Episode 5: Mizinga ya Lisa
Mapigo ya moyo yalinidunda kwa kasi huku nikitazama ujumbe wa Lisa. Nilihisi dunia nzima inanielemea. Lisa amefukuzwa? Kwa ajili yangu? Hata kama Dora alikuwa amepanda mbegu ya shaka moyoni mwangu, sikuwa na ujasiri wa kumuacha mpenzi wangu wa kiapo akitaabika mitaani.
Lakini mfukoni nilikuwa na nauli tu ya kwenda shule na kurudi. Nilikumbuka kauli ya Caroline: *"Nina zawadi yako."* Ule "Uzoefu" wa mjini ulinituma kuwa zawadi ya mwanamke kama Caroline haikosi rangi ya kijani ya noti au msaada wa haraka.
Niliasi shule siku hiyo. Badala ya kupanda gari la kuelekea masomoni, nilipanda daladala kuelekea ofisi za *Numeratorβs Entertainment*. Nilifika nikiwa nimeubeba mwamvuli wa Caroline kama fimbo ya Musa.
"Tom! Karibu sana mtanashati," Caroline alinisalimia huku akitoka kwenye kioo chake cha ofisi. Alikuwa amependaza sana, vazi lake la ofisi likionyesha weledi lakini likiacha mwanya wa kumvutia mwanaume yeyote.
"Asante Caroline. Nimeleta mwamvuli wako," nilisema kwa sauti ya kinyonge, sauti ambayo niliijua itamfanya mwanamke yeyote mkarimu aniulize kulikoni.
"Mbona huna furaha Tom? Kuna nini?" Caroline alinisogelea na kunishika mkono.
"Kuna dharura nyumbani Caroline. Mdogo wangu anahitaji matibabu ya haraka na mimi niko mbali na wazazi," nilidanganya. Katika ulimwengu wa mzoefu, uongo wa "ugonjwa" ndio unaofungua pochi kwa haraka zaidi.
Caroline hakusita. Alifungua droo yake na kutoa bahasha ndogo. "Hii ndiyo ilikuwa zawadi niliyotaka kukupa kama shukrani kwa kampani yako ya juzi, lakini chukua ifanye msaada kwa dharura yako."
Niliifungua bahasha ile; kulikuwa na noti za elfu kumi kumi tano. Laki tano! Macho yalinidunda. Sikuwahi kushika pesa nyingi kiasi hicho tangu nianze shule. "Asante sana Caroline, nitakurudishia."
"Usijali Tom, chako changu," aliniambia huku akinitazama kwa macho yaliyosema mengi zaidi ya maneno. Nilimshukuru kwa haraka na kuondoka nikiwa nimechanganyikiwa.
Nilikimbia hadi stendi ya basi kumtafuta Lisa. Nilimkuta amekaa kwenye benchi la mbao, macho yake yakiwa mekundu kwa kulia. Alikuwa amebeba begi lake dogo la nguo. Aliponiona, alinitumbukia kifuani na kulia kwa uchungu.
"Tom, Mamkubwa ameniambia nisirudi tena. Amesema wewe ni muhuni na utaniingiza matatani," Lisa alieleza huku akitetemeka.
"Usijali mpenzi. Niko hapa," nilimtoa hofu. Niliingia mfukoni na kumpa elfu hamsini. "Chukua hii, kachukue chumba kwenye gesti hii hapa karibu kwa siku mbili, nikutafutie mpango wa kukusaidia."
Lisa alinitazama kwa mshangao. "Tom, umepata wapi pesa hizi zote?"
"Nimefanya kazi ya ziada ofisini, mpenzi," nilidanganya tena.
Siku hiyo nilimwacha Lisa gesti na kurudi nyumbani kwetu. Lakini moyo wangu haukuwa na amani. Pesa ya Caroline ilikuwa mkononi mwangu, na ahadi ya Lisa ilikuwa moyoni mwangu.
Nilipoingia chumbani, nilikuta ujumbe kutoka kwa Lisa: *"Asante Tom, una moyo wa dhahabu. Nimefika gesti salama, lakini bby, nna shida nyingine... nimepoteza simu yangu wakati nakimbia, naomba elfu kumi nyingine ya vocha niongee na mama Tabora."*
Ule ujumbe ulinitia shaka kidogo. Gesti nilimlipia, chakula nilimpa, na sasa anaanza mizinga? Je, maisha ya Dar yameanza kumbadilisha Lisa haraka hivi? Au alikuwa ananijaribu?
Kabla sijajibu, simu iliita. Safari hii alikuwa **Robby**.
"Tom, nimesikia Lisa amefukuzwa. Unadhani utaweza kumtunza kwa pesa zako za pocket money? Huyo mwanamke ni ghali, Tom. Ukishindwa, nicheki nimrudishe kwangu," Robby alicheka kicheko cha ushindi na kukata simu.
Hapo ndipo nilipogundua; changamoto mpya ilikuwa imeanza. Lisa ameanza kuwa na "mizinga," Caroline anasubiri "shukrani" yake, na Robby anavizia anguko langu.
**ITAENDELEA SEHEMU YA 6...**