✦ Matangazo ✦

πŸ“– Story Tamu

Episode 5: SHIMO LA SIRI NA GIZA LA MBAGALA

Mambo yanazidi kuwa magumu! Mjomba Juma amefika Mbagala akiwa na kikosi chake cha mauaji, lakini hajui kuwa ulinzi wa Sofia unatoka ulimwengu mwingine.

Mwangaza wa taa za gari za Mjomba Juma ulimulika ukuta wa chumba alichopanga Sofia. Sofia alikuwa amerudi ndani na kujifunika shuka, moyo wake ukidunda kwa nguvu kiasi cha kuhisi kuta za kifua chake zinauma. Alikuwa ameshatii sauti ya mama yakeβ€”almasi zilikuwa chini ya udongo, mita chache kutoka alipo.

"Vunja mlango!" Sauti ya Mjomba Juma ilinguruma nje.

*BOOM!* Mlango mdogo wa mbao ulipasuka na kuanguka ndani. Juma aliingia akitanguliwa na vijana wake wawili wenye bastola. Alimkuta Sofia amekaa pembeni ya kitanda, macho yake yakiwa yamejaa hofu lakini ndani yake kukiwa na ujasiri usio wa kawaida.

"Hatimaye... binti mkaidi," Juma alisema huku akitabasamu kwa kejeli. "Umedhani unaweza kukimbia damu yako mwenyewe? Ziko wapi?"

"Ziko wapi nini, Mjomba?" Sofia aliuliza kwa sauti inayotetemeka.

Juma alimshika taya kwa nguvu na kumuinua juu. "Usicheze na mimi! Almasi za baba yako! Nazitaka sasa hivi la sivyo utaungana na mama yako huko aliko!"

Sofia alistuka. "Mama... yuko wapi? Mjomba, umemfanya nini mama?!"

Juma alicheka kicheko cha kikatili. "Mama yako ameshalala mapema sana. Sauti yake haitakusaidia tena. Niambie zilipo kabla sijapoteza uvumilivu!"

---

Wakati huohuo, kule nje kwenye mti wa mwembe ambapo Sofia alizika almasi, mambo ya ajabu yalianza kutokea. Udongo ulianza kutikisika wenyewe. Harufu nzito ya pafyamu ya waridi ilitanda eneo lote la uwanja ule.

Mmoja wa vijana wa Juma aliyekuwa akilinda gari alihisi baridi kali mgongoni mwake. Aligeuka na kuona mwanamke amesimama karibu na mti wa mwembe. Alikuwa amevaa nguo nyeupe, lakini uso wake ulikuwa umefichwa na nywele ndefu.

"Wewe! Unafanya nini hapa?" Yule kijana alitoa bastola.

Yule mwanamke hakujibu. Alinyoosha mkono wake polepole... na ghafla, matawi ya ule mti wa mwembe yalianza kurefuka kama nyoka na kumfunga yule kijana mikono na miguu. Alishindwa hata kupiga kelele, matawi yaliziba mdomo wake na kumvuta juu ya mti gizani.

---

Ndani ya chumba, Juma alikuwa anaanza kupekua kila kona. Alitupa magodoro chini, akavunja sanduku la Sofia, lakini hakupata kitu.

"Mzee! Kuna kitu hakiko sawa nje!" Kijana mwingine aliingia akitokea nje, uso wake ukiwa mweupe kama karatasi. "Sule amepotea... na kuna ukungu wa ajabu umeanza kutanda."

Juma alimtazama Sofia kwa hasira. "Unatumia uchawi wa mama yako? Hutanizidi nguvu!"

Juma alimvuta Sofia kwa nguvu kuelekea nje. "Kama huzisemi zilipo, nitakuchinja hapa hapa mbele ya huyu mzee mwenye nyumba!"

Walipotoka nje, walikutana na ukungu mzito wa kijivu. Sofia alitazama kuelekea ule mti wa mwembe. Aliziona almasi zile zikiwa zimejitokeza juu ya udongo zenyewe, zikitoa mwanga hafifu wa kijani.

"Zile pale!" Mjomba Juma aliziona. Alimwachia Sofia na kukimbia kuelekea kwenye ule mti kwa tamaa.

Lakini alipofika hatua mbili kabla ya kuzishika, sauti ya Mama Sofia ilisikika hewani, ikivuma kama radi: **"GUSA, UONE MOTO WANGU!"**

Juma alisimama ghafla. Macho yake yalitoka nje kwa hofu alipoona kivuli cha shemeji yake (Mama Sofia) kikitokea mbele ya zile almasi. Kivuli kile kilikuwa na macho ya moto.

"Wewe ni mfu! Huwezi kunifanya kitu!" Juma alifyatua bastola yake kuelekea kwenye kile kivuli.

Lakini risasi zilipogonga kile kivuli, ziligeuka na kumrudia Juma. Risasi moja ilimparaza begani, ikimfanya aanguke chini akipiga kelele. Vijana wake, walipoona vile, walitupa silaha zao na kukimbia hovyo kuelekea kwenye magari, wakimwacha tajiri wao peke yake gizani.

---

**Je, Mjomba Juma ataweza kutoroka kwenye mikono ya mzimu wa Mama Sofia? Na Sofia atafanya nini akigundua kuwa mama yake ameuawa kikatili?**

**Usikose Episode 6!**