๐Ÿ“– Story Tamu

Episode 11:

Nilishtuka sana kusikia sharti hilo kutoka kwa Mzee Manyanya. Kwenda kuiba pembe ya Mganga Kamulenga, tena kule alikolala, ilikuwa ni sawa na kujipeleka kifo kinywani. Kamulenga hakuwa mtu wa kawaida, na kitendo cha yeye kunihamishia uume usoni kilionyesha kuwa ana uwezo wa kunifanya chochote anachotaka.

โ€œMzee, hivi hakuna njia nyingine? Kamulenga akiniona atanigeuza kiumbe kingine kibaya zaidi,โ€ nilimwambia kwa sauti ya kutetemeka huku nikigusa ule uume uliokuwa unaningโ€™inia usoni mwangu.

โ€œFesto, ujasiri ndio utakaokuponya. Nikikupa dawa hii ya kupaka miguuni, utatembea bila kusikika na hakuna kiumbe, awe mnyama au binadamu, atakayekuona. Lakini sharti ni moja: Usitoe neno lolote mpaka utakapofika kule, uchukue pembe, na urudi hapa. Ukiongea neno moja tu, utaonekana na hapo ndipo utakuwa mwisho wako,โ€ Mzee Manyanya aliniambia kwa sauti nzito ya mamlaka.

Zuhura alinitazama kwa macho yaliyolowa machozi. Alikuwa bado ana ule uke katikati ya paji la uso wake, jambo lililoniumiza sana moyoni. โ€œFesto, nakuomba ufanye hivi kwa ajili yetu. Mimi siwezi kurudi kule, lakini wewe kwa msaada wa Mzee Manyanya unaweza. Nitakuwa nakuombea hapa.โ€

Nilikubali. Mzee Manyanya alichukua unga mweusi na kunipaka miguuni kuanzia kwenye nyayo mpaka kwenye vifundo vya miguu. Alinipa pia kitambaa cheusi cha kufunika ule uume wa usoni ili usiningโ€™inie hovyo wakati nakimbia.

Niliondoka kwa kasi ya ajabu. Nilishangaa kuona miguu yangu ikiwa mepesi kama manyoya. Nilipita katikati ya kijiji cha wafugaji, mbwa walikuwa wananitazama lakini hawakuwa wanabweka, walikuwa wanapitisha macho kama vile hakuna kitu kinachopita. Hapo ndipo nikaamini dawa ya Mzee Manyanya inafanya kazi.

Nilikimbia usiku kucha mpaka nikafika kwenye msitu wa Miombo, pale kwenye kambi ya Mganga Kamulenga. Moyo wangu ulikuwa unadunda kwa kasi. Nilimwona Kamulenga akiwa ameketi nje ya kibanda chake, akipuliza moshi wa kiko chake huku akicheka na wake zake wengine watatu. Pembeni yake, niliiona ile pembe ya maajabu ikiwa imetundikwa juu ya mlango wa kibanda chake.

Nilianza kusogea taratibu. Nilipita hatua chache tu mbele ya Kamulenga. Aligeuza kichwa chake upande niliokuwa, akavuta harufu ya hewa kama vile anahisi kitu, lakini hakuniona. Niliingia ndani ya kibanda chake taratibu kama kivuli. Ndani kulikuwa na giza na harufu ya damu mbichi.

Niliifikia ile pembe. Niliishika kwa mikono inayotetemeka. Ile naigusa tu, nilisikia sauti ya Kamulenga kwa nje akisema, โ€œKuna harufu ya mtu hapa ndani, wake zangu chukueni mapanga!โ€

Nilishtuka, lakini nikakumbuka sharti la kutosema neno. Niliinyakua ile pembe na kuanza kukimbia kwa nguvu zangu zote. Nilimpite Kamulenga mlangoni, nikamsukuma kidogo bila kukusudia, akatumbua macho akitafuta ni nini kimemgusa. Sikugeuka nyuma, nilikimbia kama upepo kurudi kule nilipotoka.

Nilikimbia mpaka nikafika kwa Mzee Manyanya jua likiwa linaanza kuchomoza. Nilikuwa nimechoka, nimejaa jasho, lakini pembe nilikuwa nayo mkononi.

โ€œMzeeโ€ฆ nimeileta,โ€ nilisema kwa sauti ya kukatika huku nikianguka chini kwa uchovu.

Mzee Manyanya aliipokea ile pembe na kutabasamu. โ€œUmefanya kazi kubwa kijana. Sasa, kazi ya kurejesha utu wenu inaanza rasmi.โ€
Matangazo
Matangazo