✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 20: Tamati ya Pendo la Shemeji

"Izzochapa... mimi ni mjamzito," Sasha alinong'ona huku akinitazama kwa macho yaliyojaa mchanganyiko wa hofu na ushindi. "Mimba hii ni yako, na ina umri wa mwezi mmoja na nusu sasa."

Kauli hiyo ilipenya masikioni mwangu kama sumu ya hatari. Tumbo lilinitakata! Mwezi mmoja na nusu uliopita ndio ulikuwa wakati ule tuliokuwa tukifanya mchezo wetu wa siri jikoni na uvunguni kabla fumanizi halijatokea. Mimba hiyo ilikuwa ni ushahidi usiofutika wa ushetani wetu.

Siku zilizofuata zilikuwa za giza nene. Mzee aliporuhusiwa kutoka hospitali, aliamuru kuitishwa kwa mara ya mwisho mkutano wa familia nyumbani kwangu ili kutoa hukumu ya mwisho kabla hajatutenga kabisa.

Zainabu alikuja akiwa amefuatana na wazazi wake. Uso wake ulikuwa umetulia lakini ulionyesha wazi kuwa alikuwa ameshakata tamaa na maisha ya ndoa yetu. Alipomsikia Sasha akitangaza kuwa ni mjamzito na mimba ni yangu, Zainabu hakulia wala kupiga kelele. Alivua pete yake ya ndoa taratibu kutoka kidoleni, akaiweka juu ya meza mbele yangu.

"Izzochapa... kuanzia leo, mimi na wewe hatuna uhusiano tena," Zainabu alisema kwa sauti ya baridi iliyoingia ndani kabisa ya mifupa yangu. "Kulia kwangu kumeisha. Nakutakia maisha mema na mkeo mpya pamoja na mtoto wenu."

Mzee alisimama, akamshika Zainabu mkono na kumtazama Sasha kwa ukali uliotawaliwa na simanzi kubwa: "Sasha... kuanzia leo hutakuwa mwanangu tena. Umechagua tamaa ya mwili badala ya heshima ya familia. Baki na huyo mwanamume uliyemnyang'anya dada yako!"

Wazazi waliondoka na Zainabu, wakituacha mimi na Sasha tukiwa tumesimama katikati ya sebule ile iliyokuwa pweke na yenye baridi kali.

Miezi ilipita haraka. Maisha ya mimi na Sasha hayakuwa tena ya furaha kama tulivyodhani. Hofu na majuto vilianza kutula taratibu. Kila tukitazamana, badala ya kuona mahaba, tuliona sura ya Zainabu na laana ya wazazi wetu. Sasha alijifungua mtoto wa kiume, lakini badala ya kuleta furaha, mtoto huyo alikua akitukumbusha kila siku usaliti wetu.

Rehema naye ndoa yake ilivunjika baada ya Afande Komba kumfukuza kwa aibu, na akahama mtaa huo kabisa.

Leo hii, nimeketi peke yangu barazani nikiwa nimeshika kinywaji kikali. Nikiangalia nyuma, naona jinsi tamaa ya muda mfupi ya mwili ilivyoharibu maisha ya mwanamke aliyenipenda kwa dhati, ilivyosambaratisha familia, na kunifunga kwenye maisha ya majuto na shemeji yangu ambaye hatuwezi tena kuangaliana machoni kwa amani.

Pendo la shemeji halikua na maana yoyote zaidi ya moto uliotuteketeza wote.

---

**MWISHO KABISA (THE END)**