✦ Matangazo ✦

πŸ“– Story Tamu

Episode 15: Majivu ya Usaliti Dar es Salaam

Safari ya kurudi Dar es Salaam haikuwa na vicheko kama tulivyotarajia. Sam alikuwa amekunja kipaji cha uso muda wote, akipiga simu mfululizo kwa wanasheria wake na jeshi la polisi. Mimi nilikaa pembeni yake nikitetemeka, nikiwaza ule moto ulioteketeza ofisi yetuβ€”mahali ambapo tulianzia safari yetu ya upendo na kazi.

"Boss, naona aibu! Kila tukipiga hatua moja mbele, giza linaturudisha nyuma mbili," nilisema kwa sauti ya kukata tamaa tulipokuwa tukishuka kwenye uwanja wa ndege wa JKIA.

Sam alinishika bega kwa nguvu. "Tedy, majengo yanaweza kuchomwa, lakini malengo yetu hayafi. Hussein anachofanya ni kutaka kutuogopesha tukatishe harusi. Hatushindi vita hii kwa kulia, tunashinda kwa kuwa imara."

Tulielekea moja kwa moja ofisini maeneo ya Posta. Moshi ulikuwa bado unavuka, na harufu ya vitu vilivyoungua ilitawala eneo lile. Sam alitazama kiti chake cha enzi ambacho sasa kilikuwa ni majivu matupu. Mafaili ya miaka mingi, mikataba ya watalii, na kumbukumbu muhimu zilikuwa zimepotea.

Polisi mmoja alitufuata na kutukabidhi karatasi ndogo ambayo ilikutwa kwenye lango la ofisi. Ilikuwa imeandikwa kwa herufi kubwa za damu:
> **"HII NI SALAMU TU. HARUSI YENU ITAKUWA MAZISHI YENU. β€” HUSSEIN"**

Moyo ulinidunda. Hussein alikuwa amepoteza akili kabisa. Wakati huo huo, mmoja wa walinzi wa ofisi aliyetujia alikuwa anatetemeka. Alituambia kuwa Saraphina naye haonekani tangu Hussein atoroke gerezani. Wote wawili walikuwa wameungana kufanya unyama huu wa mwisho.

Sam aliamua kutuhamishia kwenye hoteli moja yenye ulinzi mkali (Secret Location) ili kulinda usalama wetu. Lakini tukiwa huko, simu yangu ilipokea picha kutoka kwa namba ngeni.

Ilikuwa ni picha ya nyumba ya wazazi wangu kule Peramiho, ikiwa imezungukwa na watu wenye silaha. Chini ya picha hiyo kulikuwa na ujumbe:
> **"Ukitaka wazazi wako waendelee kuishi, njoo peke yako ufukweni mwa bahari ya Hindi, eneo la Ununio saa tisa usiku huu. Usijaribu kumwambia Sam wala polisi, la sivyo Peramiho itateketea."**

Nilihisi dunia inazunguka. Hussein alikuwa ametuma watu hadi kijijini kwetu ili kuniteka mimi! Nilimtazama Sam aliyekuwa bafuni akioga, nikajua nikimwambia atazuia na wazazi wangu watauawa.

Niliamua kufanya maamuzi magumu. Niliandika barua ndogo ya kwaheri na kuiweka chini ya mto. Nilitoka hotelini kwa siri kupitia mlango wa nyuma, nikapanda taksi kuelekea Ununio. Niliamua kujitoa mhanga ili kuokoa familia yangu na maisha ya Sam.

Nilipofika ufukweni, giza lilikuwa nene na sauti ya mawimbi ilikuwa ikitisha. Nikaona kivuli cha mtu kimesimama karibu na gari jeusi. Alikuwa ni Saraphina, akiwa ameshika bastola, na Hussein akiwa ameketi juu ya gari akicheka kwa dharau.

"Karibu Tedy. Umechelewa kidogo, tulikuwa tunakaribia kutoa amri ya kuchoma nyumba ya mzee wako," Saraphina alisema huku akinitolea macho ya kichaa.

Hussein alishuka na kunikaribia. "Leo ndio mwisho wa huyu 'Boss' wako kukuona. Tutakupeleka sehemu ambayo hata ramani ya dunia haijafika!"

Walinitupa kwenye buti la gari na kuanza kuondoka kwa kasi. Nikiwa ndani ya lile giza la buti, nilihisi kile kidonda changu cha figo kikianza kuniuma kwa kasi kutokana na mshtuko. Nilijua safari hii ni ya kifo... lakini ghafla, nilisikia kishindo kikubwa cha gari likigongwa kwa nyuma!

---
**Inaendelea Sehemu ya 16...**