Episode 12:
Mzee Manyanya aliichukua ile pembe kwa mikono yake iliyokunjamana, akaishika kwa nguvu huku akimtazama Zuhura na mimi. Jua lilikuwa limeanza kuchomoza vizuri, miale yake ikipenya kwenye matundu ya lile duka la madawa. Harufu ya udi na damu ilizidi kuwa nzito.
“Kijana, umefanya jambo ambalo hakuna mwanadamu aliyewahi kuthubutu kumfanyia Kamulenga. Umeiba roho yake,” Mzee Manyanya alisema huku akicheka kicheko kikavu.
Alichukua kisu kikali kilichotengenezwa kwa mfupa, akaipigapiga ile pembe mpaka ikapasuka katikati. Ghafla, damu nzito na nyeusi ilianza kububujika kutoka ndani ya ile pembe, ikifuatana na nywele ndefu za binadamu na kucha zilizokuwa zimefukiwa humo. Harufu ilikuwa mbaya kiasi cha kutaka kunifanya nitapike.
“Laleni chali, wote wawili!” Mzee aliamuru.
Tulijilaza kwenye mkeka wa kizamani. Mzee Manyanya alianza kuchovya vidole vyake kwenye ile damu nyeusi na kuanza kuipaka usoni kwangu, pale ambapo ule uume ulikuwa umening’inia. Kila tone la damu lilipogusa ngozi yangu, nilihisi kama nachomwa na pasi ya moto. Maumivu yalikuwa makali kiasi kwamba nilitaka kupiga kelele, lakini Mzee alinishika taya kwa nguvu.
“Usipige kelele! Ukipiga kelele, uchawi utarudi mara mbili!” alinguruma.
Alimgeukia Zuhura naye akampaka ile damu usoni kwenye kile kiungo chake. Nilihisi Zuhura akitetemeka mwili mzima, akiziba mdomo wake kwa kiganja ili asitoe sauti. Mzee Manyanya alianza kuimba nyimbo za ajabu, sauti yake ikibadilika na kuwa nzito kama ya radi.
Ghafla, nilihisi kama kuna kitu kinavutwa kwa nguvu kutoka usoni mwangu. Maumivu ya ajabu yalinifanya nione giza, nilihisi ngozi ya uso wangu ikichanika na damu ikinitiririka machoni. Ni kama vile ule uume ulikuwa unanyofolewa na kumerwa ndani ya ardhi. Sikuweza kuvumilia zaidi, nilipoteza fahamu hapo hapo.
Nilikuja kuzinduka saa kadhaa baadaye, nikiwa nimejaa jasho la baridi. Jua lilikuwa limeshakuwa utosi. Kitu cha kwanza nilichofanya ni kugusa uso wangu kwa hofu... nilishtuka! Uso ulikuwa flat, hakuna kitu kilichoning’inia! Nilishusha mkono haraka kwenye suruali yangu, nikashika... mashine yangu ilikuwa imerudi mahali pake, ikiwa na nguvu na uzima kama mwanzo!
“Zuhura! Zuhura amka!” nilimwita kwa furaha nikiwa nalia.
Zuhura alizinduka polepole, akajishika uso wake mrembo. Kile kiungo kilikuwa kimepotea kabisa, na sasa alikuwa amerudi kuwa yule Zuhura mrembo niliyemfahamu. Tulikumbatiana kwa nguvu, tukilia kwa furaha ya kurudishiwa utu wetu.
“Msiwe na furaha sana,” Mzee Manyanya alikatiza furaha yetu. “Kamulenga ameshagundua kuwa pembe yake haipo. Muda wowote atatuma majini yake hapa. Ondokeni sasa hivi, nendeni mbali na mkoa huu. Msiangalie nyuma, na mkifika huko, badilisheni majina yenu.”
Mzee Manyanya alitupa vifurushi viwili vidogo vya madawa ya kujilinda njiani, kisha akatuhimiza tuondoke. Tulitoka mbio kuelekea stendi ya mabasi, huku tukiwa na hofu kuwa kila mtu tunayekutana naye njiani anaweza kuwa ni mjumbe wa Kamulenga.
Tulipofika stendi, tulikuta basi la kwanza likiwa linaanza kuwaka moto kuelekea mkoa wa Mwanza. Hatukuuliza nauli wala hatukuwa na begi lolote, tulijitupa ndani ya lile basi tukijua kuwa huko tunakoenda, ndiko maisha yetu mapya yanakoenda kuanzia.

Matangazo
Matangazo