Episode 6: Sharti la Utajiri
Hassan alibaki amesimama mlangoni mwa chumba chao, akitazama mlango uliofungwa kwa kishindo. Mikono yake ilikuwa ikitetemeka, si kwa baridi ya alfajiri ya Mwanza, bali kwa maumivu ya kusalitiwa na mwanamke aliyemtoa hospitalini akiwa hajiwezi na kumfanya malkia wa moyo wake.
Saa nne asubuhi, Anifa aliamka akiwa na msisimko wa ajabu. Hakujali kuwa Hassan hakuenda kazini siku hiyo kwa sababu ya msongo wa mawazo. Alianza kupanga nguo zake mpya alizopewa na Mzee Mvule, huku akichezea simu yake mpya ya gharama.
Ghafla, simu ilivuma. Ilikuwa ni namba ngeni, lakini sauti nzito ya Mzee Mvule ilisikika upande wa pili.
> "Mrembo wangu, natumai umelala vizuri. Ile simu ni kionjo tu. Leo nataka nikuhamishie kwenye jumba langu la kifahari lililopo Rock City. Sitaki ukae kwenye kanyumba hako ka kupanga kanakonuka dawa za hospitali. Lakini sharti ni moja... uachane na huyo daktari wako maskini mara moja. Sitaki mwanamke wangu aguse mikono ya mwanaume anayenuka umaskini."
Anifa alimeza mate. Alitazama chumba kile kidogo ambacho Hassan alikuwa amekipamba kwa picha zao za harusi. Alitazama kitanda chao cha mbao cha kawaida. Kisha akawaza kuhusu "Apartment" ya kifahari yenye kiyoyozi na mlinzi mlangoni.
"Sawa mzee, nipe saa mbili tu. Nitakuwa nimefanya maamuzi," Anifa alijibu kwa sauti ya ujasiri wa bandia.
Alitoka nje ya chumba na kumkuta Hassan ameketi sebuleni, ameshika kichwa chake. Hassan alinyanyuka na kumsogelea mkewe kwa unyenyekevu.
"Anifa mke wangu, naomba tuzungumze. Najua marafiki zako wanakupoteza. Ile simu irudishe, naahidi nitafanya kazi kwa bidii zaidi, hata kama ni kufanya 'part-time' kwenye hospitali nyingine ili nikupe maisha unayotaka. Tafadhali usivunje ndoa yetu," Hassan alisihi kwa sauti ya chini.
Anifa alicheka kicheko cha madharau ambacho kilimchoma Hassan kama kisu. "Hassan, huna uwezo huo! Utafanya kazi mpaka uzeeke lakini huwezi kunipa hata robo ya anasa ninazostahili. Leo hii nahama hapa. Sitaki kukuona tena, dume suruali wewe! Umenipotezea muda wangu mwingi kwa visenti vyako vya madafu."
Hassan alidondoka magotini, machozi yakimtoka. "Anifa, mimi ni mumeo! Tuliahidi kuwa pamoja kwenye shida na raha. Uzuri wako utapita, lakini upendo wangu ni wa kweli."
"Upendo hautunzi ngozi yangu, upendo haujazi friji!" Anifa alifoka. Alianza kuchukua mabegi yake na kutupa nguo zote alizoinunuliwa na Hassan sakafuni. "Nguo hizi za mtumba baki nazo, nenda kawape wagonjwa wako huko hospitalini. Mimi sasa ni mwanamke wa hadhi nyingine."
Dakika chache baadaye, gari lilelile la kifahari lilisimama nje. Bi Husna na Bi Zuhura walishuka wakishangilia. "Hapo sasa! Huyo ndiye Anifa tunayemjua. Achana na huyo daktari anayenuka 'spirit', twende kwenye maisha ya asali na maziwa!"
Hassan alijaribu kumzuia Anifa mlangoni, akimshika mkono kwa mara ya mwisho. "Anifa, usiondoke... utakuja kujuta!"
Anifa alimshindilia Hassan kusukuma kwa nguvu mpaka akaanguka kwenye sofa, kisha akatoka nje huku akitingisha nyonga zake kwa madaha. Hassan alibaki peke yake kwenye nyumba iliyokuwa tupu, akitazama mabaki ya nguo na picha ya harusi yao ikiwa imepasuka kioo sakafuni.
Hassan alihisi giza likimzunguka. Moyo wake uliozoea kuponya watu, sasa ulikuwa umevunjika vipande vipande ambavyo hakuna daktari angeweza kuvitibu.
---
**Je, Anifa atafurahia maisha ya kifahari kwa Mzee Mvule, au ndiyo anajitumbukiza kwenye shimo la simba? Na Hassan atafanya nini baada ya kuachwa na mke wake mpendwa? Usikose Sehemu ya 7.**