Episode 11: Asubuhi ya Majuto
Maneno ya Dora yalikuwa kama risasi iliyopita katikati ya moyo wangu. Caroline alinitazama kwa macho yaliyojawa na maumivu, dharau, na hasira ya mwanamke aliyedunishwa. Laki tano yake ilikuwa bado mfukoni mwangu, lakini heshima yangu mbele yake ilikuwa imesambaratika kama kioo kilichopata jiwe.
"Malha?" Caroline alitamka jina lile kwa sauti ya kukata tamaa. "Yule nesi wa Muhimbili? Tom, kumbe wakati mimi nalia kwa ajili yako, wewe ulikuwa unapanga mipango ya kunitumia kama daraja la kuelekea kwa mwanamke mwingine?"
"Caroline, nisikilize..." Nilijaribu kupiga hatua kumsogelea, lakini alinyosha mkono wake kunizuia.
"Usinitiguse, Tom! Harufu ya huyo mwanamke imekuganda kama gundi. Umenidanganya kuhusu mama yako, umenidanganya kuhusu safari ya Tabora. Nilikuamini kuliko mwanaume yeyote niliywahi kukutana naye Dar es Salaam." Caroline aligeuka, akaingia kwenye gari lake na kuwasha injini kwa fujo. Aliondoka kwa kasi, akiacha vumbi likinitanda usoni.
Niligeuka kumtazama Dora ambaye alikuwa amesimama mlangoni akitabasamu kwa ushindi. "Kwanini umefanya hivi, Dora? Kwanini umemwambia kuhusu Malha?"
Dora alicheka kicheko cha kejeli huku akijirekebisha kanga yake. "Tom, nimekuambia mara nyingi, mimi ndiye ninayekujua vizuri. Huwezi kuwa na wanawake wa mjini wenye magari wakati mimi niko hapa nateseka na njaa. Kama mimi sikupat'i, basi hakuna mwanamke mwingine atakayekupata kwa amani katika nyumba hii."
Niliingia ndani na kujifungia chumbani. Nilihisi dunia imenigeuka. Lisa ameshaondoka na Robby, Caroline amegundua uongo wangu, na sasa nimebaki na Malhaβbinti niliyemjua kwa siku chache lakini aliyenipa utamu uliopitiliza.
Niliiwasha simu yangu. Kulikuwa na jumbe nyingi. Moja ilitoka kwa Malha:
*"Mume wangu, umefika salama shuleni? Moyo wangu bado una joto la mahaba yako. Nakusubiri jioni hii nimekuandalia supu ya pweza na dawa za asili za Tanga ili urudishe nguvu. Nakupenda, Tom."*
Ujumbe ule ulikuwa kama maji ya baridi kwenye kidonda. Nilijisikia mnyonge. Nilikuwa nimepoteza kazi ya Caroline, nimepoteza uaminifu wake, lakini bado nilikuwa na "fundi" wa Tanga. Lakini je, Malha alikuwa mkweli? Au naye alikuwa na siri zake?
Nikiwa bado natafakari, namba ngeni ilipiga. Niliipokea kwa unyonge.
"Halo, naitwa **Robby**," sauti ile ilinitoa jasho. "Tom, usidhani safari ya Lisa kurudi Tabora imekuacha salama. Lisa amepata matatizo makubwa hospitalini hapa Tabora, na madaktari wanasema damu yake imeathirika na kitu ambacho mlichanja mlipokuwa Tabora. Wewe pia uko hatarini. Kama hutakuja huku ndani ya saa ishirini na nne, kifo kinakuhusu."
Nilikumbuka kile kiapo cha damu. Nilishika kiganja changu ambapo chale ile ilikuwa. Nilihisi kama inawasha na kutoa joto la ajabu. Je, ni kweli kiapo kile kilikuwa kinaanza kuniua kwa sababu ya usaliti wangu kwa Malha na Caroline? Au Robby alikuwa ananitega nimfuate huko ili animalize?
Niliamua kumtafuta Malha. Alikuwa nesi, labda angetambua dalili za ugonjwa wa "kiapo." Lakini nilipofika Muhimbili kumtafuta, nilikutana na habari iliyonishtua zaidi.
"Malha? Yule nesi wa Tanga?" nesi mmoja aliniuliza kwa mshangao. "Kaka, Malha hayuko kazini leo. Na taarifa tulizonazo ni kwamba yeye si nesi rasmi, alikuwa hapa kwa ajili ya mafunzo ya mwezi mmoja tu, na leo asubuhi amekuja kuchukua vitu vyake akasema anarudi Tanga haraka kwa sababu ana mume wake anamsubiri."
Mume? Malha ana mume? Dunia ilizunguka mara ya pili ndani ya saa sita. Mimi mzoefu, nimeingizwa mjini na nesi feki wa Tanga?
**ITAENDELEA SEHEMU YA 12...**