Episode 2: Mbegu ya Mashaka
Siku chache baada ya mazungumzo na Bi Husna, Anifa alijikuta akiketi sebuleni kwake akiangalia kuta za nyumba yao kwa jicho la tofauti. Picha za harusi yao zilizokuwa zimepambwa kwa fremu nzuri sasa zilianza kuonekana za kawaida sana kwake. Kila alichokiona kilimkumbusha maneno ya marafiki zake kuwa "uzuri wake ni mtaji."
Mchana huo, Bi Zuhura alimtembelea akiwa amebeba mfuko wa rambo uliojaa nguo za gharama na marashi makali. Alijitupa kwenye sofa la Hassan kwa madharau na kuanza kujipepea.
> "Shoga yangu Anifa, hivi kweli utaendelea kuishi hivi? Yaani mpaka leo huna hata gari lako mwenyewe la kwenda sokoni? Angalia Fatuma, yule shoga yetu wa Mbezi, juzi tu kapatiwa gari jipya na 'baba mwenye nyumba' wake. Wewe unategemea mshahara wa daktari ambao mwisho wa mwezi unakatwa kodi nusu!"
Anifa alijaribu kumtetea mumewe, lakini sauti yake ilikuwa na unyonge. "Lakini Zuhura, Hassan ananipenda sana. Ananipa kila anachoweza, laki tano kwa mwezi za matumizi madogo si haba..."
Zuhura alicheka kicheko cha kejeli kilichovuma nyumba nzima. "Laki tano? Shoga, hiyo ndiyo hela yangu ya kusuka rasta tu! Amka Anifa, uzuri wako huu unaweza kukuweka kwenye mjengo wa kifahari na kukupeleka likizo Dubai. Hassan ni mtu mwema, sawa, lakini wema haulipi kodi ya maisha ya kistaa."
Zuhura alipoondoka, alimwachia Anifa gazeti la udaku lililojaa picha za matajiri wa mjini na maisha yao ya anasa. Anifa alikaa kitandani, akijitazama kwenye kioo kikubwa cha chumbani kwao. Alijiona anapoteza muda wake na Hassan.
Saa kumi na moja jioni, Hassan alirejea kutoka kazini akiwa amechoka. Mikono yake ilikuwa na mfuko wa matunda na keki ndogo ambayo alijua Anifa anaipenda.
"Hellow my lovely wife, mke wangu mpendwa!" Hassan alisalimia kwa bashasha akitaka kumkumbatia Anifa.
Anifa hakunyanyuka. Alibaki ameketi, macho yake yakiwa kwenye simu akichati na Bi Husna. "Karibu," alijibu kwa sauti ya mkato, bila hata kutazama usoni mwa mumewe.
Hassan alihisi hali ya hewa imebadilika. "Kuna nini mpenzi? Mbona leo umepoa sana? Mama anaendeleaje huko nyumbani?"
"Hassan, tuache habari za mama kwa sasa," Anifa alifoka ghafla, jambo lililomfanya Hassan ashtuke na keki kumdondoka mkononi. "Nimechoka kusikia habari za wagonjwa na hospitali kila siku. Maisha yetu yamejaa habari za 'pole' na 'asante'. Lini tutaanza kuishi maisha ya maana kama watu wengine?"
Hassan alibaki ameduwaa. Hakuwa amewahi kumuona Anifa mwenye hasira kiasi hicho tangu waoane. "Maisha ya maana gani mke wangu? Kwani tunakosa nini?"
Anifa alinyanyuka, akamtazama Hassan kwa dharau tangu mguuni mpaka kichwani, kisha akaingia bafuni na kufunga mlango kwa kishindo, akimwacha Hassan akiwa amesimama peke yake sebuleni na keki yake iliyopasuka sakafuni.
---
**Je, dharau ya Anifa itafika kikomo gani? Na Hassan atachukua hatua gani kumuokoa mkewe? Usikose Sehemu ya 3.**