Episode 13:
Basi lile la kampuni ya "Nyota ya Alfajiri" lilikuwa limejaa tele, harufu ya jasho na vumbi la njiani ikitanda kote. Mimi na Zuhura tulikuwa tumeketi kiti cha nyuma kabisa, tukiwa tumetuliza nyuso zetu madirishani ili mtu asitugundue. Kila mara basi liliposimama kwenye vizuizi vya polisi au kuchukua abiria, moyo wangu ulikuwa unadunda kwa kasi ya ajabu, nikihisi labda Kamulenga ametuma majini yake kutuzuia.
"Festo, unafikiri tumepona kweli?" Zuhura alinongβona, mkono wake ukiwa umekamata wangu kwa nguvu mpaka nikahisi joto lake.
"Zuhura, Mzee Manyanya ameshatusaidia. Tuamini dawa zake," nilimjibu, japo ndani yangu nilikuwa na mashaka makubwa.
Safari ilikuwa ndefu. Tulipofika maeneo ya pori la akiba la Manyoni, ghafla gari lilianza kutoa milio ya ajabu. Matairi yalikuwa yanateleza kana kwamba kuna mafuta yameimwagika barabarani. Dereva alijitahidi kudhibiti usukani lakini basi liliyumba sana na kusimama ghafla katikati ya msitu mnene, kukiwa na giza nene la usiku.
"Jamani, gari limeharibika! Kila mtu ashuke chini kwanza tuitengeneze!" utingo alipiga kelele.
Abiria walianza kushuka mmoja baada ya mwingine. Mimi na Zuhura tulibaki viti vya nyuma, tukiogopa giza la nje. Ghafla, nikiwa nimekazia macho kioo cha dirishani, niliona kivuli cha mtu mrefu aliyevaa koti refu jeusi likipita kwa kasi ya ajabu nje ya basi. Kivuli kile hakikuwa kinatembea, kilikuwa kinateleza juu ya ardhi.
"Zuhura, umeona kile?" nilimuuliza kwa sauti ya chini sana.
"Nimeona Festo... ni yule msaidizi wa Kamulenga!" Zuhura alishtuka na kuanza kutetemeka.
Punde si punde, kile kivuli kilisimama mbele ya dirisha letu. Sura yake ilikuwa haionekani vizuri, lakini macho yake yalikuwa yanangβaa kama makaa ya moto. Alinyosha kidole chake kirefu na kukigusa kioo cha dirisha letu. Kioo kile kilianza kutoa ufa mdogo uliokuwa unapanuka kwa kasi, na baridi kali ya ajabu ikaanza kuingia ndani ya basi.
"Festo, chupa ya dawa! Mzee Manyanya alitupa dawa!" Zuhura alikumbuka.
Haraka sana, nilichomoa kile kifurushi cha unga mweupe nilichopewa na Mzee Manyanya. Nilikifungua na kuumwaga ule unga kwenye ufa wa kioo. Ghafla, kilitokea kishindo kikubwa cha mlipuko nje ya basi, na kile kivuli kikapiga yowe la kutisha ambalo halikuwa la binadamu, kisha kikatokomea kwenye giza la msitu.
Abiria waliokuwa nje walishtuka na kuanza kukimbilia ndani ya basi kwa uoga. Dereva alijaribu kuwasha gari tena, na safari hii injini iliwaka kwa kishindo kimoja. Tuliondoka eneo lile kwa kasi ya ajabu, huku sote tukibaki kimya kwa hofu.
Tulipofika stendi ya Mwanza asubuhi na mapema, tulishuka tukiwa tumechoka hoi. Hatukuwa na hata senti tano mfukoni, wala nguo za kubadili. Tulijikuta tuko ugenini kabisa, katikati ya jiji kubwa la miamba.
"Tutafanya nini sasa Festo?" Zuhura aliniuliza huku akitazama umati wa watu stendi.
"Tutaanza upya Zuhura. Nitatafuta kazi ya kubeba mizigo hapa stendi, na wewe utatafuta sehemu ya kusaidia kupika kwa mama ntilie. Muhimu ni kwamba tuko salama, na hatutarudi tena kule kwenye giza," nilimwambia kwa ujasiri ambao sikuwa na uhakika nao.
Talianza maisha yetu ya Mwanza kwa kulala kwenye vibanda vya biashara usiku, na mchana tukifanya kazi za suluba. Lakini kila nilipokuwa nafunga macho kulala, nilikuwa naona ile sura ya Kamulenga ikicheka, ikiniambia kuwa deni la pembe yake bado halijalipwa.

Matangazo
Matangazo