Episode 31:
Basi Baraka akaendelea kutusimulia story yake:
"Nilivyowaza kule katikati ya mji, nikaona nitawapata waliotumika sana. Yule rafiki yangu ndiye akanipa wazo la kwenda kwenye vijiji, nijifanye nawaona halafu naenda kuwatumia kishetani. 😢 Na nikimpa mwanamke mimba akijifungua, mtoto nampa mke wangu jini. Hayo yalikuwa maisha yetu."
"Pole sana kijana. Ikawaje mpaka umefika hivi?" Mchungaji aliuliza.
"Siku moja tulilala, malkia wangu akaanza kuungua huku anasema: *'Amina ananiua!'* Aliungua mpaka akapotea. Baada ya hapo nikazinduka asubuhi, nikatoka nje ya nyumba yangu nilikuwa naongea na simu, ghafla nikakuta nyumba yangu inabomoka! Baada ya hapo kilichoendelea sikujielewa tena, mpaka nafika huku."
"Duuuh! Pole sana Baraka."
"Asante Juma. Naomba unisamehe Amina, nisamehe tafadhali. Ni tamaa tu za hela."
"Sawa, mimi nimekusamehe." Nilimjibu kwa unyonge.
Mchungaji akamshukuru Mungu wakaondoka na waumini, nikabaki mimi, Juma na Baraka.
"Mimi naomba nauli nirudi kijijini kwetu nikajipange na maisha. Ila kabla ya kwenda kwetu, naomba nikamuombe kwanza msamaha mama yake Amina, nilimnyanyasa sana."
Sawa. Tukalala, asubuhi na mapema tukampeleka kwa mama. Alikuwa anafagia uwanja, alivyomuona tu mama akaja na ufagio ili ampige nao Baraka! Alimuogopa, mama akamshika akampeleka ndani. Sijui alimwambia nini, baada ya dakika tano mama alitoka huku amepoa, akaweka vigoda wakakaa.
Baraka alipiga magoti akamuomba msamaha mama. Mama hakuwa na tatizo, akamsamehe. Tukarudi nyumbani, mume wangu Juma akampa laki na nusu, hela ya nauli na kuanzia maisha. Akarudi kwao.
Mimi na Juma maisha yakaenda. Tukawa na maduka mawili, tukawa matajiri wa kijijini. Tukaongeza mtoto mwingine, tukalea kimisingi ya dini mpaka sasa. Mungu hajatuacha, tunaendelea vizuri sana. 👌👌👌
Wale walionibaka (mwanzoni mwa hadithi) walifungwa miaka kumi kila mmoja.
**MWISHO**
> **FUNZO:** Mali za kishirikina sio nzuri. Tujitahidi kutafuta mali halali za bila masharti.
---

Matangazo
Matangazo