10. Nilijaribu kusikiliza. Ndani kulikuwa na sauti za vicheko vya chini chini. Sauti ya mwanaume ilikuwa nzitoβ€”ilikuwa ni sauti ya Robby!

"Lisa, huyu kijana atakupeleka wapi? Hana mbele wala nyuma. Mimi nitakununulia hiyo simu unayotaka," Robby alikuwa anasema.

"Asante Robby. Tom ni mtoto sana, hajui hata kuhonga. Alinipa elfu hamsini akidhani ni pesa nyingi," sauti ya Lisa ilijibu, ikifuatiwa na kicheko kilichonipasua moyo vipande vipande.

Nilihisi damu ikichemka. Nilitaka kuvunja mlango, lakini ule "Mzoefu" wa ndani yangu uliniambia: *Ukivunja mlango hapa, utaonekana mshamba na utapoteza kila kitu. Ondoka kimya kimya, na uwaache na uchafu wao.*

Nilirudi nyumbani nikiwa kama sanamu. Kesho yake asubuhi, simu yangu iliwaka. Ilikuwa Caroline.

"Tom, mbona hupokei simu yangu tangu jana? Nataka kukuona leo jioni, kuna kitu muhimu nataka nikupe," Caroline aliongea kwa sauti tamu, sauti iliyokuwa na faraja ambayo niliihitaji kwa wakati ule.

Niliitazama ile pesa ya Caroline iliyokuwa mezani. Lisa alikuwa msaliti. Robby alikuwa mshindi wa muda. Na Caroline? Caroline alikuwa mlango wangu wa kutokea.

"Nitakuja Caroline. Nitakuja mapema sana," nilimjibu.

Lakini nikiwa najiandaa kutoka, ujumbe wa Lisa uliingia: *"Bby, nimeamka naumwa sana. Naomba unitumie elfu ishirini ya dawa. Nakupenda sana."*

Nilitabasamu kwa uchungu. Safari hii sikutuma pesa. Badala yake, niliandika ujumbe mmoja mfupi: *"Msalimie Robby, mwambie elfu hamsini yangu imetosha kumlipia chumba kwa usiku mmoja."*

Safari yangu ya kuelekea kwa Caroline ilianza, huku kivuli cha Robby kikipotea, lakini kivuli kipya cha usaliti kikianza kutawala maisha yangu.

**ITAENDELEA SEHEMU YA 7...**