✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 16: Mapambano ya Damu na Upendo

Nikiwa ndani ya lile buti la gari, giza lilikuwa nene na hewa ilikuwa nzito. Nilikuwa nasikia tu mlio wa injini na vicheko vya Saraphina na Hussein wakipanga jinsi ya kuniuwa na kutupa mwili wangu baharini ili Sam asipate hata kaburi la kulia. Kidonda changu cha figo kilianza kuniuma kwa kasi, nikahisi kama fahamu zinanitoka.

Ghafla, nilisikia kishindo kikubwa! Gari liliyumba kwa nguvu na kuserereka kando ya barabara. Kishindo cha pili kikafuata, kisha milio ya risasi ikapasua utulivu wa usiku.

"Shuka! Shuka chini sasa hivi!" Sauti ya Sam ilisikika kwa mamlaka na hasira ambayo sijawahi kuisikia maishani mwangu.

Mlango wa buti ulifunguliwa kwa nguvu. Mwanga wa tochi ulinimulika machoni. Alikuwa ni Sam, akiwa ameloa jasho na vumbi, nyuma yake kukiwa na polisi na yule Bibi Mganga kutoka Mpitimbi (Songea) ambaye alikuwa amekuja Dar es Salaam kutoa msaada wa kiroho.

"Tedy! Mpenzi wangu, uko salama?" Sam alinitoa nje ya buti huku akinitetemesha kwa upendo.

Pale pembeni, Hussein alikuwa amepigwa risasi ya mguu na amepiga magoti chini huku akilia. Saraphina naye alikuwa amekamatwa, akijaribu kujitetea kwa sauti ya kilevi na kichaa.

"Sam, nimekuokoa Tedy! Huyu mbwa alitaka kumuua!" Saraphina alidanganya, lakini hakuna aliyemsikiliza. Polisi waliwafunga pingu na kuwatupa kwenye karandinga.

Sam alinikumbatia kwa nguvu sana huku akimshukuru Bibi Mganga. "Bibi, asante kwa kunielekeza huku. Bila wewe, nisingejua Tedy ametoka hotelini kwa siri."

Bibi Mganga alitabasamu na kusema, "Dawa ya moto ni moto mwanangu. Adui hacheki na wewe, na wewe usicheke nae."

Siku inayofuata, maandalizi ya ndoa yalianza haraka sana. Sam aliamua kuwa tusiendelee kusubiri maana maadui walikuwa wengi. Alimsafirisha baba yake kutoka kijijini kuja Dar es Salaam kulipa mahali yote iliyobaki, na taratibu za kanisani zikaanza.

Tulienda ofisini baada ya mwezi mmoja kupita tangu ofisi ichomwe moto. Sam alikuwa ameshakarabati ofisi na kuifanya iwe ya kisasa zaidi. Tulipofika, tulipokelewa na katafrija kafupi cha kutufurahia tumerudi salama.

Wakati wenzetu wanapita kutupongeza kwa kutupa mkono, mwanamke mmoja mfanyakazi mpya wa kitengo cha masoko aliyekuja kuchukua nafasi ya Saraphina, alifanya kitendo ambacho sikupendezwa nacho. Badala ya kumpa mkono Sam, alimkumbatia kwa nguvu.

Yaani unamkumbatia kwa nguvu zote mume wangu mtarajiwa mbele yangu? Niliona ananitania, wivu ulinivagaa ghafla. Nilivuta wigi lake kwa nguvu mbele ya kila mtu!

"Wewe binti, heshima yako iko wapi?" nilifoka huku nikiwa nimeshika wigi lake mkononi.

Minyoosho aliyosukwa vibaya na chogo lake lililoonekana wazi lilionekana vyema. Yule dada alijikuta kakasirika na kuja kunivaa, na mimi nilikuwa namsubiri kwa hamu. "Boss, naona aibu lakini huyu lazima nimnyooshe!"

---
**Inaendelea Sehemu ya 17...** (Ambayo inaelezea pambano hilo na simu ya Mzee Kavishe).