📖 Story Tamu

Episode 2:

Baada ya mjumbe kusimama kama mshale, jasho likanitoka kwapani, si kwa sababu ya joto, la hasha! Ilikuwa ni presha ya kushangaa kile nilichokiona. Yani Tina bana, kawa kama sinema ya bongo, haijaingia sokoni lakini kila mwanaume mtaani kaanza kuizungumzia.

Nilikuwa namtazama huku nameza mate fundo la nguvu. Mi mate yenyewe michungu kama nini. Lile kufuri la pink lilikuwa linanipa wazimu. Nakutaka kuvuruga utaratibu wangu kama kidume chenye msimamo. Nilikuwa nahangaika kama mfamaji ni kubana na kutanua miguu.

Akanitazama kwa tabasamu dogo la kihuni, macho yake yakiwa na ujumbe wa “najua umeona.”

TINA: (Akitabasamu huku akichuchumaa kuokota kitambaa chake kilichokuwa kimeanguka) “Pole Kelvin, mbona umeshtuka kama vile hujawahi kuona msichana kavaa vizuri au umeona nini cha ajabu? Au unataka kuona nini sema uonyeshwe?”

Nikameza mate tena, halafu nikakaa pembeni ya kitanda kama mtu aliyekutwa anatazama movie yenye vionjo vya watu wazima halafu mzazi akaingia ghafla. Nilihisi aibu lakini nilijitahidi kujiweka kawaida.

KELVIN: “Aah, siyo hivyo Tina… ni kwamba hujaelewa mazingira ya huku. Hapa si salama sana… unavyojichelewesha kwa watu kama sisi, unachanganya kabisa ratiba.”

TINA: (Akicheka kifedhuli) “Sasa unataka niondoke ama nikae na hata kama nikibaki unadhani nini kitatokea?”

KELVIN: “Sijui, wewe ndiyo unajua kilichokuleta. Simu ikijaa, nadhani utaondoka siyo?”

TINA: “Au nikae hadi kesho?” (Akirusha rasta nyuma huku ananitazama moja kwa moja machoni)

Weeeeh! Kijasho kilizidi kunitoka. Hapo hapo akanyanyuka na kuanza kupiga hatua kwenda upande wa meza yangu. Alisimama pale na kuanza kuchezea laptop yangu niliyoiweka juu ya meza baada ya yeye kuja.

TINA: “Unapenda movie? Au hapa hadithi zako?”

KELVIN: “Kuna movie na kazi zangu pia. Lakini usijisogeze sana huko bana… vitu vingine ni personal.”

Nilisema hivyo huku nikimgwaya asifungue folda ya “PRIVATE STUFF”, si unajua tena single boy lazima uwe na folder la 'mafunzo ya utu uzima'.

TINA: “Relax bwana, sifanyi tu utani. Halafu we ni mkali sana. Nani kakufundisha kutokuwa friendly na wasichana?”

KELVIN: “Siyo hivyo. Nimeamua kujitunza. Mapenzi ni kifungo cha moyo, tena siku hizi watu wana mambo. Bora nikae kivyangu.”

TINA: “Aaah wacha zako. Hapo nje wanakusema vibaya. Wanasema eti wewe hujui hata wanawake wanavyoshikwa. Unajua walivyosema jana?”

Nikamtazama, nikiwa nimeshtuka kidogo.

KELVIN: “Wamesema nini?”

TINA: “Eti jogoo hapandi mtungi. Eti labda wewe ni shoga au unaogopa wanawake.”

Nilijisikia vibaya, ila nikajizuia. Nilimkazia macho halafu nikamwambia:

KELVIN: “Sikuzaliwa kwa ajili ya kuwafurahisha watu. Siwezi kulala na kila demu ili kuwathibitishia kuwa mimi ni mwanaume. Na kama wewe ndio umekuja kuni-test, ngoja uone.”

Alitabasamu, akapiga kelele ya “heeeh, kumbe kuna moto ndani eeh?” kisha akavuta kiti na kukaa vizuri zaidi. Akaanza kuonesha miguu yake kwa makusudi, sijui kama alikuwa amekuja kupima mashine au kuchaji simu.

Aligeuka na kuniambia kwa sauti ya kimahaba:

TINA: “Mbona unaning'ata kwa macho lakini kwa mdomo husemi? Kama unanitaka sema, life is too short.”

Nilikosa cha kusema, akili yangu ikaanza kupigana na moyo. Kwa upande mmoja nilihisi nafaa kumfurahisha, kwa upande mwingine nikakumbuka mama yangu alivyonifundisha nidhamu, plus vile vibaya nilivyoshuhudia majirani wanavyoharibikiwa kwa mambo ya 'jirani na jirani'.

Tina aliendelea kunizunguka kama simba anayemfuatilia swala. Ghafla akanyanyuka, akaja hadi pale nilipokaa, akainama kunichukua simu yake ambayo ilikuwa karibu na mapaja yangu. Harufu ya mafuta yake ilianza kunukia puani kama radi.

TINA: “Aah… bado haijajaa. Ila nimesikia mtaani wewe ni msafi sana. Ngoja nijiridhishe mwenyewe…”

Akanyosha mkono na kugusa kidogo bega langu. Hapo nikashtuka, nikasimama haraka haraka kama nimepigwa shoti ya umeme.

KELVIN: “Wee Tina, acha hizo bana! Huku ni geto, siyo gesti. Kama umechaji, nenda zako!”

Akasimama, akanikazia macho kama vile anashindwa kuamini kilichotokea.

TINA: “Aisee Kelvin, kumbe hufai kuwa single boy. Unajikaza sana. Wewe ni mume material bwana lakini unakosea style.”

KELVIN: “Naipenda hiyo style yangu. Sina haja ya kuharibu maisha yangu kwa tamaa za muda mfupi.”

Alijifanya kucheka kwa dharau, akachukua simu yake, akavaa slippers zake za pinki, kisha akasimama mlangoni.

TINA: “Sawa. Ila kumbuka, wanaume wanaopendwa sana ni wale wagumu. Tutaonana geto la pili.”

Alisema hivyo huku akitoka, akitikisa makalio kwa makusudi kama vile anasema “ukinikosa utajijua.”

Nilifunga mlango kwa nguvu, nikavuta pumzi kwa shida, kisha nikajilaza kitandani. Moyo ulikuwa bado unadunda kwa kasi kama wa mtu aliyeingia kwenye ring na Mike Tyson.

Nilijitazama kwenye kioo cha kabati, nikajiuliza:
“Hii nyumba ya kupanga sasa inataka kuniingiza mjini. Hawa majirani wa siku hizi bwana… full mitego, full drama.”

Nikiwa nawaza hayo, meseji ikaingia kwenye simu:
“Nimeacha kikoi changu chini ya kiti, kesho nakuja kukichukua. Usikifue!” – Tina

Nikaitupa simu pembeni, nikajifunika shuka, nikasema kwa sauti ya chini:
“Jirani acha ukorofi bana…”
Matangazo
Matangazo