✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 15: Fumanizi la Mfanyabiashara na Maamuzi ya Usiku

Khalfan alipuuza kabisa machozi na magoti ya Zuleha. Alimfukuzia mbali kwa kumpiga teke jepesi la paja na kukimbilia jikoni, ambako alinyakua panga kubwa lililokuwa likitumika kukata kuni. Macho yake yalikuwa yametoa kope za damu, na mishipa ya shingo ilimsimama pwaa. Alitembea kwa hatua za uzito kuelekea mlangoni pa chumba cha akiba cha Jabir.

*BOOOM!*

Khalfan alipiga teke la kwanza kwenye mlango wa chumba cha Jabir. "Jabir! Toka nje wewe msaliti! Toka kabla sijavunja huu mlango nikakukata vipande vipande!"

Ndani ya chumba, Jabir alikuwa amesimama akitetemeka kama jani lililoshikwa na upepo wa dhoruba. Mfanyabiashara huyo aliyekuwa akijidai kwa fedha na magari, sasa alikuwa hana tofauti na panya aliyenaswa kwenye mtego wa chuma.

*BOOOOM!* Teke la pili liliipua mbao ya fremu, na Khalfan alipitisha panga kupitia nyufa hiyo na kukata komeo la ndani. Mlango ulianguka kwa kishindo!

Khalfan alitinga ndani, panga likiwa limeinuliwa juu. Jabir alipiga magoti haraka sana, akainua mikono yake juu huku sauti yake ikimtokana na woga mkubwa: "Khalfan! Ndugu yangu, nisamehe! Usifanye maamuzi ya hasira... nitakupa chochote unachotaka! Nitakupa pesa, nitakupa hata hii nyumba bure!"

Khalfan alimkaribia Jabir na kumshika kola ya msuli wake kwa mkono wa kushoto, huku panga likiwa limemwekea koo: "Heshima ya mke wangu na familia yangu hainunuliwi kwa pesa zako chafu, Jabir! Ulitumia shida zangu ili uninyang'anye mke wangu?"

Zuleha alikimbilia mlangoni akiwa anapiga kelele na kulia kwa uchungu, akihhofia Khalfan atatenda mauaji na kuishia jera. "Khalfan! Tafadhali mwache! Usijitie mkosi mume wangu... watoto wetu watalelewa na nani?"

Ghadhabu ya Khalfan ilishuka kidogo alipowaza kuhusu Karim na mdogo wake waliokuwa wamelala chumbani kwao wakitetemeka kwa hofu. Alimtupa Jabir chini kwa nguvu, kisha akamtemea mate ya dharau.

"Jabir, umeonyesha uanaume wako wa kishoga. Chukua funguo za gari lako uondoke kwenye hii nyumba sasa hivi kabla sijabadili mawazo!" Khalfan alifoka.

Jabir hakusubiri kuambiwa mara mbili. Alikimbia akiwa peku, akaingia kwenye gari lake na kuondoka kwa kasi katikati ya kimbunga na mvua kubwa, akiacha matairi yakilia kwa nguvu.

Khalfan aligeuka taratibu na kumtazama Zuleha aliyekuwa akilia chini kwenye korido. Nyumba hii iliyokuwa hifadhi yao sasa ilikuwa imeingia unajisi na hiana.

---

**UTANGULIZI WA EPISODE 16: Maamuzi Magumu na Virago vya Usiku**

Baada ya kumfukuza Jabir, Khalfan anaamua kuchukua hatua ngumu na ya ghafla usiku huo huo kabla ya kucha. Anaamuru Zuleha kufunganya virago vyao vyote ili kuondoka kwenye nyumba hiyo ya usaliti, bila kuwa na picha kamili wanakokwenda katikati ya mvua. Usikose **EPISODE 16: Maamuzi Magumu na Virago vya Usiku**.