đź“– Story Tamu

Episode 1:

Niliteswa sana na maisha baada ya kufiwa na wazazi wangu wote waliokuwa wamefariki katika ajali ile ya MV Spice miaka saba iliyopita, nilichanganyikiwa maana nilibaki nyumbani peke yangu kwa sababu nilikuwa mtoto pekee wa kiume na dada zangu wanne walikuwa wote wameshaolewa na wanaziendesha familia zao

Nilijaribu kumpigia simu dada yangu mmoja ambaye kidogo alikuwa anajiweza nikamuomba mtaji wa shilingi laki mbili nikaanzisha biashara ya kuuza mitumba katika mji wetu mdogo wa Igunga kwa majina naitwa Festo Hamisi.

Baada yaa kuingia katika biashara ya mitumba niliweza kuifanya ndani ya miezi mitatu ikafa ile biashara, kwa sababu nahisi nilikuwa natumia pesa vibaya sana, nilikuwa na mademu wa kutosha katika mtaa wetu wote wakiniita handsome boy na kweli nakubali mimi ni handsome boy lakini nilikuwa sina akili ya maisha kabisa

Dada yangu aliyenipa mtaji alinifokea sana halafu akaamua kunipa tena laki mbili ili nifufue mtaji, lakini aliniambia kwamba nitakuja kumlipa baadaye kwani alikuwa anaamini biashara ile inalipa na uzembe wangu tu ndio unafanya mimi ninaacha kufanikiwa kimaisha

Hata hivyo niliichukua ile pesa nikarudi sokoni lakini hata haikuisha wiki mbili nililetewa kesi ya kutembea na mke wa mtu na nyingine ya kufumaniwa na mwanafunzi, ilibidi nihonge pesa zote ili tu niweze kuyahendo hayo matatizo lakini haikutosha, ya mwanafunzi ilikuwa ni ngumu mpaka ikapelekea mimi kuuza kiwanja nilichoachiwa na baba kwa sh milioni tatu

Dada yangu alinifokea sana akisema nifanye juu chini niweze kurudisha hicho kiwanja la sivyo atanifanyia kitu kibaya,

Stress za maisha zilianzia hapo ndipo nilipoenda kwa mtu mmoja tajiri sana aliyekuwa anafahamika kwa jina la Atanas Mushi, alikuwa ni mchaga mwenye biashara za kutosha hapo Igunga sasa nilitaka akaniajiri

“Mangi ee” nilimuita baada ya kumkuta akinywa bia sehemu fulani

“Niambie kijana angu” aliongea kwa lafudhi fulani hivi ya kichaga kabisa

“asee broo life limetaiti sana naomba unisevu hata kibarua basi “

“hahahaa tutaongea, hivi una namba yangu?” aliniuliza Mushi

“Hapana sina broo”

“chukua sasa” alisema kwa mkato na kuitoa simu yake mfukoni akapokea, ila sikuelewa alichokuwa azungumza maana kilikuwa ni kichaga fulu

Hata hivyo baada ya kumaliza kuongea alinipatia namba yake ya simu nikambipu naye akapata ya kwangu ndipo nikaondoka***

Baada ya wiki moja Mangi alinipigia simu alikuwa anataka mtu wa kwenda kusimamia biashara zake mjini, akaniambia niende lakini ningefanya kwa mwezi mmoja tu niache, mimi sikujali ilimradi ananilipa vizuri, onyo aliyonipa ni onyo pekee kwamba nisiibe chochote kwake ndio tutaelewana

Kwa kweli kutokana na matatizo niliyokuwa nayo niligeuka mtiifu ndani ya mwezi mzima,

Siku moja niliamua kumuuliza mangi ni namna gani anavyofanya mpaka anaweza kuwa na mafanikio makubwa kwenye biashara kiasi kile, mangi alicheka sana sana sana, nikajiuliza tatizo nini

“Ndugu yangu kwani na wewe unataka kuwa kama mimi?” aliniuliza huku akicheka

“Sana broo nieleweshe mimi nitafanya chochote”

“Broo kuna mtaalamu kashikia hizi biashara sio bure hivi hivi, hii ni siri usimwambie mtu, sikiliza, kama utakuwa tayari mimi nitakupeleka kwa huyo mtaalam na ndani ya miezi mitatu tu utakuwa ok”

“mmmh kumbe unatumia mtaalam” niliuliza

“Sikiliza bwashee, unawaona matajiri wakubwa kama kina Bakhresa, Mengi, Manji na kadhalika, yaani wote wale wanatumia utaalamu wa hali ya juu, bila utaalam nina imani kwamba ungekuta washakufa wewe, unacheza na duniaa nini” aliniambia ikabidi nicheke sana sana nilikuwa nacheka ile lafudhi yake ya kichaga kabisa

“usicheke bwanamdogo, sikiliza wewe kama kweli upo tayari mimi ninakupeleka sio mbali hata na wala hamna kafara yoyo”

“yoyote” nilimalizia sentensi

“Aya mimi nikalale eti “aliniambia Mangi

Siku zilizidi kusogea nikasema kwamba haya maisha mbona yanakuwa magumu zaidi, maana nilikuwa nishatoka kwa Mangi tayari, hivyo basi nilijikuta nazidiwa nguvu na ushawishi ukitaka mimi niweze kwenda kwa mganga kwa ajili ya kwenda kutafuta hizo pesa za haraka haraka, nilichukua simu yangu na kumbip mangi maana nilikuwa sina sms wala dakika

Mangi hakupiga, mpaka nkaamua kuinuka na kwenda moja kwa moja hadi katika ofisi yake nikamtazama usoni

“Asee broo”

“niambie”

“Kwa hili life mzee……twende tu unipeleke”

“Umeonaee” aliniambia huku akinyoosha mkono na kuangalia saa

“Ndio broo”

“NItafute saa nne usiku”

***

Ikiwa ni saa nne usiku nilitoka nyumbani na kufunga mlango vizuri nikawahi kwenda moja kwa moja hadi kwa mangi ili nikamuone, nilikuta pia naye amejiandaa vyema na alikuwa ameshavaa hadi koti

Safari ilianza na pikipiki halafu baadaye tukashuka na kuanza kutembea kwa miguu katikati ya msitu, kelele mbalimbali zilisikika zikiwa ni za wadudu na wanyama wasiolala usiku, tulitembea maeneo ya kutisha huku nikiogopa sana eneo lile

“Usiogope, mchumia juani hulia kivuli?”

“kivulini” niliongea kwa uoga zaidi baada ya kusikia sauti ya bundi akilia juu ya mti nikajua hapa mpaka bundi kalia, basi ujue kwamba mimi maisha yangu yameshafika katika tamati kuu

Tulizidi kutembea safari ilikuwa ni ndefu sana, mara nikasikia lindege limenivamia na kunibeba mzima mzima, nilijitahidi kupiga kelele lakini sauti ilikuwa haitoki, nilibebwa kama Kifaranga abebwavyo na Mwewe nikaogopa hadi nikapoteza fahamu

Baada ya dakika kadhaa nilishtuka nikajikuta nimezungukwa na watu watano, nikashtuka kwanza

“Shikamoo” niliongea kwa uoga” huku nikiwatazama wale watu waliokuwa wamevaa nguo nyekundu wote, huku nyuso zao wakifunika kwa vitambaa vyeusi hivyo sikuweza kuviona lakini sauti ilitoka na ilikuwa ya mtu wa makamo kidogo

“hahahaa……tulijua una nia mbaya kuzunguka katika misitu hii ya Miombo” alisema mtu huyo “lakini tumeishukuru mizimu imeweza kutuonyesha kuwa wewe sio mtu mbaya” alizidi kusema mimi nikawa nimetulia huku ninatetemeka

“Festo abdul” ilitoka sauti ya kike nyororo kabisa nikageuza macho na kumtazama anayeongea “Karibu kwa Mganga Kamlenga, tafadhali ukiulizwa kitu chochote utajibu tawire” aliniambia

“hiiiii” nilijikuta naanza kulia baada tu ya kukumbuka kwamba niliyekuwa nimefuatana naye hakuwepo pale “Nilikuja katika msitu huu nikiwa na mtu lakini sijui kama ni mzima”

“Ahhaahahaaaa…..alishafika nyumbani”

“tawire” nilitamka mimi

Nilishangaa mwanga umenipiga usoni na wale watu wanne waliinuka na kunizunguka huku wakiimba nyimbo za ajabu ajabu, wote walikuwa ni wanawake isipokuwa yule mmoja aliyebaki akiwa ameketi, walinizunguka zaidi ya dakika tano, halafu wakakimbia na kuishia ndani ya msitu mimi nikabaki na mtu yule mwanaume tu

Yule mwanaume alifunua uso wake na kuvuta pumzi ndefu “Akontatawireee ambrirrrr” alitamka na kutikisa kichwa chake, kisha akanitazama usoni

“Mimi ndiye mganga mkuu, hao waliokuwa hapo wote ni wake zangu, wao ndio waliokuleta….ahaahaaaa kijana akontatawire akontatawire” alisema mzee yule na kucheka nikaona meno yake yamepungua kidogo mdomoni na kubaki machache nafikiri ni kwa sababu ya uzee

“Kijanaaa”

“Tawireee”

“Ninajua shida yako kubwa ni utajiri” aliniambia mzee yule

“Ndio umeyajua vipi hayo mganga?” niliongea kwa mshtuko

“ahahaaaa, kila mtu ninaweza kutambua shida yake, hivyo basi wewe nimeshajua kwamba una shida hiyo”

“Tawire”

“Sasa sikiliza, nilipoangalia katika nyota wewe hauna wazazi wala mke wala mtoto, wa kutoa kafara….hahahaa” alisema nikashtuka “lakini sasa ninataka nikupe utajiri mkubwa kwa masharti makuu mawili hahahaa”

“Tawire mganga”

“Sharti la kwanza, ni kwamba huruhusiwi kuoa hahahaa”

“Tawire mganga”

“La pili ni kwamba hauruhusiwi kuzaa mtoto hahaaa” aliniambia ikabidi nikubaliane maana nilikuwa na shida, kichwani mwangu nilipanga kabisa nitatumia kwa miaka kadhaa halafu nitaachana na uchawi

“sasa ukifanya hivyo, ukavunja masharti basiiii utajiri wako utapukutika na utakufa haraka sana hahahaa” alisema mganga na kuinuka halafu akavua mkufu wake wa shanga aliovaa shingoni halafu akanikabidhi “Kila mara unatakiwa uuvae shingoni, ukiuvua basi haitasaidia aaaanbrrr” alisema na kupotea yule mganga.

Niliogopa maana mianga yote ilizima nikabaki mwenyewe kwenye giza, nikapiga keleele “Mamaaa” ghafla nikajikuta niko kitandani mwangu, ni kama vile nilikuwa naota

Nilinuka na kuketi kitandani lakini nilipotazama mkononi nilikuwa nimeshikilia mkufu alionipa yule mganga “mh hii mbona ilikuwa kweli jamani?” nilijiuliza na kutoka nje kumeshakucha tayari

Ule mkufu sikuuvaa, niliuweka mfukoni nikatembea hadi dukani kwa mangi ili nikamuoleze kama ni kweli au ni ndoto.

Nilitembea haraka haraka nikiwa nawahi kufika, ndipo njiani nilipokutana na mtoto mmoja mzuri sana akiwa amevaa taiti tu iliyomshika vizuri mapaja yake, “HI” alinisalimia huku akitoa tabasamu nikafanikiwa kuona mwanya kwenye meno yake

“Hi, mambo” nilimsalimia halafu nikapita lakini alinishika mkono

“Vipi sister” nilimuuliza kwa mshangao huku nikiutoa mkono wangu aliokuwa ameushika

“Usiogope, mmi ni mke wa mganga, jana usiku nilikuona umekuja pale kwa mganga nikasema kwamba nitakufuata mpaka huku” alisema na kunikagua katika kifua changu halafu akatoa mkono “Hongera, usiuvae ule mkufu kwani ni kiapo kibaya sana utateseka maisha yako yote, ona jinsi ulivyo mkaka handsome halafu unatafuta hela za kichawi usiwe hivyo mkufu inabidi uutupe usiuvae” aliniambia nikaogopa

“Wewe ni mke wa mganga?” nilimuuliza kwa mshangao maana alikuwa ni bonge la pisi, halafu alikuwa ameumbika

“Ndio kwani sifananii jamani?” aliniuliza

“ndio, hufananii hata kidogo”

“Ok bye, mi ninaondoka, nitarudi kwa muda mwingine, ila zingatia nilichokuambia”

Alianza kutembea na kuondoka huku sehemu zake za nyuma akizizungusha mimi nikabaki nnamezea mate tu……ASEEE
Matangazo
Matangazo