✦ Matangazo ✦

πŸ“– Story Tamu

Episode 17: Wivu wa Kikata Shombo

Tulipelekeana makofi mfululizo pale ofisini! Kwenye kitengo cha kupigana mbona natisha mimi? Nilimchezeshea vibao vya kukata shombo na ngebe huku nikimfokea kuwa mimi si mwanamke wa kijijini wa kuchezewa mume mtarajiwa. Yeye wa mjini alifikiri hawezi kupigwa, akaanza kutaka kuning'ata, hapo ndipo nilitaka kumnyoosha vizuri kwa magumi ya mbavu.

Bahati nzuri Sam aliniwahi, akanikamata kwa nguvu na kunipeleka ofisini kwake huku nikiwa bado natupa miguu hewani. Kwa nyuma, Saraphina (yule mpya) alikuwa analia kwa kwikwi huku akishika kichwa chake ambacho sasa kilikuwa kipara baada ya wigi kuvuliwa.

"Tedy! Una nini lakini? Hii ni ofisi, siyo uwanja wa michezo!" Sam aliniongelesha kwa ukali mara tu tulipofika ndani ya ofisi yake.

Nilimtazama Sam kwa macho ya hasira yaliyojaa machozi. "Boss, naona aibu lakini huyu dada amezidi! Unamkumbatiaje mume wa mtu mbele ya mke wake? Alitaka kunijaribu, na mimi nimeshamuonyesha kuwa mimi ni kiboko yake!"

Nilipoona Sam bado ana hasira, niliamua kutumia mbinu za kike. Nilimwahi kumwomba msamaha kwa sauti ya upole, nikamkumbatia na kulaza kichwa changu kwenye kifua chake. Nilijua hapo ndipo udhaifu wake ulipo. Nilijidekeza kwa sauti za mahaba mpaka nikahisi hasira zake zimeyeyuka kabisa.

"Haya basi, yameisha. Twende tukapumzike kidogo," Sam alisema huku akitabasamu kwa unyonge.

Tukatoka zetu ofisini na kupanda gari. Sam alinipeleka eneo fulani maalumu kwa watu wanaopenda kuendesha farasi. Nilikua siwezi kuendesha, lakini Sam alikuwa mtaalamu wa mambo hayo. Aliniweka mbele yake kwenye farasi na yeye kukaa nyuma yangu, tukaendesha kwa mwendo wa polepole huku upepo mwanana ukitupuliza.

"Hivi ni mimi Tedy au naota?" nilijisemea moyoni. Maisha haya niliyokuwa nafanyiwa yalikuwa yamepita ukomo wa kufikiria kwangu. Nilizoea kuona mambo haya kwenye tamthilia za Kikorea tu, lakini sasa Boss wangu alikuwa anayafanya kuwa kweli kwangu.

Baada ya hapo, tulipanda boti na kwenda **Kisiwa cha Mbudya**. Huko tulichezea maji, tulipiga picha nyingi sana, na kula samaki wa kuchoma. Jioni tulirudi nyumbani tukiwa na furaha tele, tukimmsahau kabisa yule "kidudu mtu" Saraphina wa ofisini.

Tukiwa tumekaa sebuleni tunapumzika, Sam alipokea simu ya mtu mzito sanaβ€”**Mzee Kavishe**, mmiliki wa kampuni. Mzee alikuwa amepata habari za vurugu za ofisini.

"Vipi hali ya kampuni Sam? Nimesikia kuna wafanyakazi wamepigana ofisini kwa ajili yako," Mzee Kavishe aliuliza kwa sauti ya mamlaka. "Mwanangu amekuwa akinitumia video akidai kuwa uongozi wako umepoteza nidhamu. Anataka nimshushe cheo chako nimpe yeye."

Sam alishtuka. Nilimtazama usoni, alionekana kufadhaishwa sana na swali hilo. Nilijilaumu sana; kwa wivu wangu wa kijinga, nilikuwa nimeingiza kibarua cha mume wangu mtarajiwa kwenye hatari.

"Mzee... ni kweli kulikuwa na mgogoro kidogo," Sam alianza kueleza kwa sauti ya kutetema.

---
**Inaendelea Sehemu ya 18...**