📖 Story Tamu

Episode 4:

Nilipofika nyumbani usiku ule, sikulala. Kila nikifunga macho, lile "dude" lilikuwa linanitokea kama jinamizi. Nilihisi kama nimeepuka ajali ya mwendokasi ambayo ingenivunja nyonga na kunipeleka wodini moja kwa moja. Ile elfu kumi ya nauli niliitupa mezani, nikaichukia kana kwamba ina nuksi.

Wiki mbili zilipita nikiwa nimepoa kama maji ya mtungini. Hata marafiki zangu wa mjini, akina Shila na Sandra, walishangaa kwanini sitaki kwenda klabu wala "kuchuna" mabuzi. Nilikuwa nimepata kiwewe (trauma) cha maumbile.

"Wewe vipi mwanamke? Mbona umekuwa kama mlokole?" Shila aliniuliza asubuhi moja tukiwa tunapata kifungua kinywa.

"Acha tu Shila, kuna mambo nimeyaona mjini hapa... nimegundua kuna 'fala' na kuna 'majanga'," nilimjibu kwa kifupi, sitaki kutoa siri yangu.

Siku ya kumi na tano, nilijiona nimeanza kurejea katika hali ya kawaida. Niliamua kutoka kwenda kwenye duka moja kubwa la vifaa vya kielektroniki (Electronics Store) pale mjini. Nilihitaji kununua pasi mpya na baadhi ya vifaa vya nyumbani maana nilikuwa nimeanza kuchoka na maisha ya klabu kila siku.

Nikiwa kwenye rafu za pasi, nikichagua kati ya *Phillips* na *Black & Decker*, nilihisi mtu akinitazama. Moyo ulinidunda. Niligeuka taratibu... na hapo hapo nikatamani ardhi ipasuke nimezwe!

Alikuwa yeye! Yule kaka wa gesti!

Safari hii hakuwa amevaa jeans wala ile kaptula yake ya ajabu. Alikuwa amepiga suti ya maana, ya rangi ya kijivu, iliyomkaa vizuri sana. Alikuwa amependeza kiasi kwamba kama nisingekuwa nimeona kile "dude" chake, ningeweza kuanguka miguuni pake na kuomba anioe papo hapo.

"Mrembo wa Fanta Passion?" aliniuliza huku akitabasamu kidogo. Sauti yake ilikuwa tulivu na yenye mamlaka.

Niliganda kama sanamu. "Eh... kaka... habari?" nilijibu kwa sauti ya kukwama, huku mikono yangu ikichezea kamba ya pochi yangu kwa wasiwasi.

"Nzuri tu. Nashukuru kukuona tena ukiwa salama. Naona umependeza leo, huna yale mapozi ya klabu," alisema huku akisogea karibu. Nilirudi nyuma hatua moja bila kujijua, nikihofia ukaribu wake.

Aligundua hofu yangu akacheka kwa sauti ya chini. "Usiogope. Niko hapa kikazi. Mimi ndiye mmiliki wa hili duka."

Nilipigwa na butwaa lingine. Yale maisha ya gesti na klabu yalinifanya niamini ni mzugaji tu au mtu wa mkoani, kumbe ni mfanyabiashara mkubwa! Nilihisi aibu ya ajabu. Nilimkumbuka jinsi nilivyomwita "fala" na jinsi nilivyombenulia mdomo kisa mlija wa soda.

"Samahani sana kaka kwa yaliyotokea... nilikuwa..." nilianza kujitetea, lakini alininyamazisha kwa mkono.

"Haina shida. Jina langu ni Kelvin. Na yaliyotokea kule gesti yashapita. Kila mtu ana hofu zake, na mimi nimeshazoea kukataliwa kwa sababu hiyo hiyo. Huwa najaribu bahati yangu klabu nikitumaini nitapata mwanamke shupavu, lakini wapi," alisema kwa sauti iliyojaa upweke fulani.

"Kelvin... mimi naitwa Tasha," nilijitambulisha kwa mara ya kwanza.

"Tasha, naona unachagua pasi. Chukua hiyo hapo ya mvuke (steam iron), ni nzuri zaidi. Na kwa kuwa tulikutana mazingira ya ajabu, nakuombea punguzo la asilimia hamsini," alisema huku akimwita mfanyakazi wake mmoja.

Niliishia kumshukuru kwa unyonge. Lakini nikiwa naondoka, Kelvin aliniambia neno lililonifanya nisimame: "Tasha, unaweza kunipa namba yako? Safari hii sihitaji 'huduma', nataka tu tuwe marafiki. Nataka unisaidie kitu kimoja."

Moyo wangu uligawanyika pande mbili. Upande mmoja uliogopa lile "dude" lake, lakini upande mwingine ulivutiwa na uungwana wake na utajiri wake. Je, namba nimpe? Na anataka nimsaidie nini?
Matangazo
Matangazo