✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 12: SIRI YA SCREEN

Ubaridi mwanana wa AC uliendelea kupiga kwenye miili yao iliyokuwa uchi na iliyolowana jasho jepesi la mahaba. Cynthia alikuwa amelala kifua wazi juu ya kifua imara cha Tino, vidole vyake vikitengeneza mistari isiyoonekana kwenye vile vinyweleo vya Tino. Kila mmoja alikuwa na tabasamu la kuridhika, lakini utulivu huo wa kiparadiso ulikatishwa na sauti ya simu iliyokuwa ikivuma kutoka chini sebuleni.

*Buzzzz... buzzzz...*

Simu ilikuwa inaita mfululizo ndani ya ile pochi ya Cynthia iliyoachwa juu ya kochi. Tino aligeuka kidogo, akatazama saa ya ukutani iliyokuwa inasomeka saa tano na nusu asubuhi.

"Mpenzi wangu, nenda kaangalie simu yako, isije ikawa kuna jambo la dharura," Tino alisema kwa sauti ya chini na ya upole, akimpiga busu jepesi la paji la uso.

Cynthia aliguna kwa uvivu, hakutaka kabisa kuondoka kwenye ule mto wa nyama uliompa utamu wa aina yake. Lakini simu ilipoita kwa mara ya tatu, ilibidi anyanyuke. Alivuta lile dera lake jepesi sakafuni, akalivika kwa haraka bila kuvaa chupi, miguu yake mieupe ikitembea taratibu kuelekea mlangoni. Alishuka ngazi hadi sebuleni na kuifuata pochi yake.

Alipoitoa simu, alikuta jina la *'Eddy'* likimemetuka kwenye kioo cha screen. Hasira zilimpanda mara moja. Alitaka kuikata, lakini kidole chake kikagusa sehemu ya kupokea kwa hasira.

"Wewe mbwa una shida gani na mimi? Baada ya kunidhalilisha na kunikana mbele ya wale wahuni wenzako jana, bado una jeuri ya kunipigia simu?" Cynthia alifoka kwa sauti ya kunong'ona iliyojaa sumu, akitazama juu ghorofani asije akamfanya Tino achafukwe na roho.

"Cynthia... naomba usikate simu, tafadhali nisikilize!" Sauti ya Eddy ilisikika kwa mbali, ikitetemeka kwa uoga na kuwa na haraka. Alikuwa mafichoni. "Jana ilibidi nifanye vile ili kuokoa maisha yangu na yako pia. Yule Asha ni mwendawazimu, angeweza kukuua mwanangu! Lakini sasa hivi niko kwenye matatizo makubwa zaidi."

"Matatizo gani na yananihusu nini mimi?" Cynthia alisonya kwa dharau.

"Yanakuhusu kwa sababu Asha amegundua kuwa Tino alikuwa anadanganya! Ameingia kwenye simu yangu asubuhi hii nikiwa nimelala na kukuta picha zako na meseji zetu za nyuma," Eddy aliongea kwa haraka huku akitwanga pumzi. "Asha amechanganyikiwa kwa hasira. Amewalipa vijana wa kihuni wa kijiweni kwake, na sasa hivi wako njiani wanakuja hapo getoni kwa Tino na mapanga na marungu! Wanajua uko hapo kwa sababu taxi yako ilionekana ikija huko. Wanasema wanakuja kuvunja nyumba na kukuharibu sura kwa wembe, na Tino watamfanya kilema kwa kumsaidia mchepuko wangu! Cynthia, kimbia hapo getoni saa hivi kabla hawajafika!"

Cynthia alihisi miguu yake ikikosa nguvu. Simu ilikaribia kumponyoka mkononi. Yale maisha ya maringo na dharau yaliyomponza jana, sasa yalikuwa yanaleta dhoruba ya damu inayotishia maisha yake na ya mwanaume aliyempa utamu na kumwokoa masaa machache yaliyopita.

"Tinooo!" Cynthia alipiga kelele kwa uoga, akisahau kila kitu na kukimbia ghorofani kuelekea chumbani huku dera lake likipepea, uso wake ukiwa umejaa hofu ya kifo.

---

**Katika Episode inayofata (Episode 13: Amri ya Ghorofani):** Cynthia anamueleza Tino kuhusu hatari inayokuja ya kundi la wahuni wenye silaha waliotumwa na Asha. Wakati Cynthia akitetemeka kwa uoga na kutaka wakimbie kupitia mlango wa nyuma, Tino anabaki ametulia, akivaa nguo zake taratibu huku akionyesha sura ya ukali na mamlaka ambayo Cynthia hajawahi kuiona, akisema maneno yatakayomsisimua mwili. Usikose **Episode 13** hivi punde!