📖 Story Tamu

Episode 8:

**Tulipoishia**

“Haipo” aliniambia kwa mshangao, ndipo nikashtuka na kuinuka kutazama

“Haipo nini?” nilimuuliza na kujaribu kujishika katika sehemu zangu nyeti, kiukweli nilshangaa pako flat yaani hakuna kitu, lakini mkojo ulikuwa umenibana, yaani niliogopa kwa kweli “We acha masihara” nilisema huku nikianza kutetemeka halafu nikainuka na kushusha bukta vizuri nikashangaa kweli haipo nikaogopa zaidi baada ya kuthibitisha kwamba haipo kweli

**Endelea**

“Festo” Aliniita Zuhura na kunishika mimi nikawa ninaanza kulia machozi maana ni mateso nilikuwa ninaanza kuyapata “Relax, jilaze kitandani niirudishe kichawi” Aliniambia

“Unaweza kweli?” niliongea naye kwa wasiwasi mkubwa

“Usijali we lala chali”

Ilibidi nifuatie maelekezo aliyokuwa amenipa hivyo nikajilaza chali na kusubiri anifanyie mchakato wa kurudisha “daaaah ikirudi hakika sitarudia tena” niliwaza kichwani mwangu na machozi yalikuwa yananitiririka

Zuhura alianza kuzungusha mikono yake juu ya tumbo langu huku akisema maneno ambayo mimi nilikuwa siyaelewi kabisa, lakini nilihisi hali ya baridi kali ikipita katika maeneo yale lakini haikuweza kurudi

“Daaah Festo, mume wangu amefunga vibaya sana, yaani ameweka kufuli ambayo mimi siwezi kuifungua” aliniambia kwa huzuni na mimi nikazidi kulia kwa uchungu

“Sasa nitakuwaje mimi? Nitakojolea wapi mkojo unanibana Zuhura nisaidie jamani” nilisema huku nikijigeuza geuza kitandani

“Sikiliza, nenda kwa Mangi, mwambie akulete mpaka katika misitu ya miombo, mimi nitawatafuta huko kisha nitawapeleka kwa mganga mwingine ambaye ana nguvu kuliko mume wangu, hapo ndipo utapona” aliniambia na kuniaga haraka haraka kisha akatoka nje

Nilibaki ninalia kama mtoto mdogo, nikawa nawaza maisha yangu yatakuwaje bila ile mashine, niliinuka nikavaa nguo zangu na kuelekea kwa Mangi, nilipofika huko nikamkuta yuko na wateja ikabidi nisubiri pembeni huku nikijikaza mkojo unanitoka mpaka nikaanza kuhisi maumivu ya kibofu

Baada ya nusu saa wateja waliondoka nikamsogelea Mangi na kumuelezea kila kitu kilichotokea, Mangi alishangaa sana na kunicheka mwanzoni lakini alipoona ninalia kweli alinyamaza

“Kijana wangu, nilikuambia uache lakini hukunisikia, sasa mambo yamekuwa magumu” aliniambia “haya panda pikipiki twende huko miombo tukatafute suluhu”

Tulipanda pikipiki na kuelekea kule msituni, tukiwa njiani nilikuwa nahisi maumivu makali sana, ghafla tulipofika katikati ya msitu pikipiki ilizima yenyewe.

Tukiwa tunashangaa pale, ghafla kundi la nyuki wengi lilituvamia, lakini cha ajabu wale nyuki walikuwa wananing'ata mimi tu na kumuacha Mangi salama. Nilipiga kelele za maumivu huku nikikimbia huku na kule

“Kaka nisaidie! Nyuki wananiuwa!” nilipiga yowe lakini Mangi alikuwa amesimama tu akinitazama kwa mshangao

Ghafla moto mkubwa ulitokea na kutuzunguka pande zote, ulikuwa ni moto wa ajabu ambao haukuwa unatoa moshi mwingi lakini ulikuwa na joto kali sana. Mbele yetu, pembeni na nyuma yote ilikuwa ni moto tu.

“MUNGU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NILIZOWAHI KUKUKOSEA KWA KUWAZA KWA KUNENA NA KWA KUTENDA, MAANA NAJUA HUU NDO MWISHO WA MAISHA YANGU, NINAOMBA NIJE NIURITHI UFALME WAKO… AMEN”

Hiyo ilikuwa ni sala yangu ya mwisho kabla sijaona giza nene na kupoteza fahamu.
Matangazo
Matangazo