Episode 12: Kivuli cha Ushirikina Nyumbani
"Mume wangu, mwanangu... nakufa jamani!" Mama Sam alikuwa akigaagaa chini huku akishika koo lake kama mtu anayekabwa na mikono isiyoonekana. Sam alipagawa, alimbeba mama yake na kumuegesha kwenye kochi huku akipiga kelele za kuomba msaada.
Mimi niliinama haraka na kukivuta kile kitambaa cheusi kilichokuwa chini ya kiti. Kilikuwa kimefungwa kwa kamba za manyoya ya kuku, na ndani yake kulikuwa na picha yangu na ya Sam ikiwa imetobolewa sindano kwenye macho. Moyo ulinidunda kwa kasi. "Boss, naona aibu! Huku mjini pia kuna mambo haya?" niliwaza huku nikitetemeka.
Baba Sam alikinyaka kile kitambaa kwa hasira. "Huu ni mchezo wa yule kimwana! Alisema nitarudi kwake kwa magoti, na asiponipata mimi, basi familia yangu haitakaa iwe na amani!"
Mzee alikimbia nje na kurudi na chupa ya mafuta ya upako ambayo alikuwa amepewa kanisani. Alianza kumpaka mkewe huku akisali kwa sauti kuu. Baada ya dakika kumi za mapambano ya kiroho, Mama Sam alitulia na kuvuta pumzi ndefu. Alizinduka na kuanza kulia kwa uchungu.
"Sam mwanangu, nisamehe. Yule mwanamke alikuja hapa asubuhi akijifanya anataka kuomba msamaha, kumbe amekuja kupanda mbegu za mauti," Mama Sam alieleza huku akitetemeka.
Sam alisimama na kukaza taya zake. Alinitazama mimi kisha akamtazama baba yake. "Baba, tangu leo, hakuna mwanamke mwingine atakayekanyaga hapa zaidi ya Tedy. Na yule mwanamke (kimwana), nitaenda kumshughulikia kisheria kwa kuingilia amani ya familia yetu."
Siku hiyo tulishinda pale nyumbani tukifanya maombi na kusafisha nyumba. Sam alitoa kadi ya benki yenye milioni tano na kuwapa wazazi wake kama mtaji wa kuanzisha duka kubwa la bidhaa za jumla ili wasitegemee tena pesa za mafao ambazo zilikuwa chanzo cha migogoro.
"Tedy, sasa tuko huru," Sam aliniambia tulipokuwa tunarudi nyumbani kwetu usiku ule. "Baraka za wazazi wangu tunazo. Kesho, tunakata tiketi ya ndege. Tunaenda Songea, Peramiho!"
Safari ya kuelekea Songea ilianza alfajiri ya siku iliyofuata. Tulishukia uwanja wa ndege wa Ruhuwiko, kisha tukachukua gari mpaka Peramiho. Kufika kijijini kwetu, watu walishangaa kuona gari la kifahari likiingia kwenye vumbi la kijiji.
Kaka yangu (yule aliyekuwa ameiba kampuni) alitupokea kwa unyenyekevu mkubwa. Alikuwa ameshajirudi na kuanza kulima mashamba ya wazazi. Wazazi wangu walitoka nje, wakishangaa kumuona binti yao Tedy amependaza na anaambatana na kijana mtanashati kama Sam.
"Baba, Mama, huyu ndiye Sam. Ndiye bosi wangu, na ndiye mtu anayetaka kuwa mume wangu," nilimtambulisha kwa aibu.
Wazazi walifurahi sana. Kuku wa kienyeji walichinjwa na sherehe ndogo ikaanza. Lakini wakati tunaendelea na mazungumzo ya posa, rafiki yangu wa zamani wa kijijini aitwaye **Vick** alipita pale nyumbani. Aliniona na Sam, na macho yake yalijaa husuda na chuki.
"Ohoo! Tedy umerudi na mzungu mweusi? Hongera sana," Vick alisema kwa kejeli kisha akaondoka akicheka kicheko cha ajabu.
Nilihisi baridi ghafla. Nilijua Vick tangu tukiwa shule ya msingi; hakuwa na heri na mtu yeyote anayepiga hatua. Usiku ule, tukiwa tumelala, nilianza kusikia sauti za ajabu zikiita jina langu nje ya dirisha...
---
**Inaendelea Sehemu ya 13...**