Episode 2:
Nilibaki nikitafakari kwanini ameniambia kwamba niache kuvaa ule mkufu, niliutoa mfukoni nikautazama kwa muda mrefu lakini nikaurudisha mfukoni
Kichwani mwangu nilijua kuwa ameniambia vile labda katumwa na mganga ili kunipima kama nitaweza kutii masharti, nilirudi nyumbani sikutaka kuendelea kwenda kumuona Mangi, hata hivy akilini mwangu bado niliendelea kuteseka maana nilitaka kuwa tajiri
Nilijilaza kitandani kwa muda murefu mchana maana nilikuwa na njaa ambayo sio ya nchi hii, hivyo basi nilitoka nikaenda hadi kwa mshikaji wangu mmoja aliyekuwa anafahamika kwa jina la Linus halafu nikakaa pale huku nikiwaza namna ya kudusia nipate msosi
Kweli yule jamaa angu alikuwa amesonga ugali na dagaa, nilikula kidogo halafu nikaondoka na kurudi nyumbani kwangu
“Hivi kwanini nisioteshe hata mboga zangu hapa nyumbani?” nilijiuliza “mh subiri”
Maisha kiukweli yalikuwa magumu na yalitosha kunishawishi mimi kuweza kutaka kuuvaa ule mkufu lakini niliogopa sana, nikawaza kwamba kama mke wa mganga ameniambia kwamba mimi nikivaa nakuwa mtumwa, ndipo nilisita kidogo na kuendelea kukaa kitandani
Jioni ilipofika mida ya saa moja hivi niliuchukua ule mkufu nikautazama, ulikuwa unang'aa sana, nikasema liwalo na liwe ninauvaa, ile nauelekeza shingoni hivi nikasikia sauti kwamba kuna mtu anapiga hodi nje ya nyumba
“Karibu” Nilisema na kuuweka mkufu pembeni kitandani halafu nikainuka na kuelekea mlangoni kuchungulia,
Sikuweza kumjua vizuri kwani kulikuwa na giza, hivyo nikapiga hatua muhimu na kuondoka nikaenda moja kwa moja hadi karibu yake, nikakuta ni yule msichana ambaye aliniambia kwamba yeye ni mke wa mganga
“Festo” Ilitoka sauti kutoka kwake
“Nambie”
“Nimetoroka kule msituni, kuna kikao tunakutazama kwenye kioo maalumu cha kuangalia watu ambao ni wateja wa mume wangu, lakini sikiliza nimetazama kwa makini roho yako inaonekana kwamba inataka kuvaa mkufu ule niliokukataza”
“Samahani dada, wewe unaitwa nani”
“Naitwa Zuhura” Aliniambia mimi nikatikisa kichwa kisha akaendelea “Mimi ni Mbulu kutokea huko karatu”
“Ok sawa, Zuhura, mimi nafikiri maisha ni magumu kwangu, sina njia nyingine zaidi ya hii kwani naona ndio njia pekee ya kupata pesa”
“hata ukizipata pesa hizi kamwe hautakuwa na furaha, sikiliza Festo, fanya kazi nyingine” alisema na kunishika mkono kisha akanivuta mkono “Twende nikakuonyeshe kitu”
“Kitu gani? Ngoja nifunge mlango” nilimuambia kisha nikautoa mkono kwake then nikarudi na kuufunga mlango “Lakini Zuu, unafikiri kwamba hawatuoni tukiwa pamoja hivi?” nilimuuliza
“Mkufu wako umeuacha ndani najua, hivyo hawataweza kutuona”
“Ok sawa”
Tuliondoka pale tukiwa pamoja tunatembea, lakini moyoni niliogopa sana maana sikujua kwamba zuhura ananipeleka wapi, tulizidi kutembea
Tulifika katika nyumba ya mangi yule Atanas Mushi kisha tukasimama nyuma ya dirisha lake “Festo” Zuhura aliniita
“Naam”
“mimi ninaondoka kwani kule watanitafuta,” alisema na kunishika kichwani “ithe kuthe nkugure tho kutire lololio fo” alitamka maneno hayo ya ajabu halafu akaniachia “Hapa akija mtu yeyote hatokuona, hivyo kaa hapa utakachokiona utakuja kuniambia asubuhi nikija” aliniambia yule msichana na kuondoka zake
Nilitulia pale mpaka ikafika mida ya saa tano usiku, nilikuwa na njaa hatari lakini nilitulia nione kwamba ni kitu gani alichoniambia, ghafla nilisikia mlango...

Matangazo
Matangazo