✦ Matangazo ✦

πŸ“– Story Tamu

Episode 17: Kimbunga cha Saa 12

Giza la Kibaha lilikuwa zito, lakini uzito mkubwa zaidi ulikuwa kwenye mwili wa Bahati. Baada ya hirizi ya shaba kupasuka, ule ulinzi wa mwisho ulikuwa umetoweka. Bahati alikuwa amelala chini, kifua chake kikipanda na kushuka kwa tabu, huku kiganja chake cha kulia kikianza kutoa usaha wa kijivu na harufu ya ajabuβ€”harufu ya udongo wa makaburini.

Afande Mwema, akiwa bado anatetemeka kwa mshtuko wa kurudishiwa utu wake, alirudisha bastola yake kiunoni. Alimtazama Bahati kwa huruma iliyochanganyika na hofu.

"Sikilizeni," Mwema alisema kwa sauti ya mamlaka ya kipoilisi iliyorejea. "Hamna muda wa kupoteza. Kule makao makuu ya polisi Dar es Salaam, kimeundwa kikosi kazi kinaitwa *'Operesheni Tokomeza Utapeli'*. Kiongozi wake ni **Kamishna mstaafu, Mzee Jengua**. Mzee huyo anatoka kule kule Chunya, na anajua siri zote za Mzee Kibatala. Alishawahi kumfunga Kibatala miaka kumi iliyopita kabla haijatoka kwa msamaha."

Musa alishtuka. "Kama Jengua anajua siri za Kibatala, basi anajua kuwa Bahati ndiye funguo ya kila kitu."

"Ndio," Mwema alijibu. "Na agizo ni moja tu: Bahati akionekana, apigwe risasi ya kichwa kwa sababu wanaamini yeye ni 'biohazard'β€”chanzo cha ugonjwa wa ajabu unaoitesa jamii. Lazima mtokomee Chunya sasa hivi. Lakini barabara zote kuu zina vizuizi."

Zubeiri alimtazama Bahati. "Chunya ni mbali, Musa! Kwa hali hii ya Bahati, hatofika Morogoro!"

Bahati alijitahidi kunyanyua mkono wake ulioanza kuoza. Kwa vidole vilivyokuwa vimeanza kukakamaa, aliandika neno moja kwenye vumbi la ardhi: **"LORI."**

Musa alielewa. Njia pekee ya kupita vizuizi vya polisi ni kujificha kwenye malori makubwa ya mizigo yanayoelekea Zambia au Malawi, ambayo mara nyingi hayakaguliwi ndani ya matenki au chini ya maturubai kwa umakini kama mabasi ya abiria.

Afande Mwema aliwasaidia kumbeba Bahati mpaka kwenye kituo cha mafuta cha jirani ambapo malori yalikuwa yamepaki. Kwa kutumia kitambulisho chake cha zamani (ambacho bado alikuwa nacho), Mwema alimshawishi dereva mmoja wa lori la mafuta kuwapakiza kwenye nafasi ndogo iliyoko nyuma ya kiti cha dereva.

"Nenda kijana," Mwema alimnong'oneza Bahati. "Nenda kamalize ulichokianza. Ukishindwa, damu ya watu wote waliouawa Dar es Salaam kwa kusingiziwa itakuwa juu ya roho yako."

Lori lilianza kuondoka, likitembea kwa mwendo wa kobe kuelekea milima ya Kitonga. Lakini ndani ya lile lori, hali ya Bahati ilizidi kuwa mbaya. Saa 12 za kifo zilikuwa zimeanza kuhesabu. Kila saa moja ilivyopita, kidole kimoja cha Bahati kilikuwa kinakufa na kuwa cheusi kama mkaa.

Wakati huo huo, kule Dar es Salaam, Kamishna Jengua alikuwa amesimama mbele ya ramani. "Wametoroka Kibaha," Jengua alisema kwa sauti ya ukali. "Fungeni njia zote za kuelekea Nyanda za Juu Kusini. Huyo mwizi wa nyeti asifike Chunya!"

---
**ITAENDELEA...**

**Kionjo cha Episode 18:**
Lori lao linasimamishwa kwenye mlima wa Kitonga na kikosi maalum. Musa na Zubeiri wanalazimika kufanya uamuzi mgumu: kumtupa Bahati bondeni ili kumuokoa, au kupambana na askari wenye silaha. Je, chale ya Bahati itatoa nguvu ya mwisho ya kujilinda? Usikose sehemu inayofuata: **Kona za Mauti Kitonga.**