Episode 15:
Baada ya tukio lile la usiku kwenye duka la Sheikh Rashid, hofu ilitanda mioyoni mwetu. Pamoja na maombi ya Imamu na ulinzi wa Sheikh Rashid, nilihisi kuwa Kamulenga hatuachi kirahisi. Kila nilipolala, nilihisi harufu ya udi na damu, ishara kwamba bado anafuatilia nyayo zetu kwa kutumia majini yake.
Siku tatu baadaye, hali ya Zuhura ilianza kubadilika. Alianza kupoteza fahamu mara kwa mara, na kila akizinduka, alikuwa anaongea lugha ambazo mimi sizielewiβlugha za kale za kiganga. Macho yake yalikuwa yanageuka na kuwa mekundu kama damu.
"Festo... mtoe... mtoe ndani yangu..." Zuhura alikuwa analia huku akijinyonga-nyonga kitandani.
Sheikh Rashid aliniita ofisini kwake. Uso wake ulikuwa na huzuni kubwa. "Kijana wangu, nimeongea na wazee wa busara. Huyu mganga wenu hajaja kuchukua roho ya mkeo tu, ameweka 'kiapo cha damu' ndani yake. Ile pembe uliyoiiba, ilikuwa na sehemu ya roho ya Zuhura pia."
Nilishtuka. "Inamaanisha nini mzee?"
"Inamaanisha kuwa Zuhura hawezi kuwa huru mpaka kilele cha ile pembe kirudishwe kwenye ardhi alikozaliwa Kamulenga, au Kamulenga mwenyewe afe," Sheikh Rashid alieleza kwa sauti ya chini.
Nilikumbuka maneno ya Mzee Manyanya kuwa Kamulenga ni mwanafunzi wake aliyeasi. Niliamua kuwa siwezi kuendelea kukimbia maisha yangu yote. Nilibeba mkoba wangu mdogo, nikachukua panga langu nililokuwa nimelichovya kwenye maji ya baraka, na kumuaga Sheikh Rashid.
"Naenda kumaliza hii vita mzee. Nilinda mke wangu mpaka nitakaporudi... au mpaka habari za kifo changu zitakapofika," nilisema kwa uchungu.
Safari ya kurudi kuelekea mikoa ya kati ilianza. Wakati huu sikuwa naogopa tena. Hasira ilikuwa imetawala moyo wangu. Nilipofika kwenye msitu wa Miombo, mazingira yalikuwa yamebadilika. Miti ilikuwa imekauka na ndege walikuwa hawalii.
Nilifika kwenye kambi ya Kamulenga usiku wa manane. Nilimkuta ameketi katikati ya moto mkubwa, akiwa hana nguo yoyote isipokuwa ngozi ya chui kiunoni. Alikuwa anapiga yowe la ajabu kuelekea mwezi.
"Umerudi kijana?" Kamulenga aligeuka na kunitazama. Sura yake ilikuwa imeharibika vibaya, nusu ya uso wake ulikuwa umeungua kufuatia lile shambulio la Zuhura kule Mwanza.
"Nimekuja kumaliza mchezo mzee. Mwache mke wangu awe huru!" nilifoka huku nikichomoa panga langu.
"Hahaha! Mkeo ni sehemu ya madhabahu yangu. Ukiniua mimi, na yeye anakufa. Ukiniacha, anaendelea kuwa mtumwa wangu. Chagua kifo unachotaka, Festo!"
Alisimama na kuanza kutoa sauti ya kutisha. Ghafla, ardhi ilianza kupasuka na mikono ya mifupa ikaanza kunitokea miguuni ikinitaka kunivuta chini ya ardhi. Nilijaribu kukata ile mikono kwa panga, lakini ilikuwa mingi sana.
Mganga Kamulenga alianza kunisogelea huku mkononi akiwa ameshika fuvu la kichwa cha binadamu. "Leo, nitaweka uume wako usoni milele, na mara hii nitaupiga msumari wa moto!"

Matangazo
Matangazo