Episode 5: Mtego wa Serengeti
Sam alikaa kimya kwa muda, akichezea kalamu iliyokuwa mezani kwangu. Macho yake yalionyesha uchovu fulani ambao sikuwa nimeuona tangu tukiwa Dodoma.
"Tedy, Saraphina ni mkuu wa kitengo cha masoko hapa kampuni. Ni kweli, familia zetu zinafahamiana na kuna shinikizo kubwa kutoka kwa wazazi wetu tukae pamoja," Sam alieleza kwa sauti ya chini. "Lakini moyo wangu haujawahi kuridhia. Anatumia nafasi yake kunitishia na kunifuatilia kila hatua. Naomba upuuzie maneno yake, fanya kazi yako, mimi nitakulinda."
Nilitikisa kichwa, ingawa moyoni nilikuwa na wasiwasi mkubwa. Nilijua wanawake kama Saraphina hawaachi jambo kirahisi.
Siku za mwanzo kazini zilikuwa ngumu. Saraphina alihakikisha ananipa majukumu mengi kupita kiasi. Alinituma mikoani, ananipa mafaili ya dharura saa kumi na moja jioni, na kila nikipishana naye ananitolea macho ya chuki. Lakini mimi nilikaza moyo; nilihitaji kazi hii ili nisaidie familia yangu na nijiinue kimaisha.
Siku moja, Sam aliniita ofisini kwake saa kumi na mbili jioni, wafanyakazi wengi walikuwa wameshaondoka.
"Tedy, kuna safari ya kikazi ya wiki mbili kuelekea mbuga za wanyama Serengeti na Ngorongoro. Tunapeleka watalii muhimu kutoka nje. Nataka uandamane nami kama msaidizi wangu wa karibu," Sam aliniambia.
Moyo ulinidunda. Safari ya Serengeti na Sam? "Lakini Sam, Saraphina akijua si itakuwa balaa?"
Sam alitabasamu. "Hii ni kazi, Tedy. Na yeye atabaki hapa kusimamia ofisi. Ni fursa kwako kujifunza nyanja za utalii kwa vitendo."
Maandalizi yalifanyika haraka. Siku ya safari, tuliondoka na gari la kampuni tukiwa na kundi la watalii wanne. Safari ilikuwa ya kuvutia sana. Tulipofika mbugani, tulifikia kwenye kambi ya kifahari (Luxury Tented Camp). Usiku ule, tukiwa tumekaa pembeni ya moto wa kambi (campfire), Sam alianza kusogea karibu nami.
"Tedy, unaonekana mrembo sana ukiwa hapa porini. Mwanga wa moto unakurembesha zaidi," Sam alinong'ona.
"Boss, unanichanganya sasa," nilijibu kwa sauti ya utani iliyochanganyika na aibu.
"Nimeshakwambia usiniite Boss tukiwa huku," Sam alicheka. Alinishika mkono na kunitazama kwa namna ambayo ilinitoa pumzi. "Tedy, tangu siku ile kwenye basi, nilijua wewe ni mwanamke wa tofauti. Nataka tuwe zaidi ya bosi na mfanyakazi. Je, unanipa nafasi?"
Kabla sijajibu, tulisikia kishindo cha gari likiegeshwa kwa kasi nje ya kambi. Taa kubwa za gari zilitumulika pale kwenye moto. Mlango wa gari ulifunguka kwa nguvu.
"Sam! Kumbe huku ndiko unakuja kufanya 'kazi' na huyu binti wa kijijini?" Sauti ya Saraphina ilipasua utulivu wa usiku wa Serengeti.
Sote tulisimama kwa mshtuko. Saraphina alikuwa amefika mbugani usiku wa manane, akiwa na hasira kali na macho yaliyovimba kwa kulia na hasira. Alielekea upande wangu huku amenyoosha kidole.
"Wewe Tedy, nilikuonya! Leo utajua kwanini mimi naitwa Saraphina!"
Alinyanyua mkono kutaka kunizaba kofi, lakini Sam aliwahi kuushika mkono wake kwa nguvu. "Saraphina, imetosha! Unafanya nini hapa?"
"Nimekuja kuchukua kilicho changu, Sam! Na huyu mdudu lazima aondoke usiku huu huu, la sivyo nateketeza kambi nzima!" Saraphina alifoka huku akitoa chupa ya kitu kinachoonekana kama petroli kwenye begi lake.
Aibu ilinizidi. Nilijiona mdogo sana mbele ya watalii waliokuwa wameanza kuchungulia nje ya mahema yao. Nilitamani ardhi ipasuke nimezwe.
---
**Inaendelea Sehemu ya 6...**