Episode 3:
Nilitulia pale mpaka ikafika mida ya saa tano usiku, nilikuwa na njaa hatari lakini nilitulia nione kwamba ni kitu gani alichoniambia, ghafla nilisikia mlango wa chumba cha mangi ukifunguliwa na viumbe wa ajabu wakaingia ndani huku wakiwa na mapanga mkononi.
Nilishtuka sana nikaanza kutetemeka, niliona viumbe wale wakimvua nguo mangi na kuanza kumkata kata huku mangi akipiga kelele za maumivu lakini hakuna mtu aliyekuwa anamsikia, damu zilikuwa zinamtoka sana na wale viumbe walikuwa wanaziramba zile damu.
Nilishindwa kuvumilia nikaanza kukimbia kurudi nyumbani kwangu nikiwa nalia kwa uoga, nilipofika nyumbani nilijifungia ndani na kuanza kusali japo nilikuwa sijui kusali vizuri lakini niliomba mungu aniepushe na ule mkufu.
Niliuchukua ule mkufu na kwenda kuutupa chooni kabisa maana niliogopa sana kuishia kama mangi, asubuhi na mapema Zuhura alikuja kama alivyoahidi.
“nitakuja kwa muda mwingine” Zuhura aliponiambia vile niligundua kuwa ni mwanamke wa kipekee sana, na hakutaka mimi niishi bila kuwa na pesa, hivyo basi, nilishtuka na kwenda moja kwamoja nikiwa na Baba Fetina kwa ajili ya kuweza kwenda kufanya kazi eneo fulani
“Festo haupo serious” Ba Fetina aliniambia
“Kwanini broo?” nilimuuliza
“Unajua huyo ni mke wa nani?” nilimuuliza kwa mshangao lakini kiukweli ni kwamba nilikuwa najua kwamba yule mwanamke ni wa mganga Kamulenga
“Utakuja kufa wewe” aliniambia
“Nife kwani yule ni mke wa mtu?” nilimuuliza
“Hahaha, yule ni mkee wa mganga mkuu katika misito ya Miombo mzee utakuja kufa wewe, usimuone kapendeza vile yule ni mke wa mtu mbaya sana” alinionya yule broo mpaka nikaanza kujuta lakini mimi nilikuwa sijafanya chochote na Zuhura
“Daaah, sijafanya naye chochote broo, hivyo nitajitahidi tuachane”
“Yaah, boy mbona mademu wapo kibao, ila mke wa mtu ni sumu, halafu mbaya zaidi sio mke wa mtu wa kawaida ni mke wa mganga”
Tulifika katika eneo la kazi, ilikuwa ni shule ya msingi, tulitakiwa kwenda kufunga mabomba ambayo yalikuwa yanatakiwa kuhamishwa, hivyo tulifanya kazi pale kwa muda wa masaa matatu tu halafu tukaondoka huku mfukoni nikiwa nimeshikilia shilingi elfu nane yangu ya fasta bila hata kuumia na kutumia nguvu
Nilienda hadi katika shamba la mzee mmoja ambaye alikuwa akiotesha Mboga mboga nkamwambia aniuzie miche ya michicha nikanunua ya 3000 ambayo ilikuwa miche 120 halafu nikarudi nyumbani nkachukua jembe lang na kuanza kulima sehemu ndogo ya kuotesha miche hiyo
Kwa sababu nyumbani kulikuwa na bomba, haikunisumbua katika suala zima la kunyeshea eneo lile, hivyo nilichukua ndo kama 20 kubwa halafu nikanyesha eneo lile na kuhakikisha pamelowa vilivyo ndipo nikaotesh mboga zangu.
Ilipofika mida ya saa moja jioni niliondoka na elfu mbili mfukoni nikasema niende kwa mama ntilie mmoja kwa ajili ya kula, lakini nilipata wazo la haraka haraka ya kwamba kwanini nisitafute tu unga na dagaa niende nikapike mwenyewe kwenye jiko la kuni huko nyumbani.
Ah niliamua kutembea nikaenda katika duka moja ambalo lilikuwa karibu sana na lile la mangi, sikutamani kwenda kwake kwa sababu nilipata kinyaa kutokana na mambo niliyokuwa nimeona akifanyiwa usiku na viumbe vile vya kishetani
“oya festo ee” Mangi aliniita baada ya kuniona
“Ee kaka, nakuja hapo” nilimjibu halafu nikamuambia muuza duka anipimia unga nusu halafu nikaenda kwanza mangi huku unga ukiendelea kupimwa
Nilipofika kwa mangi, aliniangalia sana usoni halafu akatabasamu, nafikiri alikuwa ananipima kisaikolojia kujua kuwa nilifanikiwa kule kwa mganga
“Broo kwema?” nilimsalimia
“Kwema, umepotea sana mdogo wangu” aliniambia nikatulia nikifikria cha kumuambia
“Hamna nipo broo sema tu mambo yamekuwa mengi”
“Ok vp kule ulifanikiwa?” aliniuliza nikamtazama sana halafu akacheka
“Ndio nilifanikiwa ndugu yangu” nilimuambia
“kwa hiyo sa hivi mambo ni barabara kabisa, hongera kijana wangu” alisema mangi nikatikisa kichwa huku nikimhurumia kwa yale mateso aliyokuwa akiyapata kila siku ili tu awe tajiri
“broo kuna mtu kaniagiza hapo dukani ngoja nimuwahishe” nilimuambia
“Sawa, ila kesho nitafute tuongee”
“Sawa kaka”
Niliondoka nikaenda pale dukani nikachukua unga wangu nikapewa chenji halafu nikaondoka na kwenda kibandani nikanunua vitu vingine kwa ajili ya matumizi ya kupika
Nilirudi nyumbani nikatafuta kuni nikakoka moto halafu nikaweka maji jikoni yakiendelea kuwa sawa, na mimi nilikwa nazichambua zile dagaa ziweze kuwa kitu mwake mwake, ghafla nilisikia kama mtu anakuja akikimbia kule nyumbani halafu nilipoinua macho kutazama niliona ameenda speed na kuingia moja kwamoja hadi katika nyumba yangu ya kulala
Nilishtuka nikawahi kwanza mlangoni, huku nikiwa na uoga wa hali ya juu nikasimama pale na kuokota ukuni “Wewe nani?” nilimuita yeye akiwa amekaa kitandani huku akitabasamu, kumbe alikuwa ni yule mke wa mganga.

Matangazo
Matangazo