✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 13: AMRI YA GHOROFANI

Cynthia alizama chumbani kama upepo wa kimbunga, kifua chake kikipunda na kushuka kwa kasi ya ajabu chini ya lile dera jepesi. Alikuwa anatetemeka mwili mzima, macho yake yakiwa yamejaa hofu ya kifo, huku akitazama huku na kule kana kwamba wale wahuni tayari wameshaingia ndani ya chumba kile cha master.

"Tino! Tino mpenzi wangu, tuondoke hapa haraka! Tukimbie!" Cynthia alifoka kwa sauti ya kilio huku akimshika Tino mikono yote miwili na kumvuta, akitaka amnyanyue kutoka kitandani.

Tino alikuwa amekaa pembeni ya kitanda, akasubiri Cynthia atulie kidogo. Alimtazama kwa utulivu wa hali ya juu, uso wake ukiwa hauna hata chembe ya hofu. "Tulia Cynthia. Kuna nini kimetokea huko chini?"

"Ni Eddy... Eddy amenipigia simu sasa hivi," Cynthia aliongea huku akitwanga mate kwa uoga, akijaribu kuzuia meno yake yasigongane kwa mtetemeko. "Asha amegundua ukweli wote! Amekuta meseji na picha zetu kwenye simu ya Eddy asubuhi hii. Tino, amekusanya wahuni wa kijiweni, wako njiani wanakuja hapa na mapanga na marungu! Wanasema wanakuja kutuharibu sura na kukufanya wewe kilema kwa sababu ulinikingia kifua jana. Nakuomba Tino, twendeni tukimbilie mlango wa nyuma kabla hawajafika!"

Tino alimsikiliza Cynthia hadi mwisho. Badala ya kushtuka au kukurupuka, alishusha pumzi ndefu, kisha akanyanyuka taratibu. Alitembea kuelekea kwenye kabati lake kubwa la nguo, akatoa suruali ya jeans nyeusi na tisheti nyingine nzito ya mikono mirefu ya rangi ya kijeshi. Alianza kuvaa taratibu, akifunga zipu na mikanda kwa utulivu wa kutisha.

"Tino! Unafanya nini? Huwasikii hao watu wanakuja na silaha? Hii nyumba itavunjwa!" Cynthia alipiga yowe, akishika kichwa chake kwa mikono miwili.

Tino aligeuka, akamtazama Cynthia kwa jicho kali la mamlaka ambayo Cynthia hajawahi kuiona tangu amfahamu. Sura yake ya upole ilitoweka kabisa, ikabaki sura ya mwanaume imara anayemiliki himaya yake kwa jasho na damu.

"Cynthia, nisikilize mimi," Tino aliongea kwa sauti nzito, ya chini lakini iliyojaa msisitizo wa dharura. "Mimi ni mwanaume, na hii ni nyumba yangu niliyoinunua kwa pesa zangu halali. Sijawahi kukimbia tishio lolote maishani mwangu, na sitaanza kukimbia leo kwa sababu ya wahuni wa kijiweni waliotumwa na mwanamke mwenye wivu."

Alisogea mbele, akamshika Cynthia mabega yake mieupe kwa nguvu kidogo iliyomfanya Cynthia atulize mtetemeko wake na kumtazama laivu machoni.

"Wewe unachotakiwa kufanya sasa hivi, ingia bafuni hapo, jifungie mlango vizuri na usitoke nje hata ukisikia kelele gani huku nje. Huu ni ugomvi wa wanaume, na mimi ndio bosi wa huu mjengo. Hakuna msela yeyote atakayekugusa ukiwa chini ya paa langu. Umefanya makosa mengi nyuma, lakini leo nitakuonyesha maana ya kulindwa na mwanaume wa kweli."

Maneno yale ya Tino yalikuwa na nguvu ya ajabu. Cynthia alihisi mwili mzima ukimsisimka kwa mchanganyiko wa hofu na mahaba mazito. Aliona ulinzi na jeuri ya kiume ambayo Eddy hakuwa nayo hata robo. Alitikisa kichwa kukubali amri hiyo, akageuka na kuingia bafuni haraka huku akijifungia latch ya ndani, akibaki akisikiliza kwa hofu kupitia uwazi mdogo wa mlango.

Tino aligeuka, akatembea kuelekea kwenye droo ya siri iliyopo pembeni ya kitanda chake. Alifungua na kutoa kifaa kimoja kizito cha chuma cheusi cha ulinzi (tactical baton) kilichokuwa kikirefuka kikifyatuliwa, kisha akaweka simu yake vizuri mfukoni. Aligeuka na kuanza kushuka ngazi kuelekea sebuleni, tayari kusubiri dhoruba mlangoni kwake.

Akiwa anafika hatua ya mwisho ya ngazi, nje ya geti sauti za pikipiki tatu zilisikika zikipiga breki kali, zikifuatiwa na sauti za wanaume waliokuwa wakifoka kwa ukali na kugonga geti la fensi kwa nondo.

---

**Katika Episode inayofata (Episode 14: Mapambano Getini):** Wahuni wanavunja kufuli la geti la nje na kuingia ndani ya uwanja wa Tino wakiwa na mapanga, wakiongozwa na Asha mwenye hasira. Tino anafungua mlango mkuu na kusimama peke yake mbele yao, huku mapambano ya nguvu na akili yakikaribia kuanza laivu sebuleni. Usikose **Episode 14** hivi punde!