Episode 3: MLANGO WA LAANA
Gari la Taxi lilipaki nje ya geti la Juma kwa kishindo. Moyo wa Juma ulikuwa unadunda kwa kasi kiasi kwamba niliweza kuuona ukicheza kwenye shati lake la gharama. Alikuwa akitembea huku na kule sebuleni, akishika kichwa chake.
"Mwanangu, huyu mwanamke asikanyage humu! Akikanyaga tu, kila kitu kimeisha!" Juma alipiga kelele kwa sauti ya kukata tamaa.
Lakini kabla hajafanya lolote, mlango mkuu ulifunguliwa. Msichana mmoja mrembo sana, akiwa na begi la nguo na macho yaliyovimba kwa kulia, aliingia ndani. Jina lake alikuwa Neema. Alionekana mchovu, na mara tu alipomuona Juma, alijitupa miguuni pake.
"Juma, nimefukuzwa nyumbani! Baba amesema harudi nyumbani mpaka nimuonyeshe aliyenipa mimba hii. Sina pa kwenda, nimekuja kwako mume wangu," Neema alilia kwa kwikwi.
Juma alishtuka kama amegusa umeme. Alimvuta Neema kwa ukali na kumsimamisha. "Ondoka! Ondoka hapa sasa hivi! Nitakupa pesa yoyote unayotaka, nenda kapange hoteli, nenda popote lakini usikae hapa!"
Neema alipigwa na butwaa. "Juma? Pesa? Mimi nahitaji hifadhi, nahitaji baba wa mtoto wangu. Mbona unanifukuza kama mbwa wakati unajua hali yangu?"
Wakati mabishano yakiendelea, ghafla kitu cha ajabu kilitokea. Ile hali ya hewa ya utulivu ndani ya jumba lile ilibadilika. Upepo mkali wa baridi ulianza kuvuma ndani ya sebule, ingawa madirisha yote yalikuwa yamefungwa. Picha kubwa ya Juma iliyokuwa ukutani ilianguka na kupasuka vipande vipande.
Juma alitazama saa yake ya mkononi; ilikuwa imepita saa sita tangu Neema aingie ndani ya eneo la nyumba hiyo. Alijua sharti limevunjwa.
Ghafla, simu ya Juma ilianza kuita mfululizo. Alipopokea simu ya kwanza, sauti ya dereva wake wa Fuso ilisikika kwa hofu:
*"Boss! Fuso namba moja imepata ajali mbaya mlima wa Sekenke! Imegongana uso kwa uso na basi, gari imeharibika yote na mzigo umepotea!"*
Kabla hajakata, simu ya pili ikapiga:
*"Boss, kule Hardware! Moto umezuka ghafla stoo ya rangi, kila kitu kinaungua sasa hivi na zimamoto hawajafika!"*
Juma alidondoka chini kwa magoti. Macho yake yalianza kutoa machozi ya damu. Alimtazama Neema kwa chuki ambayo sijawahi kuiona maishani. "Umeona ulichofanya? Umeona?! Umeyaharibu maisha yangu!"
Neema alikuwa amepoteza fahamu kutokana na taharuki. Mimi nilisimama pale katikati, nikishindwa namsaidia nani. Je, nimsadie Neema aliyepoteza fahamu, au nimsadie rafiki yangu Juma ambaye utajiri wake ulikuwa unaporomoka mbele ya macho yangu?
Lakini hofu kubwa zaidi ilikuja pale mlango wa chumba cha siri cha Juma ulipojifungua wenyewe, na sauti ile ya usiku ikasikika kwa mara ya kwanza mchana kweupe:
**"Mkataba umevunjwa... sasa ni zamu ya kutoa kile ulichoahidi!"**
Usikose Sehemu ya 4...

Matangazo
Matangazo