✦ Matangazo ✦

πŸ“– Story Tamu

Episode 3: Baridi Baada ya Moto

Wiki moja ilikuwa imepita tangu tukio lile la ofisini, lakini kwa Salma, ilionekana kama miaka mia moja. Kila alipofunga macho, alikuwa akihisi miguso ya Karim na harufu ya mustachi wake uliokuwa ukimtekanya. Aliamini kuwa tangu siku ile, uhusiano wao ungebadilika na kuwa kitu cha wazi zaidiβ€”angalau kwa siri.

Lakini ukweli ulikuwa tofauti.

Karim alikuwa amebadilika na kuwa baridi kama barafu ya Japan alikotoka. Alikuwa akimpita Salma koridorini kama vile ni mgeni kabisa. Hakuna tabasamu, hakuna kikonyezo, wala neno la ziada. Alisalimia kwa sauti ya kikazi, "Habari Salma," kisha anaendelea na safari yake bila hata kugeuka.

"Je, nilikuwa ni kituo cha kupumzikia tu?" Salma alijiuliza akiwa amejilaza kwenye kochi nyumbani kwake. Moyo ulimuuma. Alijihisi mpweke na mwenye aibu. Alianza kuwaza kuwa labda yeye si "ligi" ya bosi, na labda Karim alijuta kufanya kile alichofanya na msaidizi wake.

Kila alipojaribu kutengeneza mazingira ya kuongea naye ofisini, Karim alikuwa akijificha nyuma ya milundo ya mafaili na mikutano isiyoisha. Hata kina Warda walianza kumsingizia Salma kuwa amepooza, bila kujua dhoruba inayovuma ndani ya moyo wake.

Hadi asubuhi moja, Salma alipofika ofisini na kukuta kiti cha bosi kiko wazi. Aliuliza huku na kule lakini hakuna aliyekuwa na jibu la kueleweka. Alijihisi mnyonge zaidi; hata kama anaondoka, hakustahili hata kuagwa? Ni kama vile hakuwa na thamani yoyote mbele ya Karim Majid.

Aliposhindwa kuvumilia, alimfuata Mama Mkwawa. "Anti, sijamuona bosi leo, ana matatizo?"

Mama Mkwawa alivua mawani yake polepole, akamtazama Salma kwa jicho ambalo lilionekana kusoma kila siri iliyofichwa moyoni mwake. "Amepata dharura Arusha, Salma. Alinitumia barua pepe asubuhi na mapema kuwa hatafika ofisini leo wala kesho."

Salma alihisi kama amepigwa na butwaa. Arusha? Bila neno? Alirudi mezani kwake na kwa ujasiri wa mwisho, aliamua kuvunja ukimya. Alichukua simu yake na kumtumia ujumbe mfupi: *"Vipi huko, salama?"*

---

**Kionjo cha Sehemu ya 4:**
Baada ya kimya cha dakika kadhaa, simu ya Salma iliita. Ujumbe ulioingia ulimfanya asimame kwa mshtuko: *"Zaidi ya salama mpenzi wangu. Kesho uvae sketi fupi zaidi ya ile ya wiki iliyopita..."* Je, huu ni mwanzo wa mapenzi ya kweli au Karim anacheza mchezo wa hatari? **USIKOSE SEHEMU IJAYO!**