Episode 16:
Ilipoishia, Mkuu wa Shule aligundua kuwa Baraka amemtangulia kutoa gundi ya Asha, akatoa onyo la kutisha kuwa maisha yao ya shule yamefika kikomo. Asha alirudi bwenini akilia na kuanza kuhisi mabadiliko mwilini mwake.
**SONGA NAYOβ¦.**
Siku tatu zilipita tangu tukio lile la ofisini kwa Mkuu. Asha alikuwa akiishi kwa wasiwasi mkubwa, kila kengele ikigonga alihisi labda ni wito wa kwenda kufukuzwa shule. Baraka naye alikuwa amepoteza amani; hakuwa tena yule kijana mchangamfu wa darasani. Kila wakikutana, walitazamana kwa huruma na hofu, wakijua kuwa bomu lilikuwa likisubiri kulipuka.
"Asha, unajisikiaje leo?" Baraka alimnong'oneza wakati walipokuwa wakitoka chakula cha mchana.
Asha alishika tumbo lake kidogo, uso wake ukiwa umepauka. "Baraka, sielewi. Tangu usiku ule... asubuhi naamka na kichefuchefu sana, na harufu ya chakula cha shule inanifanya nitapike. Nahisi kuna kitu hakiko sawa."
Baraka alishtuka, akamshika mkono Asha kwa siri nyuma ya ukuta wa bwalo. "Huwezi kuwa na mimba kwa mara moja tu, Asha. Labda ni msongo wa mawazo kwa sababu ya Mkuu."
Lakini kabla hawajaendelea na mazungumzo yao, sauti ya spika ya shule ilisikika: **"Wanafunzi wote kusanyikeni uwanjani sasa hivi! (Assembly!)"**
Moyo wa Asha ulipiga "paa!". Walielekea uwanjani huku miguu ikiwalemea. Mkuu wa Shule alisimama kwenye jukwaa akiwa na Mwalimu wa Nidhamu, Mwalimu Ngonyani. Uso wa Mkuu ulikuwa na tabasamu la ushindi, lakini macho yake yalikuwa ya baridi sana.
"Leo tuna jambo la kusikitisha," Mkuu alianza kuhutubia. "Kuna wanafunzi wameamua kugeuza shule hii kuwa danguro la mahaba. Wamevunja sheria na maadili, na sasa wanatakiwa kuwa mfano kwa wengine."
Mkuu alinyamaza kidogo, akatazama upande waliosimama Asha na Baraka. "Asha na Baraka! Njooni mbele hapa!"
Shule nzima ilianza kunong'ona. Asha alijihisi kama anataka kuzimia, miguu ilikuwa haina nguvu, lakini Baraka alimshika mkono kumtia moyo wakatembea mpaka mbele ya jukwaa. Wanafunzi wenzao walikuwa wakitolea macho, wengine wakicheka na wengine wakihuzunika.
"Hawa wawili walikutwa usiku wa manane katika mazingira ya kutatanisha kwenye jengo la maabara," Mkuu alidanganya kidogo ili kuhalalisha adhabu yake. "Na kwa mamlaka niliyopewa, nawasimamisha masomo kuanzia sasa hivi (Suspension) mpaka bodi ya shule itakapoketi kutoa maamuzi ya kuwafukuza kabisa."
Mwalimu Ngonyani alichukua viboko na kuanza kuwatandika mbele ya wanafunzi wote kama sehemu ya "nidhamu". Asha alikuwa akilia kwa uchungu, sio kwa sababu ya viboko, bali kwa sababu ya ndoto zake za masomo kuanza kufutika. Lakini katikati ya maumivu yale ya viboko, Asha alihisi kichefuchefu kikali kikipanda...
Ghafla, Asha alijikuta anatapika mbele ya jukwaa, mbele ya Mkuu wa Shule na wanafunzi wote. Alitapika mpaka akabaki anaugulia.
Mkuu alimsogelea na kumtazama kwa dharau. "Kumbe tayari mmeshajaza na choo? Mwalimu Ngonyani, mpeleke huyu binti hospitali ya shule akapimwe. Kama ana mimba, basi hata bodi haitahitajika, anafukuzwa leo leo!"
Baraka alijaribu kumtetea Asha lakini alipewa kipigo kikali na viranja. Asha alipelekwa hospitali huku akiwa hajitambui kwa maumivu na aibu. Daktari wa shule alichukua sampuli ya mkojo na baada ya dakika kumi, alitoka akiwa na karatasi mkononi huku akimtazama Mkuu wa Shule kwa mshangao.
"Vipi daktari? Ana mimba?" Mkuu aliuliza kwa shauku ya kutaka kumkomoa Asha.
Daktari aliguna kidogo, kisha akasogea karibu na Mkuu na kumnong'oneza jambo ambalo lilimfanya Mkuu abaki ameduwaa na karatasi imdondoke mkononi...

Matangazo
Matangazo